Si lazima nielewe kila kitu ambacho Mungu anafanya ili niendelee kumwamini.
Mawazo yake ni makubwa kuliko yangu, na njia yake inaweza kuwa bora kuliko niliyoipanga.🙏🏼
kumbuka wewe mwananchi huna huu upendeleo. ukifanya kosa, sheria inachukua mkondo wake. muda mwingine hata kosa huna. lakini sheria hiyo hiyo haifanyi kazi kwa kiongozi wa serikali. wao wapo juu ya sheria. wanalindwa. wanahamishwa vituo. #JamhuriyaNdizi:
Nobody wants a city on Mars. Nobody wants AI in every app. Nobody wants data centers in space. Nobody wants humanoid robots or flying cars.
We want clean water. We want a stable climate. We want a habitable planet. We want wildlife to survive. We want to live.
@YerickoNyerereT Nimesoma kitabu cha UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI nimeona jinsi mwl Nyerere alivyokuwa anapewa pesa na Mashirika ya nje chini ya mwamvuli wa kanisa katoliki ili kuchochea harakati za uhuru wa Tanganyika, na ww kama mwandishi wa kitabu kile ulisfia uamuzi ule, leo unashangaa kuona
IWE KIFUNGO AU KIFO.
1.Msimamo wangu kuhusu Muungano uko Bayana. Tuwe na Serikali Moja au la Tuwe na Serikali Tatu.Hatuwezi kuwa na Muungano ambao Taifa moja linabaki na mambo yake yote halafu mambo yote ya Taifa lingine yanageuzwa kuwa ndiyo mambo ya Muungano .Kama hatuwezi kuwa na Serikali Moja kama ilivyokuwa kusudio la awali la waasisi wa Muungano lazima tuwe na serikali tatu.Tanganyika,Zanzibar na Mungano.Tuache hoja za kipropaganda kwenye mambo serious.
2.Msimao wangu kwamba kila raia ana haki ya kuwa na maoni huru na kuwa na mtazamo huru au kushawishi mtizamo wake ukubalike na kwamba kufanya hivyo siyo Uhalifu wala uhaini.Kufanya Maandamano,Midahalo au Maongezi kuhusu hali fulani ya kiutawala,demokrasia,sheria au uwajibikaji siyo uhalifu na watu wote wanao kamatwa na kushtakiwa kwa makosa makubwa wana haki ya kuwakilishwa na wakili mwenye uzoefu na Wakili kuwawakilisha watu wa namna hii anakuwa hajafanya kosa lolote.
3.Uchaguzi wa Tarehe 29 Oktoba hauna sifa ya kuwa uchaguzi huru na Wazi na haukukidhi vigezo vya kuitwa Uchaguzi huru na Haki.Rejea Ripoti za wasimamizi wa Uchaguzi SADC,AU na wengine.Ukitawaliwa na vificho,mauwaji,kuwekwa kizuizini kwa chama kikuu cha Upinzani na kuzuiwa kushiriki uchaguzi, uchaguzi kufanyika gizani na Kukosekana kwa Tume Huru ya Uchaguzi.
4.Namna ya Kutoka hapa tulipo ni kuhakikisha kusitishwa mara moja kwa ukamataji hovyo wa vijana na kuwabambikia kesi,Kufutwa kwa kesi zote za uwongo dhidi ya chama kikuu cha Upinzani na uwepo wa Tume huru ya Kiuchunguzi ya Kimataifa ambayo Ichunguze Mauwaji na upotezwaji wa watu kuanzia kabla,wakati na baada ya Uchaguzi na iangazie uhalisia wa Takwimu za uchaguzi na matokeo yake. Na ndiyo ije na mapendekezo ya hatua za kuchukua.
5. SERIKALI itoke hadharani Ikiri kwamba yenyewe ndiyo chanzo cha kusababisha Vijana waandamane kwa ujeuri wa viongozi wake na kutopenda kusikiliza ushauri na kwamba vijana wale hawakuwa na njia nyingine ya kueleza hisia zao kwani Mahakama ilikwisha onekana kutokuwa sehemu sahihi kitoka na aina ya utitiri wa Maamuzi hususan kupotzwa kwa watu na Bunge lilikataa kata kata kujadili matatizo ya wananchi na kujigeuza kikaragosi cha serikali na hawakuwa na njia nyingine isipokuwa hiyo na kuwa kwa Makusudi au Uzembe iliruhusu vyombo vyake vya ulinzi kutumia sila za moto dhidi ya waandamanaji na wasio waandamanaji na kuuwa wananchi hata wale ambao hawakuwepo kabisa katika maandamano ikiwemo watoti wadogo na akina mama walioshambuliwa katika nyumba zao.
6.Wahanga wote na Familia zilizoathirika serikali iwajibike kuonesha wapi waliko waliotekwa na kupotezwa na pia ioneshe miili ya wale wote waliouwawa katika sakata la Oktoba 29 na kuhakikisha kuwa wale waliohusika kutekekeza mauaji haya wote wanachukuliwa hatua za kisheria.
7. Msimamo wangu kuhusu sakata linalohusiana na uchaguzi ni kwamba Taifa linahitaji UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI.Baada ya hapo ndipo tuone namna bora ya kuwa na uongozi jumuishi unaowasilisha ridhaa ya wananchi kwani hawa waliopo sasa japo dejure ni viongozi de facto wanakosa uhalali wa Kijamii kupitia mazingira ya namna zoezi la uchaguzi lilivyo endeshwa.
8.Kwamba Maandamano ya Gen.Z kupinga dhuluma za kidemokrasia siyo uhalifu ...bali ni matokeo ya ukaidi na kutopenda mashauriano kwa baadhi ya viongozi wajuu wa serikali jambo linalopelekea vijana kukata tamaa na kukosa matumaini. Tusipo jifunza kutatua mambo yetu kwa kuzungumza asili itatufunza kutatatua mambo hayo hayo kwa kupigana.
TUSIWINDWE ILI KUUWAWA AU KUBAMBIKWA KESI KWASABABU YA MISIMAMO YETU ..HOJA HAZIPIGWI RUNGU.