Mfano Mungu anakupa bahata ya kuwa Tajiri wa maarifa,akili,na uwezo flani wa kifedha alafu unakuwa na urafiki kama wa @MwanaFA na @AyTanzania aisee utakuwa umefanikiwa sana me sikufichi
#WeEndeleaTu#fortheFullest
Najuwa aikuwa rahisi kufika walipo
Dunia imeshuhudia mengi, lakini kinachoendelea Palestina kinaacha maumivu ya aina yake.
Mpango wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, haukuwa tu vita dhidi ya Hamas kama alivyodai mwanzoni.
Bali ni operesheni kubwa ya kutokomeza kizazi cha Wapalestina, kuwaacha wakimbizi na hatimaye kuwapora ardhi yao.
Ukiutazama kwa jicho la karibu, mpango huu wa Netanyahu ulianza na hatua tatu kuu.
• Mauaji ya halaiki, Kuuwa Wapalestina kwa maelfu, bila kujali watoto, wanawake, au wazee.
• Mateso na uharibifu wa miundombinu, Kuwafanya waliohai wasiwe na sehemu ya kukimbilia wala matumaini ya kuendelea kuishi kama binadamu wa kawaida.
• Uporaji wa ardhi, Baada ya kuwafanya wakimbizi ndani ya nchi yao wenyewe, sehemu hizo zinanyakuliwa na walowezi wa Kiyahudi.
Hili si jambo geni katika historia ya Israel, lakini safari hii, ukatili wake umekuwa wa kiwango cha kutisha.
Kilichotokea Gaza si vita, ni mauaji ya halaiki.
Alikuwa na sauti iliyotikisa dunia ya muziki.
Alikuwa na misimamo isiyoweza kutetereka, ujasiri wa kipekee, na kipaji kilichozaliwa mitaani lakini kikatawala majukwaa makubwa duniani.
Alikuwa na uwezo wa kubadilisha machungu ya maisha yake kuwa mashairi yenye nguvu na hisia kali.
Huyu alikuwa Earl Simmons, maarufu kama DMX, rapa aliyepanda juu zaidi ya nyota wengine, lakini akaanguka kwa kishindo kikubwa.
Katika kilele cha mafanikio yake, DMX alikuwa na jina kubwa zaidi kwenye muziki wa hip hop, na ndoto za kuwa bilionea zingeweza kuwa ukweli.
Lakini haikuwa hivyo.
Ndoto hizo zilikatishwa ghafla, zikisombwa na dhoruba za madeni, matumizi mabaya ya fedha, na maisha yaliyogubikwa na giza la matumizi ya dawa za kulevya.
Mkewe wa zamani, Tashera Simmons, alikumbuka nyakati hizo kwa uchungu na mshangao, akisikitika kwa jinsi alivyokuwa karibu na utajiri usio na kipimo, lakini akaishia mikono mitupu.
"DMX angekuwa rapa wa kwanza kuwa bilionea," alisema kwa sauti ya huzuni, machozi yakimlengalenga alipokuwa akisimulia hadithi ya anguko la mumewe.
Tashera alisimulia jinsi walivyopata utajiri kwa kasi ya radi.
"Nakumbuka kipindi nilipokuwa naangalia akaunti yetu ya benki, sifuri zilikuwa hazikomi."
Katika historia ya uhalifu ulimwenguni, hakuna jina lililowahi kutikisa dunia kama Pablo Emilio Escobar Gaviria.
Wengi kila siku mnamtaja either kwa kusimuliwa au kuangalia documentary movie zake, ila kuna mengi hamyafahamu...
Mtu aliyekuja kutoka mitaani, akatengeneza utajiri wa dola bilioni 60, akaitikisa serikali ya Colombia, na kuitawala biashara ya cocaine kwa miaka zaidi ya kumi.
Lakini historia yake haikuwa ya kawaida. Ilijaa damu, hofu, rushwa, na utawala wa chuma.
Huyu ndio mfalme wa cocaine—Pablo Escobar.
Lakini aliwezaje kufanikisha haya yote?
Hebu tuchimbe kwenye simulizi hii ya kushangaza sana.
Uzi 🧵 👇🏾
Makosa unayofanya ni kufikiria kuwa wewe pekee ndiye unayekumbana na changamoto.
Ndiyo maana unahisi huzuni, unadhani unachukiwa na unajiona kuwa hauna bahati.
Ndiyo maana unahisi kila mtu ameshinda isipokuwa wewe.
Unakosea.
Hauko peke yako kwenye uwanja wa vita vya misukosuko ya maisha.
Sote tunapambana na pepo au tunakumbatia malaika. Mimi napigana na shoka dhidi ya pepo wangu kila siku na ninavuja damu, ninajeruhiwa na nakutana na kushindwa mara nyingi kama vile nakutana na ushindi.
Hauko peke yako!
Kuwa jasiri rafiki yangu, vumilia hata kama unavuja damu, lakini usivunjike.
Dunia hii ni uwanja wa vita vya ujanja, vita vya mahusiano, vita vya kifedha, vita vya amani, vita vya afya, vita vya nafsi na vita vingine vingi visivyojulikana.
Hivi havitaisha kamwe.
Vita hivi ni sehemu ya maisha. Huwezi kuviombea viishe. Huwezi kutamani viondoke. Utakutana na kushindwa na pia utashinda.
Kubali ukweli huu na ukweli kwamba mnyama mwenye nguvu zaidi si yule mkubwa, mkali au mwenye kasi zaidi, bali ni yule anayejifunza jinsi ya kuzoea mabadiliko na kuendelea kuishi.
Binafsi sitamlaumu mtu ambaye atanitenga kipindi sina kitu, Maana hata mimi sizipendi shida Ninazo zipitia, Ila nitamshangaa sana akirudi kipindi nimejipata, Maana hata mimi sipendi kuvuna ambacho sijakipanda.
Nini kinaendelea juu ya USAID!!
USAID, au U.S. Agency for International Development, iopo kikazi kwa zaidi ya miaka sitini kusaidia maendeleo sehemu mbalimbali duniani na hata Afrika.
Lengo lake ni kuboresha afya, elimu, ukuaji wa kiuchumi, na demokrasia, hasa katika nchi zinazokabili changamoto za umaskini mkubwa.
Lakini ghafla giza limeingia kuhusu USAID
UZI 🧵
Tarehe 17 May 2012, taifa letu lilishuhudia tukio ambalo limetokea mara moja tu kwenye historia na bado halijajirudia hadi sasa.
Majira ya saa 4 na dk 45 asubuhi msafara wa rais mkapa ulionekana ukiingia kwenye viunga vya mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
STORI YA KWELI KUHUSU KIJANA MDOGO ALIYEUWAWA KIKATILI SANA🙌🏿😭
Robert “Yummy” Sandifer alikuwa kijana wa miaka 11 kutoka Chicago, Marekani, ambaye alikua mmoja wa wahalifu wachanga wenye sifa mbaya zaidi katika historia ya Marekani.
Hadithi yake ya kusikitisha inaonyesha jinsi mazingira magumu ya kijamii na mfumo ulioshindwa unaweza kuchangia kuharibu maisha ya vijana wadogo.
Uziiii...🧵
Follow 👉🏿@mchache_tz