Hatimaye CCM waanza rasmi kumlilia Tundu Antipas Lissu na CHADEMA!
Leo nimepokea simu zaidi ya 20 zote za watia nia ubunge kwa tiketi ya CCM ambao majina yao yamekatwa bila sababu ya msingi katika vikao vya CCM ngazi ya wilaya.
Ujumbe wao kwa pamoja ni....
1.Viongozi wa CCM wanaokaa vikao vya mchujo wamejawa na kiburi na dharau kwa sababu wanajua CHADEMA haishiriki Uchaguzi Mkuu
2.Viongozi wa CCM ngazi za wilaya na Mkoa hawaangalii ubora wa wagombea bali mifuko ya wagombea kwa neno kwamba ukipita katika vikao vyao tayari wewe ni mbunge ni kama wanauza ubunge.
3.Kukosekana kwa CHADEMA katika uchaguzi Mkuu wa 2025 kumefanya Viongozi wa CCM wanaochuja wagombea kutojali ubora wa wagombea wanasema hata jiwe linashinda mwaka huu.
4.Wagombea wanasema nchi inaenda kubaya kama CHADEMA itaendelea kukosekana katika uchaguzi basi wananchi wasitarajie viongozi bora katika mazingira haya.
5.Wanakataa kuvitambua kama vikao vya CCM ngazi ya Wilaya na mkoa siyo vikao vya mchujo bali ni "MNADA WA UBUNGE"
6.Viongozi wa Juu wanatumia vikao vya mchujo vya CCM ngazi ya wilaya na mkoa kama njia ya kulipa visasi kwa wapinzani wao wa kisiasa waliotofautiana nao zamani.
7.Duniani hakuna utaratibu ambao wagombea wanakatwa baada ya kujaza fomu kabla ya kusikilizwa sera zao na mipango yao.
8.Fedha, vimemo na kujuana ndiyo kigezo kikubwa cha jupitisha majina matatu ya wagombea ngazi ya Wilaya na Mkoa.
9.Maelezo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Katibu Mkuu kwamba ni lazima Wabunge waliomaliza muda wao wawe katika tatu bora hayazingatiwi na inaonekana uongozi wa CCM Taifa ulitumia kauli hiyo kama njia ya kulainisha wabunge wapitishe bajeti kiulaini.
10.Hatimaye mwisho wote wanakubaliana na CHADEMA kwamba hapa tulipofika kama nchi ili tupate chaguzi za haki na Viongozi bora ndani na nje ya vyama basi "NO Reforms No Election" haiepukiki.
Boniface Jacob
WASAFI BETI LIPENI MILLIONI 25 π«΅
Hii kampuni inaleta Pyala Pyala huyu kijana wa kitanzania alipuna 30m kwenye mchezo wa Aviatrix,akatoa 5m account ikawa restricted mpaka leoπ
Amefatilia sana mpaka barua kaandika gaming board lakini bado anazungushwa
Tuwasalimie hawa π