KIMENUKAAAAAAAAA, naomba niingie kulala, ila nikiamka na ku-drop watoto shule na drop 💣 moja kali.
Video itakuwa hewani saa 1 usiku ya Tanzania.
ISSUE NI DIPU!!!!!
Kuna jinsi ambavyo huyu jamaa amejitoa kwa ajili ya Tanzania na Watanzania….
Na ni kweli matatizo yote ya haki tuliyonayo TZ yanatokana na kundi dogo la watu………. Watu milioni 70 tunabagazwa na kuuawa na kundi halizidi watu 100.
Wale “manabii, makuhani, mitume, wachungaji na maaskofu” wa ule mrengo wa mbogamboga hauwezi kuwakuta hata siku moja wakizungumzia mambo mazito yanayogusa maisha ya wananchi, haki na mustakabali wa taifa kama jinsi Askofu Kakobe alivyofanya katika video hii. Muda wao mwingi ni kuusifia mamlaka, kuwajengea woga waumini kwa “maono, unabii na miujiza wanayoijua wao” huku wakiwauzia maji, mafuta, udongo kama silaha za kiroho na kuchukua sadaka zao kama mbadala wa matumaini ya mafanikio ya ghafla.
Mara nyingi maombi, sala na unabii wao umejaa nyumba, magari, ajira na mamilioni yatakayodondoka kutoka mbinguni kana kwamba maisha yanaendeshwa kwa miujiza badala ya juhudi, maarifa, uwajibikaji na kufanya kazi.
Cha kushangaza zaidi, hawasemi chochote kuhusu umasikini, ukosefu wa ajira, rushwa, elimu, afya, haki na changamoto zinazowakabili wananchi. Wanapenda sana mamlaka kuliko ukweli, na wanapenda sana mifuko ya waumini kuliko mustakabali wa taifa.
Ukweli mchungu ni huu: Maombi bila hatua ni matarajio; sala bila kazi ni kujidanganya. Taifa halijengwi kwa kuuza mafuta, udongo na maji ya “baraka, miujiza au Upako” linajengwa kwa kazi, maarifa, uadilifu, haki na uwajibikaji.
"Hao watu wanaosema kwamba @HecheJohn ananizuia mimi kutoka gerezani ni kina nani?. Waambieni hivi mimi nipo tayari kukaa gerezani mpaka haki itakapopatikana, huo ujinga! ujinga! wa hao wapokea pesa za Lumumba na ukome." Mhe. @TunduALissu
Mheshimiwa @TunduALissu anasema siku zote watu wenye hatia ndiyo huwa waoga, watu wasiokuwa na hatia siyo waoga. Mimi siyo muoga kwa sababu sina hatia na niko tayari kukaa gerezani as longer as it takes mpaka haki ipatikane.
“I will be back!” 👊🏽🔥
Tundu Lissu is like the Terminator 🤣 hamtaweza kumwua isipokuwa kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu na yeye anaishi katika imani hii!
Much love and power to him ✊🏽
Tumaini la watanzania na hasa watanganyika! Hakuna kukata tamaa wapendwa na tuendelee kumwonyesha Lissu upendo mkubwa na sapoti - kamwe asije akakara tamaa
#FreeTunduLissuNOW
#FreeTunduLissu