Wanaume wanaingia kwenye mahusiano na wanawake wasio wapenda ili mradi tu wamekubaliwa na kupata uhakika wa ngono na wanawake nao wanatoka na wanaume wasio wapenda ili mradi tu wawe na pesa nyingi na kuwahudumia basi 🤔 .
Kama kila muda unakaa mwenyewe na kujiambia...
" Leo ni mwisho nimechoka dharau za huyu Mwanamke "
Ila akija tu na kukupa kinyambisi unasahau jinsi anavyokufedhehesha
Umeruhusu kichwa cha chini kikuamulie
Endelea kuteseka Mwanaume mpumbavu na dhaifu
#KuwaNiceGuyniUgonjwa
Hulazimiki kujieleza kwa kila mtu.
‘Hapana’ isiyo na maelezo inaweza kumtosha.
‘Sijui’
‘Sifahamu’
‘Siwezi’
‘Hali hairuhusu kwa sasa’
‘Wakati mwingine’
ni jibu linalojitosheleza kwa mtu usiyelazimika kujieleza kwake. Ukiongeza maelezo zaidi unaharibu.
Huwezi kuwa na furaha ukamfanya mwingine aumie. Huwezi kuwa na matumaini unawakatisha tamaa wengine. Huwezi ukawa na amani halafu ukawakosesha wengine amani. Unagawa ulichonacho.
Tunatumia nguvu kubwa kujenga ukamilifu tusiokuwa nao, kuonesha sura za tabasamu tusizokuwa nazo.
Hadharani una furaha, sirini unalia.
Hadharani ni maarufu, sirini ni mpweke.
Hadharani ni jasiri, sirini mnyonge.
Hadharani ni mwema, sirini ni mwovu.
Hadharani ni mcha Mungu, sirini ni mshirikina.
Hadharani umeridhika, sirini una roho mbaya. Hadharani unapenda familia, sirini umeitelekeza.
Hadharani ni mwaminifu, sirini unachepuka.
Hadharani una bidii, sirini ni mzembe.
Hadharani umefanikiwa, kwa siri huna uhakika na kesho.
Tunajigombanisha sana na ukweli wa sirini tusiothubutu kuujadili na yeyote. Nguvu hii kubwa tunayoitumia kujenga ukamilifu inatutengenezea maumivu mengi ya kihisia tunayoona aibu kuyatafutia tiba.
Ukitaka kuujua vyema uhalisi wako chunguza vizuri namna unavyowatendea watu uliowazoea, watu wasioweza kukuadhibu ukiwakosea, watu usiolazimika kuwafurahisha kukwepa matokeo ya tabia zako, watu usiowahitaji, na kubwa zaidi chunguza namna unavyozungumziwa [na kuwazungumzia] na watu wanaokufahamu vizuri zaidi —hasa familia yako.