#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 2
Huyu sasa ni shaidi wa pili baada ya yule wa kwanza ambae ni George.
Tarehe 03/04 mtumiaji wa mtandao huo wa YouTube yaani akaunti ya JAMBO TV alichapisha maudhui yakiyojulikana TUNDU LISSU uso kwa uso na watia nia chadema.
Katika video hiyo Lissu alisema majaji ni maccm, mapolisi wanaiba kura na vibegi na uchaguzi wa 2024 Rais alitoa maeleekezo kuwa wapinzani wasiende kokote. Yaani walienguliwa na maccm.
Pia alisema mimi nataka kacheo na nyie hamtaki kacheo sasa tunaweza kushinda au kushiriki uchaguzi wa aina hii? Sas amsimamo wetu kama Chama ni No Reforms no Election tunasimamia hapo.
Nilipakua video hiyo kwenye ukurasa wa JAMBO TV na kuiwasilisha.
Maelezo ya shaidi wa tatu PF ... Insp. Andrew Churu nae maelezo yake yanasomwa.
Mimi natokea Dodoma nafanya kazi huko na maelezo haya nimeyatolea Dar es salaam. Niko polisi toka 2000 nafanya kazi ofisi ya DCI makao makuu Dodoma. Tar. 07/04 nilipigiwa simu na DCP kuwa yupo.mfanyakazi wa JAMBO TV yuko Dodoma akanitumia namba ya simu ili nimtafute.
Siku hiyo alikuja shahidi hiyo na camera yake na kutoa ushirikiano ambapo alinipa memory card ambayo ilikuwa na video ya Lissu. Alifungua camera na kunipa kidhibiti hicho na tukaaandikiana uthibitisho wa nyaraka hiyo.
Nilimuhoji kuhusu ufahamu wake wa tukio hilo alipoenda pale Makao makuu ya Chadema na yeye ametokea Jambo TV alirekodi kupitia camera hiyo. Anakiri kuwa walipandisha instgram na mitandao mingine. Na nilielekezwa kuwa nivipeleke Dar es salaam siku hiyo hiyo na kuleta Dar es salaam.
Nikakutana na afande George Dar es salaam kwa ajili ya kumkabidhi vifaa hivyo vyote kwa maandishi.
Shahidi wa 4 ASP Kaaya ni ushahidi unaofuata.
Samwel Elibariki Kaaya mimi ni mtaalamu wa picha ni Askari wa Jeshi la Polisi ninafanya kazi ya kupiga picha za mnato.
Nilipewa vifaa vya kuvifanyia uchunguzi ikiwemo adapter, flash disk, barua na vifaa vingine nikitakiwa kufanya uchunguzi wa video mbalimbali. Zilizokuwepo kwenye memory na flash disk. Nilitahijika kuthibitisha uhalisia wa video hizo kitaalamu. Maudhui yenyewe ni yale mapolisi kuiba kura na vibegi, majaji ni maccm na taarifa kama hizo.
Chanzo cha picha mjongeo hizo ni kipi na zimetoka wapi ndio kazi yangu niliyotakiwa kufanya.
Niliakgua vifaa vyangu kuona usalama wake, Vilikuwa salama na imara kufanya kazi hiyo.
Baada ya uchunguzi wa kitaalamu niligundua picha mjongeo nilizopewa niligundua ni halisi kabisa na nikaandaa taarifa na kusaini taarifa hiyo.
Shahidi wa tano anaitwa " P"huyu ni mzaliwa wa Dar na mwaka umefichwa na ni mtoto wa kwanza. Nilisoma shule .... nilijiunga chuo cha kilimo na niliishia elimu ya certificate. Na 2020 nilijiunga chuo cha DSJ 2021 hadi 2023 na kujiunga na JAMBO TV kama mpiga picha kazi ninayoifanya hadi leo.
Nilihudhuria mkutano wa Chadema. Uliofanyika makao makuu chadema. Ulihudhuriwa na watia nia na mh. Lissu alihutubia. Tulienda wafanyakazi watano wa jambo na tukaenda. Niliona tangazo kupitia mkurugenzi wetu.
Tulikuwepo waaandishi wengi ikiwemo wa Azam na vyombo vingine tulirusha live tukio lile sisi jambo TV.
Masuala yaliyokuwa yakiongelewa ni kuhusu suala la Uchaguzi na mambo yaliyokuwa yakiongelewa ni uchaguzi na no reforms: No election na kikubwa ni matatizo wanayokutana nayo kama Chama katika chaguzi zao. Mambo hayo yapo kwenye memory kama nilivyokukabidhi yapo humo. Kikao hicho kilifanyika masaa mawili hadi matatu. Na baadae waandishi tuliondoka na wenzetu tukawaachia
Maelezo ya shahidi wa 6 anaitwa P2 nae anaanza baada ya yule aliyepita.
Mimi ni mkazi wa matalawe ni mkazi wa matalawe. Sijao sina mtoto ni mfuasi wa CHADEMA toka 2021 na ni mshabiki wa tundu Lissu nililjpia kadi ila sijapata kadiyangu. Nimekuwa namuunga mkono Lissu na kwa songea mwenyekiti wetu wa BAVICHA ndio kiongozi wetu ambae almaarufu kama mwamba wa Kigoma.
Part 3 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Retweet yako
Tanzania is officially a police state.
Hawa ni polisi wanazuia watu kuabudu kwasababu Askofu wao amekemea utekaji.
Kwamba Gwajima angepongeza watekaji leo kanisa lake lisingefungwa.
Kama uku tayari kumlinda mwenyekiti @TunduALissu kwa wivu mkubwa sana na watu wenye Nia ovu ya kukwamisha uongozi wake ndani ya chama.Retweet hapa nikuone kamanda
VIDEO:
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA @bavicha_taifa Wakili Deogratius Mahinyila @AdvMahinyila ametoa wito kwa wanachama wa @ChademaTz kuungana na kusahau u-timu waliokuwa nao wakati wa kampeni za uchaguzi.
Wakili Mahinyila amesema hayo leo Februari 16, Ikungi mkoani Singida akieleza kuwa ni vyema wale waliokuwa wakiunga mkono upande ulioshinda (Upande wa Mwenyekiti wa chama Tundu Lissu @TunduALissu ) kuwa na busara na kuepuka kujipa kuwadharau au kutoa maneno ya kejeli kwenda upande ambao haukushinda(upande wa Aliyekuwa Mwenyekiti Freeman Mbowe @freemanmbowetz).
Aidha Mahinyila ameutaka upande ule ambao pia haukushinda kuungana na upande ulioshinda kukijenga na kufikia malengo ya chama hicho.