"Pambaneni mpate Katiba mpya," wakati mnaokota vijana mnawapa kesi za UGAIDI ati sababu walitaka kuandamana.. maelfu wameuwawa, wametekwa, wameteswa, wamepotezwa, wamedhalilishwa kingono, na zaidi tunawindwa tuuwawe kwa kutoa maoni tu! Hivi Nchimbi anatuonaje?
Ukiachana na tatizo la ukosefu wa ajira, soko la ajira kuwa over loaded na man power value kushuka, vijana tumekuwa watu wa hovyo sana.
Hatuna weledi na umakini tukipewa kazi, uaminifu hakuna, viburi vya kijinga na tamaa za hapa na pale.
Huu utumwa unaofanywa na makampuni ya mafuta ni hatali kabisa
Malipo ya dereva yanakuwa kwa mileage badala ya siku ? mtu anapokwenda CONGO au Malawi anapopata changamoto njiani siku zinaongezeka za kukaa huko na matumizi yanaongezeka
nchi kama Congo fedha yao ina thamani kubwa, matumizi huko ni makubwa pia
Kwa nini madereva wanalipwa kwa mileage na sio siku wanazokaa barabarani?
Hii sekta ina watu wanaisimamia kweli ?
Maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Kigoma yatatangazwa hivi karibuni na viongozi wakuu wa chama. Nina matumaini kwamba yatatoa majibu kwa kelele na mijadala mingi iliyoibuka hivi karibuni. Hata hivyo, iwapo italazimu kutetea heshima yangu binafsi dhidi ya kauli mbalimbali za dharau na upotoshaji, nitafanya hivyo kwa ufasaha. Nasikitika kwamba naweza kujikuta katika jaribu hilo, lakini heshima ya mtu si jambo la kupuuzwa.