HILDA 'ATEKWA' AKIWA NA MTOTO MDOGO
Ndugu Watanzania! Tumearifiwa ya kuwa mwalimu Hilda Mbinda wa Shule ya Msingi mojawapo ya Gairo, Morogoro. Alichukuliwa katika mazingira tatanishi akiwa kwake tarehe 21 Oktoba 2025.
Lakini tulipopekua ukurasa wake wa Facebook, tuliona aliposti picha ya Gerson Msigwa ikiwa na maudhui ya kumkosoa na kwa muono wetu, Hilda alifanya vile kama msomi. Katika wiki za hivi karibuni, inasemekana Hilda alipishana kikauli na Mkuu wa Wilaya aliyetembelea Shule yao ambapo Hilda alikuwa Kaimu Mwalimu Mkuu wa kuwa Mwalimu Mkuu hakuwepo siku hiyo ya tukio.
Kwa maelezo ya aliowasimulia baadhi ya watu, inasemakana huyo Mkuu wa Wilaya alionyesha kutamka maneno ya 'kumkamia'! Inaelezwa pia kuwa wiki chache baadaye alianza kupigiwa simu na watu waliojitambulisha kutoka ofisi ya DCO. Lakini alipoulizia, Ofisi hiyo ilikana kuwa ilikuwa na haja naye.
Siku chache kabla hajachukuliwa, watu watatu kutoka Ofisi ya DSO walifika shuleni wakiwa ndani ya gari ambapo wawili waliingia Ofisi ya Mwalimu Mkuu na mmoja akabaki nje kuongea na Hilda na aliongea naye kwa muda mrefu pia. Baadaye, Hilda akapata barua ya uhamisho wa Kituo cha kazi.
Tukiangalia maelezo hayo hapo juu kutoka kwa 'wasamaria wema' tukioanisha na maelezo ya chini kutoka kwa mtu aliyejitambulisha ya kuwa ni mwalimu tunatoa hitimisha ya kuwa Hilda amechukuliwa na watu wa mfumo au watu wa serikali. Tunatoa wito kwa wahusika kutoa kauli juu ya wapi alipo Hilda na kuwajulisha nduguze na kama ana tuhuma wampeleke mahakamani kesho, la sivyo wamuache huru bila masharti.
Lakini habari kuwa Hilda amechukuliwa wakati akiwa na mtoto mdogo na kuwa huyo mtoto anaharisha sana inatuumiza sana. Tunawataka wahusika wampeleke mtoto hospitali mapema sana iwezekanavyo!
Kwa kuwa hakuna mamlaka yeyote iliyojitokeza kusema kuwa inamshikilia mwalimu Hilda, kwa sasa nduguze wanashikilia msimamo wa kuwa ndugu yao 'ametekwa'! Ni vigumu kuthibitisha ya kuwa yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi na ikiwa Jeshi halijakiri hivyo.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Hilda Mbinda alichukuliwa juzi jioni, 21 Oktoba 2025 anakofanyia kazi, Kijiji cha Idibo Kata ya Idibo Wilaya ya Gairo Mkoa wa Morogoro. Hilda ni mwalimu wa Shule ya Msingi. Alichukuliwa mbele ya Mwenyekiti na Afisa Mtendaji wa Kijiji na mbele ya Askari Kata na watu wengine walio shuhudia.
Alichukuliwa waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi wa Ofisi ya RCO wa Mkoa wa Morogoro. Askari Kata alifanya juhudi za kuhakikisha ya kuwa Hilda anaondoka na mtoto wake mdogo wa kike mwenye umri wa miaka miwili ili awe kinga ya mama yake. Wakiwa njiani kuelekea Morogoro Mjini, wale watu walijadiliana sana na hoja ilikuwa "ana mtoto".
Baadaye waligeuza Gari na kwenda kumwacha Kituo cha Polisi Gairo. Mpaka muda huu Hilda yuko kituo cha Polisi Gairo, kuna mtu kaongea naye kupitia simu ya askari mmoja wa Gairo. Bado hajapatiwa dhamana na mtoto anaumwa (ana harisha).
Huyo mtu alimtafuta RCO wa Morogoro na kuongea naye kwa simu. Alipotaja tu hilo tukio na kuwa kuna watu waliojitambulisha ya kuwa wanatoka Ofisini kwake, alishituka na hakutaka kuongea zaidi kwa madai ya kuwa hamjui huyo anayeongea naye ni nani.
Pamoja na kuwa alijitambulusha, lakini RCO alimkatia simu mtu huyo na l kusema kama vipi afike Ofisini kwake badala ya kumpigia simu. Nia ya mtu huyo kumwomba ushirikiano RCIO ili Hilda apatiwe dhamana haijafanikiwa.
Imeelezwa kuwa Hilda anatuhumiwa kwa kosa la "Uchochezi Mitandaoni" kwa kupitia posti yake ya tarehe 5 Oktoba 2025, Siku ya Walimu Duniani alipoandika, kuhusu Kikokotoo. Lakini sentesi wanayoiita ni Uchochezi ni iliyosema; "Sisi Walimu ni Daraja na ndiyo tunaowavusha hata hao wanasiasa".
Watu waliomchukua jumla yao walikuwa ni 6. mmoja alikuwa mwanamke na kiongozi wao anaitwa Manyama ambaye ni mrefu mweusi na anahisiwa kuwa ni mtu wa Kanda ya Ziwa (Msukuma, Mkerewe, au Mkurya). Alivaa fulana ya damu ya mzee) na walitumia gari nyeupe ya aina ya LandCrueser.
Mwalimu N. H .L;
Gairo, Morogoro; 23 Oktoba 2025
Mwaka 1997 milio ya risasi kadhaa ilisikika katika mitaa ya Los Angeles huko California, mwanamuziki kutoka katika kundi la Bad Boys.
Christopher Wallace ama B.I.G ama Biggie alidondoka baada ya risasi hizo kupenya kwenye mwili wake.
Hiyo ilikuwa ni wiki moja baada ya ikulu ya Marekani kumuita Puff Daddy, Snoop Dogg na Dr. Dre.
Na kuwaambia kwamba sasa ulikuwa ni wakati wa East na West kumaliza tofauti zao na kufocus zaidi kwenye muziki.
Walikubaliana na ikulu kwamba kila kitu kingekuwa poa, lakini sasa mauaji mengine yalikuwa yamefanyika baada ya kile kifo cha Tupac mwaka 1996.
Lilikuwa pigo kubwa kwa mwanamuziki, dogo janja aliyekuwa na pesa nyingi, Puff Daddy, kipenzi chake kiliondoka, kilifutwa katika uso wa dunia na kamwe asingeweza kumuona tena.
Mke wa marehemu, Faith Evans alilia sana, Puff akaona haiwezekani, kwa kuwa kipenzi chake aliondoka duniani akaamua kumtungia wimbo maalumu ulioitwa I’ll Be Missing You.
Hiyo ilikuwa ni sample ya ngoma moja iliyopigwa na mwanamuziki aliyeitwa Sting iitwayo Every Breath I Take.
𝗠𝗔𝗖𝗛𝗜𝗠𝗕𝗢 𝗬𝗔 𝗧𝗢𝗧𝗢𝗭 𝗝𝗜𝗝𝗜𝗡𝗜 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠.
Karibu Daslamu ardhi iliyojaa kila aina ya Takataka,
Kama Mdau wa Pisi za Mtaani || Vyuoni katika jiji hili,
Basi hii ni Special Thread kwaajili yako Mkuu 🧵🧵
Endelea na Uzi ⤵️
MCH. GERALD JOHNSON ASIMULIA ALIYOYAONA KUZIMU:
UZI 🧵
🗣️ Kunatisha..!
Mwaka 2016 Mchungaji Gerald kutoka Michigan Nchini Marekani Alisumbuliwa Na Mshtuko Wa Moyo, Alikikaribia Kifo Kiasi kwamba Alijikuta Ameenda Sehemu Ambayo Hakuwahi Kwenda "KUZIMU” Gerald Johnson Anasema..