#OnThisDay in 2⃣0⃣1⃣9⃣ we visited Tanzania to face Simba SC in a friendly 🇹🇿
An unforgettable experience sharing football and friendship with our Tanzanian friends ❤️🤍
02
Hata kabla ya sheria nyingi kuandikwa,dhamiri tayari ilikuwa imeanza kushtaki.
Ndiyo maana ukweli mkubwa ni huu:Unaweza kuwadanganya watu kwa muda.Unaweza kuikwepa sheria kwa muda.Lakini ni vigumu sana kuikwepa dhamiri yako mwenyewe milele.
Kwa sababu dhamiri ya mwanadamu…ni mahakama ambayo haifungwi milele.
Kuna watu wanatembea huru leo,
lakini akili zao zimekuwa magereza yao.
Watu waliovikwa medali,
waliosifiwa majukwaani,
waliosalimiwa kwa heshima kubwa—
lakini usiku wanashindwa kulala wakiteswa na kumbukumbu
ambazo hawawezi kuzizika.
Kwa nini?
Kwa sababu kuna tofauti
kati ya kile kilicho halali
na kile kilicho sahihi mbele ya ubinadamu.
Mtu anaweza kuwa anafuata amri…
lakini bado akawa anasaliti utu wa mwanadamu.
Historia imejaa askari waliokuja kukiri baadaye:
“Tulikuwa tunafuata maagizo.”
Lakini dunia imejifunza kwa uchungu:
uovu hauwi haki
kwa sababu tu umeamriwa na mamlaka.
Na leo hii,
onyo langu linaenda kwa kila kiongozi,
kila taasisi,
kila afisa,
na kila mwanachama anayelinda mfumo bila kuhoji:
Tusijenge taifa
ambalo utii ni muhimu kuliko dhamiri.
Kwa sababu taifa likifika hapo,
watu huacha kutetea ukweli
na kuanza kutetea mamlaka.
Na mamlaka yanapoanza kuogopa uwajibikaji, kufichiana
(cover-up)huanza.
Na cover-up inapoanza,
haki huanza kufa.
Na haki ikifa,
taifa linaweza kuonekana lina amani kwa nje
lakini ndani linaoza taratibu.
Ndugu watanzania wenzangu
Taifa lenye afya si taifa lisilo na wakosoaji.
Taifa lenye afya
ni taifa ambalo ukweli bado unaweza kupumua.
Uzalendo si kulinda makosa.
Uzalendo wa kweli
ni kulipenda taifa lako kiasi cha kuthubutu kukemea
kile kinacholiharibu.
Watu hatari zaidi katika jamii yoyote
sio tu wale wanaofanya maovu
bali wale wanaoyahalalisha,
wanaoyatetea,
au wanaonyamaza
kwa sababu wahusika ni “wa upande wao.”
Leo nauliza:
Tunataka kuwa taifa la namna gani?
Taifa linalotawaliwa na hofu?
Au taifa linalotawaliwa na haki?
Taifa la watu wanaotii bila kufikiri?
Au taifa ambalo dhamiri bado ina thamani?
Kwa sababu ipo siku,
vyeo vitaondoka.
Serikali zitabadilika.
Vyama vya siasa vitapita.
Lakini historia itabaki.
Na historia haina huruma
kwa viongozi waliochagua mamlaka
kuliko ubinadamu.
Tusije tukawa taifa
linalozika ukweli kwa kina sana
mpaka vizazi vijavyo virithi ukimya wetu kama mateso yao.
Kwa sababu…
Hatia haina kaburi.
Rev Peter Simon Msigwa
Iringa
From the past to the present! Proud to be part of the @Arsenal family and to see our team defending our legacy.
Come on Gooners, we're @premierleague 𝐜𝐡𝐚𝐦𝐩𝐢𝐨𝐧𝐬! 🏆❤️🤍
KAN U believe it??? Arsenal Forever. The Gunners worked so hard for this. Difficult but they fought.
Very well deserved. Come on you gunners #congratulations@arsenal#arsenal