KINACHOENDELEA KIGOMA KUHUSU KIFO CHA DEREVA WA MHE. HECHE.
Anaandika Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Deogratius Mahinyila
Ni muhimu pia taarifa zikawa zinasemwa zote.
1. Marehemu pia alikutwa na pesa Cash na nilikabidhiwa mimi kiasi cha Shilingi laki 4 na elfu 28.
2. Alikuwa ametokwa na damu mdomoni.
3. Pathologist ambao ndo wanatakiwa kufanya postmortem walifika usiku wa kumkia leo wametoka Mkoani Mwanza na Geita hadi muda huu majira ya saa nane mchana na dakika bado Postmortem haijaanza.
4. Tumejulishwa kwamba kuna Pathologist mwingine anakuja kuungana na waliopo yeye anatokea Dodoma ni wa Serikali.
5. Tumejulishwa kwamba wataalam wote hao baada ya kufika Kigoma, leo asubuhi walipelekwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Simon Sirro, Hatujui walienda kufanya kikao cha nini na kwa ajili ya nini. Je huo ndio utaratibu wa kazi yao?
6. Hapo hapo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amenukuliwa na Clouds TV alisema kwamba kwa uzoefu wa Polisi (Yeye alikuwa IGP) kifo cha Maradufu ni cha kawaida tu. Je majibu ya uchunguzi yakija tofauti na maoni ya Polisi mtasemaje? Je majibu ya uchunguzi yakija kufanana na maoni ya Polisi mtakataaje kuwa ni matokeo ya mjadala uliofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo asubuhi??
6. Muda ni Mwalimu mzuri. Ukweli una tabia ya kuchelewa kidogo kibinadamu lakini lazima utajidhihirisha ndani ya wakati wake sahihi, tuupe muda nafasi.
7. Sisi tutaendelea kuwepo hapa Mochwari hadi hapo Wataalamu watakapofika na Uchunguzi kufanyika. Matokeo yoyote ya Uchunguzi yatatusaidia kuweka sawa kumbukumbu ya kila jambo.
Mahinyila.
02/07/2026.
Maweni, Kigoma.
Ukaribu na mamlaka haukuhakikishi kinga
Rev Peter Simon Msigwa
Moja ya makosa makubwa ambayo watu hufanya katika siasa na utumishi wa umma Tanzania ni kuamini kwamba ukaribu na wenye mamlaka ni kinga ya maisha yao ya kisiasa au kitaaluma.
Wanadhani wakionekana jukwaa moja na wakubwa, wakisafiri nao, wakikaa kwenye vikao vyao, wakisifiwa hadharani au wakitajwa kama “watu wa karibu,” basi hakuna kitakachowapata.
Huo ni udanganyifu mkubwa.
Historia ya Tanzania imeonyesha mara nyingi kwamba mamlaka hayana marafiki wa kudumu; yana maslahi ya kudumu.
Leo unaweza kuwa mtu wa karibu zaidi. Kesho unaweza kuwa mzigo unaopaswa kutupwa ili kulinda taswira ya mfumo. Katika siasa, maamuzi mengi hayafanywi kwa sababu ya urafiki, bali kwa sababu ya maslahi ya mamlaka.
Ndiyo maana ukaribu si kinga.
Ukaribu si agano. Ukaribu si bima. Ukaribu si ulinzi.
Mamlaka yanapokumbwa na msukosuko, shutuma au mabadiliko ya kisiasa, jambo la kwanza linalolindwa si watu waliopo pembeni yake; linalolindwa ni mamlaka yenyewe. Waliokuwa wakionekana kuwa muhimu jana wanaweza kusahaulika leo, na waliokuwa wakisifiwa jana wanaweza kuwa wa kwanza kubebeshwa lawama kesho.
Usikope kujiamini kwa sababu tu uko karibu na mwenye madaraka.
Jenga kujiamini kutokana na uadilifu wako, uwezo wako, weledi wako na msimamo wako. Hayo ndiyo mambo ambayo hayaondolewi na mabadiliko ya viongozi, uchaguzi, wala mabadiliko ya upepo wa kisiasa.
Kwa sababu siku milango ya mamlaka ikifungwa, swali halitakuwa “Ulikuwa karibu na nani?”
Swali litakuwa:
“Ulisimamia nini?”
Na kumbuka, katika siasa hakuna anayefukuzwa chini ya basi kwa bahati mbaya. Inapotokea mamlaka yanahitaji kujinusuru, mara nyingi hutafuta wa kumbebesha mzigo. Wakati huo, ukaribu wako wa jana haukupi kinga; unaweza hata kuwa sababu ya wewe kuwa mhanga wa kwanza.
Usijenge maisha yako juu ya kivuli cha mamlaka. Vivuli hubadilika jua linapogeuka. Jenga maisha yako juu ya tabia, uadilifu na ukweli. Hivyo ndivyo vitu pekee vinavyoweza kusimama wakati mamlaka, marafiki na nafasi vinapobadilika.
Kamwe usichanganye ukaribu na madaraka na ulinzi. Mara nyingi, watu wanaosimama karibu zaidi na moto ndiyo wa kwanza kuungua.
Tomorrow is another day - Tundu Lissu's trial continues
Madhulmat wajipange kesho maana wamezoea kuleta ujinga kila wakati! Safari hii hawachomoki
Hatutaki kusikia hili wala lile
Muachieni Lissu
#FreeTunduLissu
Baada ya video zangu za jana, nimeambiwa tatizo sio kwamba wanaharakati wanaona uvivu kuondoa comments za ku demoralize wananchi na mwishowe kuharabu harakati, nimeambiwa tatizo ni kwamba wanaharakati wengi wanataka engagement na followers.
Dah, basi tatizo ni kubwa kuliko nilivyodhani. Nilidhani labda ni uvivu tu ila ndo nimeleeweshwa kuwa wengi ni hawajali kama harakati zao zinaleta manufaa yoyote, wao wanataka engagement na followers regardless hata kama harakati zinaharibika na zinakuwa hazina mashiko kutokana na comments wanazoacha kwenye post zao.
Basi kazi ipo!!!!!
‼️ALERT‼️
Nimepokea taarifa kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Hospital ya Mkoa Kigoma (MAWENI) kwamba madaktari wa hospitali hiyo wapo kwenye pressure kubwa kutoka kwa wauaji kuhusu Uchunguzi wa mwili wa dereva wa Mhe. John Heche Mzee wetu Suez Dani Maradufu.
Waujaji wanawashinikiza Madaktari wa Maweni wachezee report (Postmortem) lengo lao wanataka ionekane Dereva wa Mhe. Heche amekufa kifo cha kawaida, Madaktari wameambiwa waseme alikuwa anaumwa ndo maana jana Polisi walikuja na propaganda ya kusema kwamba walipovunja mlango na kuingia kwenye chumba cha Suez Dani Maradufu, walipokagua walikuta anadawa nyingi kwenye kibegi chake jambo ambalo sio kweli.
Polisi wanahangaika kuwalazimisha Madaktari watoe taarifa ambayo itaendana na propaganda ambayo waliitoa jana kupitia kile kipeperushi chao ili kuhalalisha kifo cha Mzee Suez Dani Maradufu so tangu jana kuna mvutano mkubwa sana unaendelea Hospital ya Maweni.
Ikumbukwe tangu jana Viongozi wa Chadema walitaka mwili uchunguzwe kabla hawajaondoka nao Kigoma.
Madaktari wa Kigoma, wakasema kwamba wao hawana uwezo wa kuchunguza, wakaomba wataalam kutoka Mwanza ili waje wachunguze sasa Madaktari kutoka Mwanza walifika usiku wa kuamkia leo lakini mpaka muda huu bado hawajafanya chochote wanapiga dana dana.
Watanzania tunataka Uchunguzi wa KWELI ufanyike haraka ili tujue nini sababu ya kifo cha mpendwa wetu, chonde chonde Madaktari msikubali kutumika kutoa report ya uwongo ili kuwalinda wauaji, kitawaramba.
Tunapitia kipindi hiki cha giza ili tujifunze kuthamini Mwanga unaokuja!
Tusisahau haya magumu na uovu mkubwa wa hawa madhulmat ili yasije kurudia tena
Sasa tupige moyo konde - tumekaribia kumaliza hiki kipindi kigumu na tumeshashinda!
Just try to stay alive 💪🏽🔥
Mungu atusimamie katika yote 🙏🏽
#TutaelewanaTu
KINACHOENDELEA KIGOMA KUHUSU KIFO CHA DEREVA WA MHE. HECHE.
Anaandika Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Deogratius Mahinyila
Ni muhimu pia taarifa zikawa zinasemwa zote.
1. Marehemu pia alikutwa na pesa Cash na nilikabidhiwa mimi kiasi cha Shilingi laki 4 na elfu 28.
2. Alikuwa ametokwa na damu mdomoni.
3. Pathologist ambao ndo wanatakiwa kufanya postmortem walifika usiku wa kumkia leo wametoka Mkoani Mwanza na Geita hadi muda huu majira ya saa nane mchana na dakika bado Postmortem haijaanza.
4. Tumejulishwa kwamba kuna Pathologist mwingine anakuja kuungana na waliopo yeye anatokea Dodoma ni wa Serikali.
5. Tumejulishwa kwamba wataalam wote hao baada ya kufika Kigoma, leo asubuhi walipelekwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Simon Sirro, Hatujui walienda kufanya kikao cha nini na kwa ajili ya nini. Je huo ndio utaratibu wa kazi yao?
6. Hapo hapo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amenukuliwa na Clouds TV alisema kwamba kwa uzoefu wa Polisi (Yeye alikuwa IGP) kifo cha Maradufu ni cha kawaida tu. Je majibu ya uchunguzi yakija tofauti na maoni ya Polisi mtasemaje? Je majibu ya uchunguzi yakija kufanana na maoni ya Polisi mtakataaje kuwa ni matokeo ya mjadala uliofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo asubuhi??
6. Muda ni Mwalimu mzuri. Ukweli una tabia ya kuchelewa kidogo kibinadamu lakini lazima utajidhihirisha ndani ya wakati wake sahihi, tuupe muda nafasi.
7. Sisi tutaendelea kuwepo hapa Mochwari hadi hapo Wataalamu watakapofika na Uchunguzi kufanyika. Matokeo yoyote ya Uchunguzi yatatusaidia kuweka sawa kumbukumbu ya kila jambo.
Mahinyila.
02/07/2026.
Maweni, Kigoma.
Nimempoteza BRO WANGU MDUDE kwenye hizi harakati.
Leo kwasababu ya Njaa zangu nianze kujali tumbo langu nikatishe tamaa watanzania ambao wanaamua kuandamana kumpigania ndugu yangu?
Mimi miaka miwili nahudhuria clinic za TAYA yangu kwasababu ya KUPIGWA RISASI YA KICHWA—mnajua gharama ngapi naingia kujitibia?
Leo kwasababu ya njaa zangu nianze kukatisha tamaa watanzania wenzangu walioamua kuandamana kunipazia sauti kukataa haya mambo ya KUTEKA NA KUPOTEZA WATANZANIA?
Mimi sina BEI kwenye haya mapambano, bei yangu ni HAKI itendeke, kinyume na hapo NITANYOOKA NA NYIE MPAKA NAKUFA.
Nipo tayari kuishi mafichoni milele.
Nipo tayari kuendelea kuishi kwa mashaka milele.
Nipo tayari kuendelea kuishi kwa tahadhari milele.
Haya yote ambayo yananiumiza leo nipo tayari kuyageuza kuwa maisha yangu ya milele ila najua siku moja USHINDI UNAKUJA.
Kwahiyo ndugu zangu MAANDAMANO YA 7/7 NAYAUNGA MKONO ASILIMIA 200–HII NCHI LAZIMA TUIKOMBOE TUANZE UPYA.
#77Tunatoka
#FreeTunduLissu
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Leo #MariaSpaces tunajadili: Maandamano ni haki kikatiba, tusijitetee bali tujipange kutekeleza 7/7
Maandamano si uhalifu na ni haki ya kikatiba! Mafedhuli wanatututisha na utekaji, mauaji na ukamataji kana kwamba ni kosa! Tusitetereke tutekeleze! Mikakati leo saa 2 uck!
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Magharibi, Wakili Dickson Matata, akizungumza kuhusu mwenendo wa zoezi la postmortem ya mwili wa marehemu Suez Dani Maradufu, aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mheshimiwa John Heche.