Hawa ndio vijana wanaojielewa.
Sio machawa.,wanazo hoja za msingi.
Nafikiri zikija Reforms kwenye Taifa letu wabunge wawe na vigezo vya elimu yenye tija kama hawa wanachuo. Nimependa sana waliyo yawasilisha.
TUNDU LISSU KUMUHOJI MKUU WA GEREZA LA UKONGA NA KAMISHNA MKUU WA MAGEREZA KATIKA SHAURI LA KIKATIBA NAMBA 7300/2026
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mhe. Tundu Lissu, atawahoji kwa maswali ya dodoso Kamishna Mkuu wa Magereza pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga tarehe 1 hadi 3 Julai 2026 katika Shauri la Kikatiba Na. 7300 la Mwaka 2026 mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma.
Shauri hilo lilifunguliwa na Mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga.
Katika shauri hilo, Mahakama inaombwa kuamua kuhusu masuala mbalimbali ya kikatiba yanayohusu vikwazo vya Jeshi la Magereza dhidi ya Mhe. Tundu Lissu, mawakili wake, ndugu, viongozi na wanachama wanaomtembelea gerezani.
Miongoni mwa masuala yanayolalamikiwa ni pamoja na kuzuiwa kwa viongozi na wanachama kumuona Mhe. Lissu gerezani, pamoja na vitendo vya askari wa magereza vya kusikiliza mazungumzo kati ya Mhe. Lissu na mawakili wake wanapofanya mashauriano ya kisheria, jambo ambalo linakiuka haki ya faragha na haki ya mawakili kufanya kazi yao kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
Katika shauri hilo, Mhe. Tundu Lissu ni miongoni mwa wajibu maombi (Respondents, huku Chama cha Wanasheria Tanganyika kitashiriki kama mdau mwenye maslahi katika shauri (Interested Party) baada ya Mahakama kukubali maombi yake.
Aidha, kutokana na uzoefu wao wa kukumbana na changamoto hizo wanapomtembelea Mhe. Lissu gerezani kwa ajili ya mashauriano ya kisheria, Mhe. Lissu anatarajiwa pia kuwahoji mawakili waliofungua shauri hilo ili waweze kuieleza Mahakama kuhusu mazingira halisi wanayokumbana nayo wanapotekeleza wajibu wao wa kitaaluma.
Shauri hilo litasikilizwa kwa njia ya Mtandao mbele ya Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu; Mhe. Jaji Mruma, Mhe. Jaji Dkt. Rumisha na Mhe. Jaji Dkt. Longopa.
Shauri hili ni miongoni mwa mashauri muhimu ya kikatiba yanayoweza kuweka mwelekeo wa kisheria kuhusu haki ya mawakili kufanya mashauriano ya faragha na wateja wao waliopo mahabusu au gerezani, pamoja na kulinda misingi ya haki ya kupata msaada wa kisheria na usiri wa mawasiliano kati ya wakili na mteja.
Imetolewa na:
Wakili Paul Kisabo
Dar es Salaam
30 Juni 2026
What you see in this video is the reason political rallies have now been banned in Tanzania. The opposition’s rallies were growing larger with each passing day. Not only were they drawing massive crowds, but people attending the rallies were also voluntarily donating money to support the opposition.
It was a clear and powerful rebuke of Samia Suluhu’s regime by the people of Tanzania.
@POTUS@SenTedCruz@SenatorShaheen@SenateForeign@SFRCdems
TAFSIRI YA ALICHO-POST X WAKILI MSOMI NA RAISI WA TLS
Kuendelea kutoa maelezo kuhusu ripoti yako inayodaiwa kuwasilishwa kwa Rais ni chuki ya moja kwa moja kwa akili zetu.
Baada ya kukamilika na kuwasilishwa kwa ripoti hiyo, ikiambatana na maagizo kwamba umma ukae kimya kwa misingi kwamba jambo hilo haliwahusu, kwa hivyo unazuiliwa kutoa ufafanuzi kwa umma huo huo.
Maelezo yoyote yanapaswa kuelekezwa kwa mamlaka ambayo ripoti hiyo iliwasilishwa.
Sio sahihi na haina mantiki kujifanya kufafanua mambo kwa umma wakati ripoti nzima na ukweli wake wa msingi unabaki ndani yako pekee.
Kitendo kama hicho si chochote zaidi ya zoezi la ziada na lisilo la lazima la kujitetea.
Ripoti hiyo si yetu wala haituhusu sisi kama umma, kwa madai yako mwenyewe.
Tunakataa kabisa maana yoyote kwamba hatuwezi kuwa na mawazo au hukumu huru.
Hatutalazimishwa kukaa kimya. Tuna uwezo wa kutathmini, kuhoji, na kufikia hitimisho.
Kitendo chochote kinachodhoofisha hili hakikubaliki na ni uvunjaji wa heshima.
kinachohitajika ni kuanzishwa kwa tume huru ambayo haina upendeleo, inaaminika, na ina imani ya wadau wote.
Ukweli, haki, na uwajibikaji vinabaki kuwa misingi pekee inayofaa ambayo taifa linaweza kurejeshwa.
BAK MWABUKUSI @Mwabuk2Boniface
Wakili Jebra Kambole kutoka TLS ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, Aprili 27, 2026 wakati Asasi 14 za kiraia zikitoa msimamo wao kuhusu Ripoti iliyosomwa na Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktoba 29, 2025 Jaji Othman Chande.
Jana niliandika ujumbe nikikosoa kitendo cha Mzee MBOWE kumuombea msamaha SABAYA. Nimepata maoni mengi; wengine wakisema sikuwa sawa.
Ipo hivi. Kuna mambo katika siasa hayawezi kufutwa na maneno laini na mepesi ya “msamaha,” hususani msamaha usiotoka kwa mtenda dhambi mwenyewe.
Utawala wa SABAYA katika wilaya ya Hai haukuwa wa kisiasa tu; ulikuwa ni utawala wa chuma na ukatili uliopitiliza. Hata Mzee MBOWE anafahamu hilo.
Makosa ya uhujumu uchumi na unyang’anyi wa kutumia silaha (armed robbery) yaliyomfunga gerezani wakati ule, ni tone dogo sana katika bahari ya unyama wake.
Wapo watu walitekwa, kuteswa, na kuachwa na vilema vya kudumu. Kusema mtu huyu anastahili msamaha bila toba ya dhati kwa wahanga, si tu ni kosa, ni dhihaka.
Miongoni mwa wahanga wa genge la SABAYA ni ndugu yetu Simon MNYAMPANDA, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hai. Ndugu yetu aliteswa.
Simon Mnyampanda aliteswa kwa umeme. Ameeleza wazi kwamba, alihojiwa kuhusu mahusiano yake na Mzee MBOWE. Mwisho, alipigwa misumari ya miguu.
Huyu ni mtu aliyepata mateso hayo akimlinda Mzee MBOWE na CHADEMA. Leo Mzee MBOWE anajigeuza kadinali na kumuombea msamaha mtesaji SABAYA?
Genge hilo halikuishia hapo. Genge hilo lilikuwa kama MAHARAMIA. Walivamia nyumbani kwa mgombea udiwani wa kata ya Narumu katika jimbo la Hai.
Baada ya kumkosa, walitoa adhabu ya kinyama kwa watu waliokuwepo nyumbami kwa kuwakata masikio na sehemu nyingine. Nyumba nzima ilitapakaa damu.
Hawa ni binadamu, si takwimu za kisiasa. Hawa watu waliotendewa mambo hayo wapo. Baadhi ya ushahidi wa masuala hayo nimeambatanisha katika makala hii.
Inasikitisha kuona Mzee Mbowe anatumia mateso ya wafuasi wake kama mtaji wa kisiasa (political capital). Binafsi nimejiuliza maswali mengi tangu hiyo jana.
Je, wahanga wameombwa msamaha na kufidiwa? Je, mateso yao yamekuwa ngazi ya makubaliano ya kisiasa? Hii si dharau kwa wale walioteswa wakikupigania?
Sabaya anapaswa kuomba msamaha kwa waathirika, si kuombewa. Vinginevyo, hii ni michezo ya kumtengenezea mazingira ya kupata uteuzi katika Serikali ya CCM.
Watu wa Hai hawajasahau. Damu na machozi ya wahanga bado vinadai haki. Msamaha bila toba ni baraka kwa ukatili mwingine ujao. Haki kwanza, msamaha baadaye.
Binafsi, nilimheshimu Mzee Mbowe kiasi cha kumpa mwanangu wa tatu jina la “Freeman”. Leo hii, nahisi usaliti mkubwa moyoni mwangu kwa mambo hayo.
Kunyamaza mbele ya usaliti huu si busara, bali ni upumbavu ambao kesho utatunyong’onyesha. Nimeandika ili kulinda hadhi ya jina la mwanangu.
Siku mtoto wangu akiniuliza, nitamjibu kwa utimamu kabisa. “Nilitetea maana halisi ya ‘Freeman’ wakati jina hilo lilipotaka kuchafuliwa na siasa za kimaslahi.”
"Chadema, chama chenu hakitakuwa tayari kwa maridhiano yenye kupambaza, kuhadaa, yenye ulaghai na yenye kuliondoa Taifa kwenye ukweli, haki na kile ambacho Taifa inataka, kamwe hatuwasaliti Watanzania." Mhe. @HecheJohn