Dear, RANGO.
Hadi umemaliza muda wako wote wa kuongoza The Inter-Parliamentary Union (IPU) umeshindwa kabisa kuthubutu kukemea mauaji ya raia yaliyofanywa na Serikali yako katili ya CCM. Wewe ni KATILI
Rango, utamaduni wa mtu ndiyo utu wake
Vazi la Maasai ni costume/ensemble. Siyo vazi tu la kawaida la kusitiri mwili, ni muundo kamili wa kisanaa na kiutamaduni unaobeba ujumbe maalum (total aesthetic & cultural presentation)
Kila rangi katika shuka ya Maasai imebeba maana yake; nyekundu inawakilisha ushujaa na damu; kijani inawakilisha ardhi na lishe; bluu inawakilisha anga na mvua; nyeupe inawakilisha amani. Ipo hivyo.
Muundo wa urembo wa shanga shingoni, mikononi, na masikioni hutofautisha rika (age-sets), jinsia, hadhi ya kijamii, na kama mtu ameolewa au yuko katika kipindi cha rika la ushujaa (Moranism)
Kuanzia viatu vya ngozi (Akala), fimbo au mkuki, hadi mpangilio wa nywele na rangi ya samawati au udongo mwekundu (Olkaria), vinatengeneza muundo kamili (ensemble) ambao hauwezi kutenganishwa
Mavazi ya asili hayavaliwi tu kama pambo au mtindo wa mavazi (fashion); ni tamko la wazi la utambulisho na uwepo wa jamii husika duniani. Mavazi ni lugha inayojieleza bila kusema neno. Ni UTAMADUNI
RANGO, huwapendi Maasai, unapenda mavazi yao?
Maasai wanafukuzwa katika ardhi yao. Serikali katili ya CCM ikaenda hadi kutangaza katika gazeti la Serikali kufuta kata 11, vijiji 25 na vitongoji 96 wilaya ya Ngorongoro. Wewe ukiwa SPIKA wa Bunge
Unatumia utamaduni rasmi wa jamii ya Maasai kujitangaza kwa watasha/mabeberu. Lakini ukiwa Spika ulishindwa kuisimamia Serikali Katili ya CCM ilipokuwa inawaondoa Maasai Ngorongoro
Unafurahia mavazi ya asili ya Maasai wakati huo Maasai wanafukuzwa kutoka katika ardhi yao. Wamewekewa vikwazo vya elimu, afya, uchumi, miundombinu ili wahame katika asili yao
Hakuna Hospitali. Hakuna shule. Hakuna vyuo vya ufundi stadi. Unaona fahari gani kutumia mavazi yao ya asili? Ukiwa Spika, uliunga mkono Maasai kuhamishwa kwa nguvu kutoka Ngorongoro
Maasai Ngorongoro hawaruhusiwi kulima mazao ya chakula. Muda mrefu, wananunua chakula Karatu. Ukiwa SPIKA, Maasai walizuiwa kununua chakula kutoka nje ya Ngorongoro. Huo ni UKATILI
That’s Cultural genocide. Ethnocide.
February 11, 2022, Serikali katili ya CCM kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) waliwapa Flying Medical Service (FMS) barua ya kutakiwa kusitisha huduma zao zote kwa Maasai wa Ngorongoro
FMS wanafanya shughuli za utabibu kwa njia ya anga Arusha na Manyara tangu 1983. FMS wakazuiwa wasifanye shughuli zao Ngorongoro. Ukiwa SPIKA, hukuona sababu zozote za kuwatetea MAASAI.
FMS walikuwa wanatoa chanjo za IPV kuzuia polio, hepatitis B kuzuia homa ya ini, Varicella kuzuia tetekuwanga, DTAP kuzuia diphtheria, pepopunda, kifaduro, MMR ya surua, mabusha na rubela
Kwa siku moja, (Flying Medical Service - FMS) waliruka mara tatu na kufanya kliniki zao za kitaalam sehemu tatu tofauti ndani ya Eneo la mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Wakapigwa STOP.
Wakati FMS wanapewa barua kusitisha huduma zao, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) alikuwa Hamza JOHARI. Huyu sasa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). RANGO ulikuwa SPIKA
RANGO, mwarabu ana thamani kuliko Maasai?
Ukiwa SPIKA, Serikali yako katili ya CCM imechukua ardhi ya vijiji LOLIONDO na kumpa Otterlo Business Corporation (OBC) ambao wanatoka familia ya kifalme Dubai. RANGO, ni MTESI wa Maasai
Ngorongoro Conservation Area (NCA) kuna eneo lenye ukubwa wa 8,292 km² (mara 3 ya eneo lote la Zanzibar, 2,462km2). Loliondo Game Controlled Area (LGCA) ukubwa wa eneo ni 4,000km²
Waarabu kutoka familia ya falme ya Dubai (Otterlo Business Corporation – OBC) ameongezewa 1,500km² kutoka 4,000km2 zilizokuwa kwa wananchi ambao wamebaki na 2,500 km²
February 2022, ukiwa SPIKA, ukaitaka Serikali katili ya CCM kuwachukulia hatua kali za kisheria watu na taasisi zinazopotosha kuhusu zoezi la watu kuhama Ngorongoro na uwekaji mipaka Loliondo
Mtikila, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Mheshimiwa Rais @SuluhuSamia ,
Kwa masikitiko na mshangao mkubwa, tumepokea taarifa za kuzuiwa kwa wanasheria, wanaharakati wa haki za binadamu na waandishi wa habari waliokuwa njiani kuingia nchini kushiriki kwa njia ya amani katika mchakato wa kisheria unaomhusu Mheshimiwa Tundu Lissu.
Waliodhulumiwa katika tukio hili ni pamoja na:
Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya, Mh. Willy Mutunga
Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya na Mwanasiasa mashuhuri, Martha Karua
Mwandishi wa Kimataifa na Mpigania haki za binadamu, Hanifa Farsafi
Mwanaharakati mashuhuri Boniface Mwangi, ambaye alivamiwa usiku akiwa hotelini na baadaye kukamatwa hadharani asubuhi akiwa anapata kifungua kinywa.
Wote hawa walikuwa wamekusudia kushiriki kwa njia ya amani kama waangalizi wa haki na utawala wa sheria katika kesi ya wazi inayomkabili kiongozi wa Upunzani nchini na mwenyekiti wetu @ChademaTZ2, Mh. @TunduALissu.
Mheshimiwa Rais, nilidhani matukio haya ni hujuma dhidi yako binafsi na taswira ya taifa letu. Lakini niliposikia kauli yako ya hadharani ukiwadhihaki na kuwashambulia wageni hawa wa heshima kutoka mataifa jirani, nikatambua kwa masikitiko kuwa si hujuma tu, bali ni msimamo rasmi wa serikali yako. Hili ni jambo la kutia hofu kubwa kwa mustakabali wa haki, uhuru na demokrasia nchini kwetu.
Umeisahau Tanzania ya Nyerere?
Tanzania hii ndiyo iliyoandikwa kwenye historia kama ngome ya ukombozi Kusini mwa Afrika. Hapa ndipo wapigania uhuru wa Afrika Kusini, Zimbabwe, Namibia, Angola na Msumbiji walikimbilia kwa usalama wao. Hapa ndipo chimbuko la mshikamano wa Waafrika kupitia harakati za Pan-Africanism.
Umesahau kuwa hapa nchini kwetu ndiko yalipoanzishwa mashirika na taasisi za ukombozi kama vile Pan African Freedom Movement of East and Central Africa (PAFMECA) na PAFMECSA, ambazo baadaye zilisaidia kuunda Umoja wa Afrika (OAU)? Umesahau kuwa Arusha ndipo yalipo makao ya MS-TCDC, chuo kinachofundisha Pan-Africanism na utetezi wa haki za binadamu?
Umesahau kuwa Tanzania ndiyo mwenyeji wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambayo mojawapo ya misingi yake ni uhuru wa watu wake kusafiri, kushirikiana na kushiriki mijadala ya umma kwa njia ya amani?
Mheshimiwa Rais, kwa kuzuia wageni hawa mashuhuri kuingia nchini, Tanzania inavunja kwa wazi misingi ya mikataba ya kikanda na kimataifa, ikiwemo:
1. Mkataba wa Umoja wa Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu (ACHPR, 1981)
2. Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR, 1966)
3. Tamko la Umoja wa Mataifa la Watetezi wa Haki za Binadamu (1998)
4. Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Treaty), ibara ya 104 kuhusu Uhuru wa Kusafiri
5. Azimio la Arusha (1990) juu ya Utawala Bora, Haki na Uwazi katika Afrika
Mheshimiwa Rais, haya mambo mnayoyatenda ni fedheha kwa taifa letu. Ni aibu kwa nchi iliyoasisi uvumilivu, haki za kiraia, mshikamano wa Afrika na uhuru wa kujieleza. Ni doa kwa historia ya taifa ambalo liliwahi kuaminika kuwa kinara wa amani na maridhiano barani Afrika.
Nikuombe utazame upya mwelekeo huu wa hatari. Tanzania ya 2025 haipaswi kuwa kivuli cha hofu na ukandamizaji, bali iwe kinara wa haki, utu, sheria na demokrasia kwa wote — raia na wageni.
VIDEO:
Kufuatia uwepo wa taarifa ya kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini @orpptanzania ametengua uteuzi wa vigogo wanane (8) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA @ChademaTZ2) waliokuwa wameteuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Tundu Lissu @TunduALissu na kisha kuthibitishwa na Baraza Kuu la Januari 22.2025, Wakili Maduhu William kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC @humanrightstz) ameeleza kushangazwa na hatua hiyo aliyoitaja kuwa kinyume cha sheria
Akihojiwa na Jambo TV, Wakili Maduhu amesema kwa mujibu wa sheria, Msajili wa Vyama vya Siasa ni mlezi wa Vyama vya Siasa na kwamba hana mamlaka ya kisheria ya kuingilia shughuli za ndani ya vyama, kuteua au kutengua uteuzi wa kiongozi yeyote wa chama chochote cha siasa
Wakili Maduhu ameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa hata yule aliyepeleka suala hilo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa alikosea badala yake alipaswa kufuata taratibu za ndani ya chama chao na kama bado angeona hajatendewa haki ni vyema angekimbilia Mahakamani
Ikumbukwe kuwa, viongozi wa CHADEMA wanaotajwa kutenguliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa ni Wajumbe wa Kamati Kuu Godbless Lema @godbless_lema, Salma Kasanzu, Sheikh Hafidh Ali Saleh, Rose Mayemba @RoseMayemba na Dkt. Rugemeleza Nshala @rugemeleza (ambaye pia aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA), na Wajumbe wa Sekretarieti watatu (3) wakiongozwa na Katibu Mkuu John Mnyika @jjmnyika, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Amani Golugwa @amanigolugwa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Wakili Ali Ibrahim
VIDEO:
Viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameamua kujivua uanachama wa chama hicho kwa kile walichokieleza kutopendezwa na mwenendo uliopo chamani kwa sasa ambao wameeleza kuwa umesababishwa na uongozi uliopo madarakani.
Viongozi hao ambao ni Masanja Katambi, Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Magharibi; Sifa Gadafi, aliyekuwa Katibu Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) Mkoa wa Katavi, na Hamisa Korongo; aliyekuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Baraza la Wazee CHADEMA (BAZECHA) Mkoa wa Katavi.
Wakizungumza na wanahabari siku ya Alhamisi Mei 15, 2025, viongozi hao wamesema katika chama kumekuwa na misimamo mikali isiyo na tija kwa siasa za Tanzania huku wakieleza kuwa hatua ya viongozi wa chama hicho kushinikiza kuzuia uchaguzi ni kuwanyima Watanzania haki yao ya kupiga na kupigiwa kura.
Jumla ya wananchama 50 wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kutoka Mkoani Morogoro wamejivua uanachama wa chama hicho huku baadhi yao wakijivua nyadhifa mbalimbali za uongozi wa ndani ya chama hicho.
Hatua hiyo inakuja baada ya wanachama hao kudai kuwa hawaridhishwi
Baada ya Polisi kuthibitisha Watu watatu wakiwemo wawili wa Familia moja kufariki dunia katika Kata ya Mbokomu, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, baada ya kuangukiwa na Nyumba zao kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali Mkoani humo hatimaye tumempata Kijana Marko Steve ambaye ametrend baada ya kusaidia kuwaokoa Watoto wanne na Watu wazima wawili katika eneo la Kiboroloni.
Marko steve maarufu kwa jina la Waziri Mkazi wa Kata ya Mbokomu Wilaya Moshi Mkoani Kilimanjaro amejichukulia umaarufu baada ya video yake kusambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha akifanya uokozi kwa kuwamebeba Watoto wadogo huku akitembea kwa kutumia kamba.
#MillardAyoUPDATES
@TunduALissu aliwahi kusema " kama mliweka #NoReformsNoElection ili dau lipande yeye hafanyi biashara ya siasa"
Sikieni biashara yenyewe ya siasa sasa hapa👇👇👇
Wednesday
14th Oct, 2020
KITAYA, MTWARA
Kampeni za uchaguzi wa rais na wabunge zikiwa zimepamba moto, na ikiwa ni siku ya mapumziko kitaifa kuadhimisha kifo cha muasisi wa taifa hili, mkoani Mtwara hawakujua kama wangehitimisha siku hii vibaya
kabisa.
Naam!
OBC wamerudi tena wanataka kile kipande cha juzi cha KM 1502 walichopewa NCAA wapewe OBC. Hawa wamefanya propaganda miaka yote kuhakikisha kuwa watu wa Ngorongoro wanaporwa maeneo yao yote.
Hawa waandishi wa Jamhuri- Acheni kutumika dhidi y’a watu wa Loliondo na Ngorongoro. Acheni mara moja hichi mnachokifanya - Lengo lenu ni kuona watu wa Ngorongoro wanafukuzwa na kutokomea kabisa wilayani Ngorongoro. Balile waambie watu wako this time watu wa Ngorongoro hawatavulia hii propaganda tena . Fanyeni kazi zenu za uanahabari bila kuandama jamii miaka yote.
Hii ni kauli mbaya sana. Nafikiri kuna tatizo kubwa sana. Nasikitika kuwa imetolewa na Kiongozi kutoka ktk Chama changu. Nashindwa kupuuza maneno haya kwa namna yoyote ile. Maneno haya yanajengwa na mikakati wa siri ambayo wengi tunanaweza kuwa tunaiona lakini tunaogopa kuchukua hatua. Siasa zenye misingi ya udini sio za bahati mbaya ktk Nchi hii. Kauli chafu kabisa hii wala sio ya bahati mbaya. Siri zikiwa nyingi moyoni huwa zinatoka zenyewe.