Maranyingi tafuta kupatana na mtu anayepambana kugombana na wewe,mfuate katika hali ya kujishusha muombe tafadhali mkae muyaongee kwani ugomvi wenu hata upambe moto mpaka nje ya mipaka ya kimataifa kamwe hauwezi kuwa dawa ya kuiponya mioyo yenu.✍️
Mwaka Jana October katikati tuliingia biashara ya Logistics rasmi
Tumeweza ajiri full time vijana watano
Tumeweza safirisha containers zaidi ya 700(export na Import)
Bado ni wachanga lakini mdo mdo tunasonga.
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 3
Mheshimiwa Lissu alisema wakati namfuatilia kuwa tutazuia uchaguzi, tutaenda kukinukisha vibaya sana. Video hiyo ilinipa hamasa sana na video hiyo hamasa.
Nilianza maandalizi ya kukinukisha hapa Songea. Na nimeshiriki kwenye TONETONE nilichangia elfu 10. Na tar. 07/10 tulitaarifiwa wapo viongozi watakaokuja ambao watakuwepo John Heche na viongozi wengine.
Wakiwa Mbinga tulipata taarifa kuwa amekamatwa Mwenyekiti wa Chama taifa. Tukaambiwa Mwenyekiti amekamatwa na baadae nikamuuliza mwenyekiti wa Bavicha songea akasema tutaambiwa mkutanoni.
Niliwakuta Polisi na viongozi wa Chama wengine Mhe. Heche alikuwa anajiandaa kutoa taarifa. Na baadae tukaamuliwa na polisi kuwa tuko chini ya ulinzi. Tukapelekwa polisi. Nikahojiwa kwa kufanya vurugu na nilivyorudi nikaletwa kwako nanunanihoji tena. Hayo ndio maelezo ya "P2"
Shahidi wa 7 "P3" nae ni yule wa siri anaishi Matengule kule Mbeya nina mke na watoto wanne. Ni derva wa bodaboda kijiwe kipo eneo . .. nina mikaa 8 kijiweni hapo na mfuasi wa Chadema miaka 4 kwa sasa. Nimeshiriki shughuli mbalimbali ikiwemo maandamano.
Nilikuwa mfuasi wa Freeman Mbowe na pia nimeshiriki mikutano mbalimbali.
Tarehe 04/04/2025 nikiwa nasoma YouTube Mwenyekiti Lissu alisema tutahamasisha uasi na kuzuia uchaguzi kufanyika.
Nilihamasika na nitakuwa mstari wa mbele kwa kupiga wananchi watakaokuwa wanashiriki uchaguzi. Nilienda kijiweni kwangu kuhamasisha vijana wangu. Na nikiwa kijiweni alinikamata afisa wa polisi kwamba nilikuwa nafanya hamasa pale kijiweni.
Nilidhaminiwa pale kituoni na baadae nikaitwa hapa polisi kuhojiwa. Hayo ndio maelezo yangu.
Anamaliza anakuja P4 huyu atakuwa ni shahidi wa 8. Nae ushaidii wake uko kama ifuatavyo.
Mimi ni Dereva wa bajaji nafanya kazi ya bajaji morombo arusha na boss wangu ni ...... nimesoma Murieti.
Nakumbuka tarehe 03/04 nilikuwa nafuatilia Mkutano wa Chadema live. Niliona Chadema wanahamsisha uasi na njia watakayoitumia kupata madaraka. Chadema wanaamini katika uasi. Na pia Lissu alisema majudge ni maccm na wafuasi wake waache ndoto za kushinda uchaguzi.
Niliamini nikiasi pia pengine mambo yatabadilika hivyo nilihamasika na nikaanza kusubiri kukinukisha. Nikakuta bajaji wenzangu wanajadili jambo hilo.
Wengi tulikuwa tunaunga mkono kauli za LISSU. Bora kinuke tu. Bajaji wengi walikuwa wanaunga mkono wa kikinukisha ndio askari walitokea na kutuambia tunapanga vurugu.
Huu ushahidi utachekesha sana yani ni zaidi ya Futuhi 🤣🤣🤣🤣
Haya tuendelee na kesi yetu
Amemaliza maelezo yake, anakuja shahidi wa 9 "P5"
Najishughulisha kuuza vifaa vidovidogo kariakoo. Nikiwa napeluzi mtandaoni nikiwa Posta ya zamani niliona mtu ambae ni Lissu mtandaoni anasema mwaka huu hakutakuwa na uchaguzi na watakinukisha kweli.
Binafsi nilielewa kuwa anahamsisha watu kufanya fujo.
Nilienda nyumbani Riverside nikapita kijiweni. Nikakuta rafiki angu anaangalia. Mabishano yakaanza kijiweni maana wengine walisema tunaunga mkono maneno ya Lissu na wengine wakasema atazuiaje.
Maongezi makubwa pale kijiweni ilikuwa ni maelezo ya Lissu. Mimi nikaona nchi yetu itaenda kuingia kwenye machafuko nikawasiliana na ndugu yangu ambae ni Askari kuwa ameyasikia hayo.
Akaniambia tumeyasikia na tunayafanyia kazi.
Nikapigiwa simu na mtu baadae ambae akasema niende kutuoni kutoa maelezo yangu.
Anafuata P6 ambae ni shahidi wa 10.
Na yeye ameapa na ushahidi wake ni kwamba mkazi wa bomba mbili bodaboda. Mimi nashiriki siasa ni Chadema. Jan. 2025 nilimfuata mwenyekiti wa vijana songea essau Chiza. Nilimueleza nia yangu na akanikaribisha kwenye chama.
Nilimtafuta Essau Chiza Mwenyekiti wa Bavicha na akasema atanishirikisha kwenye mkakati wote wa kuleta kuvurugu.
Na akanieleza nijiandae kuwapokea viongozi wa kitaifa pale Matalawe.
Part 4 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Retweet yako.
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 2
Huyu sasa ni shaidi wa pili baada ya yule wa kwanza ambae ni George.
Tarehe 03/04 mtumiaji wa mtandao huo wa YouTube yaani akaunti ya JAMBO TV alichapisha maudhui yakiyojulikana TUNDU LISSU uso kwa uso na watia nia chadema.
Katika video hiyo Lissu alisema majaji ni maccm, mapolisi wanaiba kura na vibegi na uchaguzi wa 2024 Rais alitoa maeleekezo kuwa wapinzani wasiende kokote. Yaani walienguliwa na maccm.
Pia alisema mimi nataka kacheo na nyie hamtaki kacheo sasa tunaweza kushinda au kushiriki uchaguzi wa aina hii? Sas amsimamo wetu kama Chama ni No Reforms no Election tunasimamia hapo.
Nilipakua video hiyo kwenye ukurasa wa JAMBO TV na kuiwasilisha.
Maelezo ya shaidi wa tatu PF ... Insp. Andrew Churu nae maelezo yake yanasomwa.
Mimi natokea Dodoma nafanya kazi huko na maelezo haya nimeyatolea Dar es salaam. Niko polisi toka 2000 nafanya kazi ofisi ya DCI makao makuu Dodoma. Tar. 07/04 nilipigiwa simu na DCP kuwa yupo.mfanyakazi wa JAMBO TV yuko Dodoma akanitumia namba ya simu ili nimtafute.
Siku hiyo alikuja shahidi hiyo na camera yake na kutoa ushirikiano ambapo alinipa memory card ambayo ilikuwa na video ya Lissu. Alifungua camera na kunipa kidhibiti hicho na tukaaandikiana uthibitisho wa nyaraka hiyo.
Nilimuhoji kuhusu ufahamu wake wa tukio hilo alipoenda pale Makao makuu ya Chadema na yeye ametokea Jambo TV alirekodi kupitia camera hiyo. Anakiri kuwa walipandisha instgram na mitandao mingine. Na nilielekezwa kuwa nivipeleke Dar es salaam siku hiyo hiyo na kuleta Dar es salaam.
Nikakutana na afande George Dar es salaam kwa ajili ya kumkabidhi vifaa hivyo vyote kwa maandishi.
Shahidi wa 4 ASP Kaaya ni ushahidi unaofuata.
Samwel Elibariki Kaaya mimi ni mtaalamu wa picha ni Askari wa Jeshi la Polisi ninafanya kazi ya kupiga picha za mnato.
Nilipewa vifaa vya kuvifanyia uchunguzi ikiwemo adapter, flash disk, barua na vifaa vingine nikitakiwa kufanya uchunguzi wa video mbalimbali. Zilizokuwepo kwenye memory na flash disk. Nilitahijika kuthibitisha uhalisia wa video hizo kitaalamu. Maudhui yenyewe ni yale mapolisi kuiba kura na vibegi, majaji ni maccm na taarifa kama hizo.
Chanzo cha picha mjongeo hizo ni kipi na zimetoka wapi ndio kazi yangu niliyotakiwa kufanya.
Niliakgua vifaa vyangu kuona usalama wake, Vilikuwa salama na imara kufanya kazi hiyo.
Baada ya uchunguzi wa kitaalamu niligundua picha mjongeo nilizopewa niligundua ni halisi kabisa na nikaandaa taarifa na kusaini taarifa hiyo.
Shahidi wa tano anaitwa " P"huyu ni mzaliwa wa Dar na mwaka umefichwa na ni mtoto wa kwanza. Nilisoma shule .... nilijiunga chuo cha kilimo na niliishia elimu ya certificate. Na 2020 nilijiunga chuo cha DSJ 2021 hadi 2023 na kujiunga na JAMBO TV kama mpiga picha kazi ninayoifanya hadi leo.
Nilihudhuria mkutano wa Chadema. Uliofanyika makao makuu chadema. Ulihudhuriwa na watia nia na mh. Lissu alihutubia. Tulienda wafanyakazi watano wa jambo na tukaenda. Niliona tangazo kupitia mkurugenzi wetu.
Tulikuwepo waaandishi wengi ikiwemo wa Azam na vyombo vingine tulirusha live tukio lile sisi jambo TV.
Masuala yaliyokuwa yakiongelewa ni kuhusu suala la Uchaguzi na mambo yaliyokuwa yakiongelewa ni uchaguzi na no reforms: No election na kikubwa ni matatizo wanayokutana nayo kama Chama katika chaguzi zao. Mambo hayo yapo kwenye memory kama nilivyokukabidhi yapo humo. Kikao hicho kilifanyika masaa mawili hadi matatu. Na baadae waandishi tuliondoka na wenzetu tukawaachia
Maelezo ya shahidi wa 6 anaitwa P2 nae anaanza baada ya yule aliyepita.
Mimi ni mkazi wa matalawe ni mkazi wa matalawe. Sijao sina mtoto ni mfuasi wa CHADEMA toka 2021 na ni mshabiki wa tundu Lissu nililjpia kadi ila sijapata kadiyangu. Nimekuwa namuunga mkono Lissu na kwa songea mwenyekiti wetu wa BAVICHA ndio kiongozi wetu ambae almaarufu kama mwamba wa Kigoma.
Part 3 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Retweet yako
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 1
Mahakama imeamuru kuwa committal itasomwa yote bila kurushwa live.
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea kusoma kwa sasa.
Maajabu yaliyotokea ni kwamba mawakili wa serikali waliomba maelezo ya mashahidi wa siri yasirushwe live.
Lakini cha ajbu mahakama imesema maelezo ya mashahidi wote yafichwe na yasiwe live.
Kifupi mahakama imetoa uamuzi ambao hata serikali haijaomba. Imefunga kila kitu na kesi kuzimwa.
Katuga anaendelea, amemkumbusha Mtuhumiwa Shitaka lake na kumkabidhi taarifa ya mashitaka.
Anasema Jamhuri itakuwa na mashaidi 30 na vielelezo vya myaraka 9.
Maelezo yataanza kusomwa na Thawabu Isa wakili wa serikali.
Anasimama na kuanza kusema SSP Kangio, atakuwa shahidi wa kwanza. Ameapa kusema ukweli na maelezo yake ni kama ifuayavyo.
Nimeajiriwa 2003 polisi na mikoa mbalimbali ninefanya. Nimekuwa na vyeo tofauti na sasa ni mrakibu wa polisi kanda ya Dar es salaam. Nafanya majukumu ya kusimamia askari katika majukumu ya kiupelelezi.
04/04/2025 nikiwa ofisi afande Kaaya anayefanya Doria mtandaoni nilimtaka anipe picha mjongeo kuhusu maudhui yakiyokuwa yanatoa taarifa yenye uchochexi.
Maudhui hayo ni mapolisi wanakuja na mabegi ya kura feki kwenye vituo. Jambo ambalo ni uongo. Majukumu yetu ni ulinzi na sio kuiba kura.
Pia maelezo yaliyokuwepo ni kuhusu majaji ni MACCM hivyo wanafanya kazi kwa mujibu wa CCM. Na sio kweli kwamba majaji wanafanya kazi kuwaonea wapinzani. Na hivyo taarifa hii ni uongo na yalilenga kuleta chuki.
Pia alisema kuenguliwa kwa wapinzani ni mkakati wa serikali hivyo zilikuwa ni uongo na kutengeneza chuki dhidi ya Rais.
Na msimamo wetu ni wa uasi. Ni kweli ni msimamo wa uasi kwani tunaenda kukinukisha na huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli.
Katika picha mjongeo hiyo mzungumzaji alikuwa ni LISSU. Na aliyokuwa anafanya yalikuwa na nia ya kuitishia serikali ili ayapate yeye na wafuasi wake.
Niliamuru Insp. Kaaya aanze kufanya uchunguzi wa jalada hilo na taarifa hiyo ndio akafungua kesi na kuanza uchunguzi. Na akaanza kujaza PF500
Baada ya kutoa maelekezo kutafuta mjengeo iliyoerekodiwa eneo husika nilitoa taarifa kwa mabosss wangu na kuhusu kile alichosema TUNDU LISSU mtandaoni. Niliripoti kwa afande DCI akasema tuendeleee
Nilimtafuta kiongozi wa JAMBO TV anipe video ile na baadae akasema video anayo P ambae kasafrir. Hivyo nikatoa taarifa kwa maboss kuwa video tutaipata kwa P ambayo yuko Dodoma.
DCP NG'ANZI nilimpa taarifa kuwa tutaipata kwa kijana wa Jambo TV ambae yuko Dodoma.
Haya ni maelezo ya George ambae ni kaimu mkuu wa upepelezi kanda ya Dar es salaam. Yansomwa maelezo yake hapa mahakamani.
Nikaeleza lifunguliwe kosa la uhaini kwasababu aliesema TUNDU lisuu hayo maneno yake, yeye ni Askari ambae ana cheti cha Kujenga taifa kutoka jeshi la JKT hivyo alikuwa na wajibu wa kulinda amani ndani ya Taifa letu. Kusema maneno kama hayo ni kosa kisheria.
Hayo ndio maelezo yangu yote. Yameisha maelezo ya George na anasemaa anayo maelezo ya nyongeza Ya huyo SSP George akasema pia nilikabidhiwa TUNDU LISSU akitokea RUVUMA.
Nilimpokea Lissu na wakati nafanya mahojiano walikuja mawakili wake pia Tulienda kwenye ofisi yenye utulivu na nikamuonya kuwa anatuhumiwa kosa la uhaini. Na kumpa haki zake za msingi.
Huyu George ni msaidizi wa Mafwele. Anasemaa Lissu aligoma kutoa maelezo yoyote.
ASP. John. Ni shaidi wa pili ambae ni mkazi wa Temeke. Amekula kiapo na ushaidi wake ukaanza kuandikwa.
Nimeajiriwa 2005 na nina elimu ya computer na mfanyakazi wa polisi. Nimesoma vyuo ikiwemo Chuo Cha Polisi kurasini.
Nafanya kazi kwa DPP dawati la Doria mtandaoni. Na huwa napeleleza makosa yanayofanywa mitandaoni.
Huyu sasa ni shaidi wa pili baada ya yule wa kwanza ambae ni George.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Retweet yako.