Look on hawa sister waliozaa kabla ya kuolewa na hawana Ramani kitaa.
Halafu angalia wewe mwanaume unaepambana japo maisha yamekunyokea then angalia nani kachalala.
Bro wewe ni wa thamani.
The best prayer ambayo kila binadamu anapaswa kuomba ni Mwenyezi Mungu kumpa utambuzi wa kujua kwanini unaishi, kwani without purpose (kusudi)kuzaliwa inakuwa kazi bure,batilli na mzaha mtupu ktk maisha yetu hapa Duniani.Hasara inayotokana na kupenda haki ni faida kubwa kuliko faida inayopatikana kwa njia ya hila lakini tu utajua kama una weza kuwa na tafakari ya rohoni.Fahamu kuwa Binadamu ni Roho anayo nafsi na anaishi ktk mwili.Ndio maana mtu akifa tunasema mwili wa marehemu huko mochwari. Ukipotea njia speed inakosa maana.
Ulikuja duniani huwezi kuongea kila kitu walikusemea na utaondoka duniani huwezi kuongea, kila Mtu atasema analojua.
Siku ya kwanza kufika duniani ulilia sana na siku unayoondoka utawaliza sana watu, ingali wapo watakaofurahia.
Uliishi kwenye tumbo la Mama kwa miezi tisa na siku ya mwisho utaondoka kwenda kuishi milele kwenye tumbo la ardhi peke yako.
Kwenye birthday yako unakata keki na kushangilia ila siku ukiondoka tarehe ya kifo chako watachoma mishumaa na kuomboleza.
Ulikuja duniani ukiwa mtupu bila nguo na utaondoka mtupu bila nguo.
Ulikuwa Kiongozi mkubwa na walinzi kila kona ila kwenye jeneza utakuwa peke yako na Walinzi pekee ni Malaika wako kama ulifanya mema, inatisha sana.
Ulipofika duniani walipambana kutafuta jina lako kwa furaha kubwa ila siku ya mwisho jina pekee ni Marehemu ambalo kila Binadamu atalibeba, majina ni mengi sana ila jina la kipekee ni hilo moja tu.
Ulikuja duniani bila pesa na utajiri wowote na utaondoka bila chochote ulichovuna ama kupanda.
Kwa mara ya kwanza ulipofika duniani uliogeshwa na siku ya mwisho unaondoka kuna Mtu atakuogesha.
Ulikuja duniani ingali Mdhaifu kila kitu wanakufanyia na utaondoka dhaifu kila kitu watakufanyia watu wengine.
Unajua nini? Tuna muda mchache sana duniani, fanya mema, heshimu watu na tumia muda wako vizuri, kesho hajaahidiwa mtu yoyote.
Umeelewa maana ya maisha? Ni kuwa hupaswi kuishi kwa kusema watu, hupaswi kuogopa watu ila chagua amani nyakati zote kwakuwa maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana na utaondoka peke yako.
MKULIMA WA BONDE LA MTO KILOMBERO, MOROGORO🇹🇿
Maji💦 → Kwa Ajili ya Figo!
Mayai 🥚→ Kwa Ajili ya Ubongo 🧠!
Carrots🥕 → Kwa Ajili ya Macho!
Nanasi 🍍→ Kwa Ajili ya Koo!
Cabbage 🥬 → Kwa Ajili ya Utumbo!
Tango 🥒 → Kwa Ajili ya Ngozi!
Tangawizi → Kwa Ajili ya Koo na Mapafu!
Parachichi & Nyanya 🥑 → Kwa Ajili ya Afya ya Moyo 🫀!
Mazoezi exercise🏋️ → Kwa Ajili ya Afya imara na Kinga Bora ya Mwili!
Mboga za Majani 🥦🫑 → Kwa Ajili ya Kuongeza Kinga yako ya Mwili.
Furaha 😆 → Kwa Ajili ya Afya yako ya Akili!
KuRepost 🔄 → Kwa Ajili ya Wengine!
NUKUU YA LEO: “Ujana ni umri wa thamani sana, isifike muda ukajikana na kujikatia tamaa, fanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi hakika utafanikiwa.” - Ivona Kamuntu
So guys, huu hapa mchango wangu wa senti mbili juu ya kuanza kitu:
1. “Elimu haijawahi kumtupa mtu.” Hii ni kauli aliitoa mwanetu mmoja tukiwa intern residences pale Muhimbili. Alikuwa amemaliza internship yake akaitwa interview sehemu, akafanikiwa kupata ajira. Starting salary ikawa 1.5m. Alirudi akatulia kwenye kochi kisha akalia sana, tukamuuliza kulikoni akasema tu “elimu haijawahi kumtupa mtu!”. Enzi hizo tulikuwa tunagomea mshahara wa kuanzia wa sh 126,000/-!
Aidha, pale Kitongo S/M nilipofundishwa kusoma na kuandika kulikuwa na motto “elimu ni ufunguo wa maisha!”. Sikuwahi kujua maana yake enzi hizo ila leo naelewa wazee wetu walimaanisha nini.
2. Jitihada hazishindi Kudra za Mwenyezi Mungu lakini “Mguu uliotoka Mtume kauombea!”
3. Kila kitu kinaanza na mindset/mentality sahihi. Clear kichwa chako kwanza, Ondoa kichwani takataka, uvivu, uzembe, ujanja ujanja, ujinga, wasi wasi, mashaka; replace na fikra safi na mawazo ya kule unakotaka kufika. Jielimishe, Jaza maarifa, ujuzi na taarifa za kule unapotaka kufika.
4. Tafakari juu ya wazo lako. Lichakate kisawasawa. Fanya utafiti. Mara nyingi idea nzuri ya biashara inaenda kutoa huduma ama product wanayohitaji wanadamu kwenye maisha yao ya kila siku, kwenye familia ama jamii, ya kihisia zao ama kimwili/kiafya - mambo ambayo yanafanya maisha ya kila siku yaende.
5. Wengi hudhani ili ufanye biashara basi unatakiwa kwanza uwe na mtaji. Hivyo kelele za kuwezeshwa na serikali huwa nyingi sana. Ila kiukweli, Mjasiriamali mahiri na makini huwa anakuwa na wazo zuri la biashara linalomkosesha usingizi! Mtaji na mengine huja baadaye.
6. Ukiishakuwa na wazo - Pamoja na utafiti, hakikisha unalitazama soko vizuri sana. Kwamba huduma ama product yako utamuuzia nani? Utaitangaza vipi? Nani mshindani wako? Utawashinda vipi?
7. Kwa vyovyote vile, uwe umesomea ama hujasomea marketing ama hujui strategy - Kuna mkakati mmoja tu wa kuuza, nao ni ‘JITOFAUTISHE’ sokoni, basi. Nyingine ni mbwembwe.
8. Ukiishajiridhisha juu ya haya yote, sasa utatafuta majibu ya maswali ya mtaji, teknolojia inayohitajika, mahala pa kuweka biashara yako, wataalamu wanaohitajika nk. Wengine huandika business plan etc
Ntaendelea baadaye kidogo….
#HK #Fighter #NjeYaBox
Shukuru sana kama
1. Una afya bora
2. Una chakula ndani
3. Una mahala pakulala
4. Una mtu anayekupenda
5. Una shughuli inayokuingizia kipato
6. Una familia inayokujali na kukuthamini
Ukipewa haya jitahidi usaidie na wengine
For boys (na Labda wasichana pia wanahitaji kusikia haya! 🤷🏾♂️):
1. Hakikisha unaoa. Kuoa ni lazima. Kuoa siyo lazima uwe na pesa. Ukikua kiasi cha kuzalisha mwanamke, oa! Mengine yatajipanga. Uoe nani sasa, sikia mtazamo wangu!
2. Oa tu mwanamke kama unampenda na una nia ya kuanzisha familia iliyo bora. Oa mwanamke atakayekuwa rafiki mzuri kwako na mama mwema kwa wanao. Oa mwanamke mwenye MUNGU ndani yake. Ni bonus ukipata mwenye shape, lakini lazima awe na Mungu ndani yake.
3. Ikitokea ukaoa usiwe mwepesi kutoa talaka. Ipambanie ndoa yako isimame. Hakuna viumbe wagumu kuwaelewa kama wanawake. Wanadamu tuko wawili tu - Ke na Me! 😀. Lakini Ke my brother, ni mgumu sana kumuelewa. Ukiishaamua kumuoa, jifunze kumvumilia, kumhurumia, kumpuuza (akianza maneno, maana kwa uhakika ataanza tu!)
4. Usije ukarogwa hata siku moja ukamuoa msichana ambaye ana MENTALITY, ya kuwa eti Wewe ni chanzo chake cha pesa na maisha mazuri; ila zingatia tu kwamba wanawake wote duniani watakupenda na kukukubali kama una pesa!
5. Jua kwamba ni jukumu lako kumhudumia mwanamke wako, lakini mwanamke aliye bora ni yule asiye na mentality ya kukuchuna, ni yule mpiganaji anayezalisha chake, anayeweza kukizalisha chako/chenu na anayeweza kukusaidia kujenga maisha ya familia yenu.
6. Mwanaume kamili aliye bora haulizi kipato cha mkewe, hamgawii mwanamke majukumu ya familia (hata kama mwanamke ana kipato kikubwa kuliko yeye). Zingatia neno ‘mentality’ ya kiume. Na mentality ya ‘kike’! Kaa kwenye mentality yako, ila kama ulichagua mwanamke sahihi, ata-step in kuinyanyua familia na hali ya maisha yenu bila kuambiwa, bila kulalamika, kwa siri na staha kubwa, na bila kukudhalilisha.
7. Epuka kukaa kwenye mahusiano na mwanamke anayekuomba nauli kila siku mkitaka kwenda out, anayekuomba pesa ya salon kila mkitaka kutoka, anayelewa pombe sana, anayependa kuwasiliana na kujenga urafiki na wanaume wengine, anayependa kufuatilia maisha ya couples nyingine na kujifananisha nao, anayetamani vitu vikubwa vikubwa wakati anakuona unajitafuta!
8. Epuka kuwa na mahusiano na mwanamke anayeona anakupa favour kuwa na wewe, anayeona uzuri wake ama show zake kitandani ndiyo kila kitu!
9. Epuka kuwa na mwanamke anayeona wewe siyo saizi yake sema basi tu, asiyeweza kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake, asiyejivunia kuwa na wewe, asiyeweza kwenda out na wewe! Epuka huyo!
10. Epuka mwanamke mwenye password nyingi sana kwenye simu yake, anayesevu namba za wanaume kwa codes, asiyeweza kupokea simu mbele yako, anayeweka airplane mode mbele yako, anayezima data mbele yako, anayeanzisha biashara bila wewe kujua mipango yake, anayependa sana kujiremba hadi kupitiliza! Epuka huyo!
#HK #Fighter #NjeYaBox