husband๐ซ | father ๐จโ๐ฉโ๐ง| politician โ| farmer๐ |enterpreneur....| future Mp.| am real i never fake life...fear always fear me and i always face it direct..
HERI YA SIKU YA KUZALIWA, MHE. @HecheJohn โ๏ธ
Leo tunaungana na maelfu ya Watanzania kumtakia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche, heri na baraka tele katika kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.
Katika siku hii ya kipekee, zawadi yenye thamani zaidi tunayoweza kumpatia si maneno pekee, bali ni kuendelea kuunga mkono wito wake wa kujenga chama imara kwa kuchangia kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
Mhe. John Heche amekuwa mstari wa mbele akihamasisha Watanzania kushiriki katika ujenzi wa chama. Hivyo, tunawaalika wanachama, wapenzi na marafiki wa CHADEMA kuadhimisha siku hii kwa kutuma mchango wao kwa ajili ya Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334.
Zawadi bora kwa Mhe. John Heche ni kuona Watanzania wakijitokeza kwa wingi kuchangia Baraza Kuu la Umma. Kila mchango, mkubwa au mdogo, ni sehemu ya mafanikio ya chama chetu.
Heri ya kuzaliwa Mhe. John Heche! Mwenyezi Mungu akupe afya njema, hekima, nguvu na ulinzi unapoendelea kulitumikia Taifa na CHADEMA.
CHANGIA KIKAO CHA BARAZA KUU KITAKACHOFANYIKA TAREHE 15/09/2026
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
SWEZI DANIEL MARADUFU
Nimekufahamu nikiwa kijana mdogo kwetu Tarime. Ulikuwa unamlinda mdogo wako, EMMANUEL aliyekuwa na changamoto ya akili, kwa upendo.
Mzee MARADUFU alikuwa mtu muungwana lakini mkali. Sisi kwenye familia, jina lake tulichukua kwa utani, tukaanza kumuita mzee Maranja.
Ulikuwa dereva wa magari ya Mzee Suguta Heche yakifanya safari zake kuanzia Tarime kwenda Mugumu (Serengeti) kupitia Sirari na Nyamongo
Magari yalikuwa ni zile Land Rover 109 Mandolin a.k.a Londo. Ulikuwa ukiyapiga gia mbaya mbovu kabisa. Ulikuwa VETA ya vijana wengi Tarime.
Mzee Heche alipofariki, uliendelea na shughuli zako, baadae ulikuwa dereva wa John Heche katika kampeni zake, ukaendelea alipokuwa MBUNGE.
Umeendelea kuwa dereva binafsi wa John Heche hata wakati alivyokuwa siyo kiongozi wa juu wa chama chetu hadi sasa ni Makamu Mwenyekiti.
Sisi wote kwa pamoja tunatoka Kata ya Bomani, Tarime Mjini kama ilivyo kwa John Heche. Wewe ni mtoto wa nyumbani. Huu ni msiba wetu.
Ni msiba mkubwa kwetu watu wote wa Tarime tuliokufahamu. Kifo chako cha ghafla kimetuachia majonzi na maswali mengi na hatuna majibu.
Tunasubiri taarifa muhimu za kitabibu ili tupate kitu cha kusema. Ndugu yetu, hatimaye, umekwenda kufariki ardhi ya mbali na nyumbani, Kigoma.
Pole sana ndugu yangu John Heche na familia yako kwa kupoteza rafiki na ndugu yako wa muda mrefu. Pole sana kwa familia ya Mzee MARADUFU.
Poleni sana wanachama wa CHADEMA. Poleni watu wa Tarime. Hakika, BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe. Ayu 1:21
Pumzika kwa amani, AMIGOLAS MAMBYA. ๐๏ธ