Ukiondoa elimu, ulikosoma, taaluma ulizosomea, kazi, mahali unakofanya kazi, mali, mamlaka na cheo ulichonacho, watu uliojitambulisha nao, unabaki na nini kinachopambanua vizuri utambulisho wako na kukupa utoshelevu? Wewe ni nani ukiacha vibandiko hivi?
Ukiweza kujisikia mtu wa thamani, mtu wa maana, mwenye furaha, mwenye utulivu na amani, bila kujishikiza mno na hivi vibandiko tunavyojipachika baada ya kuzaliwa, wewe kwa hakika ni mtu ukiyekutana na wewe, unayemfahamu ‘wewe’, unayeheshimiana na wewe, unayejitambua, uliyefanikiwa na kwa hakika, utakuwa mtu mwenye utulivu unaokupa utoshelevu katika maisha.
Ukiupata utulivu huo, mshunuzi Abraham H. Maslow anakuita ‘self-actualized’ hata kama huna chochote kinachoonekana. Katika utulivu huo unakuwa mtu mwanana, asiye na mashindano, asiyejitanguliza yeye na maslahi yake, asiyeteseka kujikweza aonekane, na hivyo unakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuipa dunia kile ulichopaswa kuipa. Carl Rogers angesema hapo unakuwa unaliishi kusudi lako na hayo ndio maisha yenye utoshelevu (fully-functioning person).
Kweli, sikio la kufa halisikii dawa! Dunia nzima inakunyooshea kidole, lakini wewe umeukaza shingo na kuziba masikio. Unadhani madaraka ni ya milele? La hasha. Madaraka ni ya muda tuu (transitory power) yanapita. Lakini haki haifi, wala haizikwi. Siku yake ikifika, haki yetu tutaipata, bila shaka! A luta continua! ✊🏾
Eeh Mwenyezi Mungu tusaidie katika mapito na nyakati ngumu tunazopitia tusiyaone matatizo yetu bali tukuone wewe MUNGU na nguvu zako MUNGU uliye Mkuu!
GM 🙏🏽
Video zote nilizoangalia zinanionesha vijana maskini waliouawa kikatili na mtawala mshenzi kwa kosa la kudai haki yao.
Yes, mtawala violent anayekwapua matrilion ya fedha za umma kila kukicha kugharamia anasa zake huku umma ukiishi kwenye umaskini mzito, anayeteka, kuua, na kupakazia kesi wote wanaoonekana kukosoa ushenzi wake na kudai uwajibikaji,
Mtawala yule yule aliyethubutu kumfunga kijana mdogo jela miaka miwili na baadae kumteka na kumpoteza kabisa kwa kosa la kuchora taswira yake na kuichoma.
Mtawala yule yule aliyekopa zaidi ya trillion 40 ndani ya miaka minne tu na kumfukuza Ndugai USPIKA wa BUNGE na baadae kumuua kwa kosa la kumwambia serikali inakopa sana.
Mtawala yule yule aliyemteka na kumuua kikatili kabisa Mzee Ali Kibao; yule yule aliyemteka Mdude na kutuachia dimbwi kubwa la damu.
Mtawala yule yule aliyeamua kuzuia huduma zote za kijamii kwa Wamasai kule Ngorongoro na kuwalazimisha kuhama ili eneo lao awapatie mashoga zake wa Uarabuni.
Mtawala huyu huyu aliyewanyang’anya watoto wa watanzania maskini bima ya Afya ya TotoAfyaKadi kwa kukosa billion 30 huku akichezea trillions kuratibu igizo la uchaguzi mkuu anaoshindana na kivuli chake.
Huyu KIBAKA MKUU na VIOLENCE IN CHIEF ndio anayetuambia aliua maelfu ya vijana wetu wanaodai haki kwa sababu ni “vibaka” na “violent.”
Anatufanya kama wapumbavu tusioona na kuelewa ushenzi anaoufanya.
Anaandika Askofu Bagonza PhD.
“NGUVU” ALIFUNGA NDOA NA “HEKIMA” HUKO KENYA 2017.
Tujikumbushe:
1. Uchaguzi Mkuu ulifanyika 8/8/2017 huko Kenya. Rais Kenyatta akashinda. Odinga akakataa matokeo. Mahakama ikafuta matokeo, Uchaguzi ukarudiwa. Odinga akasusia kushiriki. Uchaguzi ukafanyika. Mahakama ikamtangaza Kenyatta kuwa mshindi.
2. Odinga akaandaa mgomo na maandamano. Majeshi yakajipanga. Kabla maandamano hayajaanza, Bw. Nguvu akamwona Bi. Hekima akamtamani na kumpenda. Akamvisha pete ya uchumba. Majeshi yakatoka mitaani, maandamano yakafanyika kwa amani.
4. Odinga akaapishwa kuwa Rais wa wananchi, Kenyatta akaapishwa kuwa Rais wa Jamhuri. Bw. Nguvu na Bi. Hekima wakawaalika Kenyatta na Odinga kwenye breakfast ili kuwapongeza. Wakakumbatiana hadharani. Kenya ikashinda, Odinga na Kenyatta wakashindwa.
5. Kila mmoja akajitukana badala ya kumtukana mwenzake. Tangu siku hiyo Kenyatta na Odinga wakawa kama kumbikumbi. Bibi mbele, Bwana nyuma au kinyume chake.
6. Mtoto mshamba huwa anadhani mama yake ndiye bingwa wa mapishi duniani. Hatembei, kwa hiyo nyumbani ndiyo dunia yake na mapishi ya mama yake ndiyo "chiboko" yao. Tujiulize:
7. Tungepoteza nini kuwaruhusu “wahuni” wanaotaka kuandamana? Tukawapisha njia yao. Wakaenda waendako. Wakapokelewa na Afisa Mtendaji wa kata. Wakasoma risala yao. Kesho yake wakarudi, wakapokelewa na kada aliyeshindwa kura za maoni. Siku ya tatu wakaja, wakapokelewa na Afisa aliyetumbuliwa kwa rushwa wakati rushwa haikutumbuliwa. Mwishowe mwenye nyumba akajitokeza.
8. Mwenye akawasikiliza, wakamsikiliza. Kwa pamoja wakaubariki wizi au kwa pamoja wakaulaani wizi. Kama ni wizi kwani yeye aliiba? Kama kuns walioiba kwa niaba, Mkuu akaahidi kuwafuatilia.
Mbona ni suala la muibiwa kura na mnufaika na wizi "kujifanya" wanamlaani mwizi na kupatana kumshughulikia kwa pamoja?!
Hiyo ndiyo ndoa kati ya nguvu na hekima. Lakini sasa?;
a. Mabomu na risasi zetu vimelipuka!
b. Ardhi imekunywa damu badala ya
maji. Familia zooote poleni😭😭
c. Polisi wanashughulika na waandamanaji badala ya kushughulika na walioiba,
d. Viongozi wa dini wanawasikiliza watuhumiwa kuliko wanavyomsikiliza Mungu
e. Walioiba hawana amani, walionufaika na wizi hawana amani, walioua hawana amani, hata wasioamini kuna wizi nao hawana amani.
f. Mtandao wetu usingefungwa na kusababisha hata walioufunga nao wakose mawasiliano.
g. Walioshinda wamezuiwa kufanya sherehe na walioshindwa wamezuiwa kufanya matanga. Waliofiwa hawana uhuru wa kuomboleza kwa sababu walitoka nje ya nchi.
h. Makanisa ambayo hayakufunga kwa COVID, yakafunga kwa Gen Z wa kigeni!
Kweli, Ukikosea njia, kila njia ni sahihi.
Bila nguvu kuoana na hekima, tutapanda bangi tutegemee kuvuna mchicha.
Atakayekubali kurudi nyuma ndiye mshindi. Nchi ina mipaka lakini magonjwa, haki, uovu, na uhalifu havina mipaka.
Mataifa yenye amani ya kudumu ni yale yanayowaogopa raia wake. Mataifa yenye mashaka ya kudumu ni yale yanayoogopwa na wananchi wake.
Internet karibu, tulikumiss kweli.
Taarifa ya Dw swahili iliyosoma na Bakari Ubena Dw Swahili wamemtaja Mtoto wa Rais Samia, Abdul Hafidhi kama Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa asiye Rasmi na Mtu aliyenyuma ya Mateso ya Mauaji ya Waandamanaji na Msuka mikakati nyuma ya Mama yake
Abdul Anatuhumiwa kuwa ndiye Msuka Mikakati ya kuwaandama waandamanaji sikiliza Video 👇
Kutoka 11:1 Bwana akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa.
"I will stand with you until Tanzania is liberated," Tanzanian activist Mange Kimambi tells citizens, just a day after the country's Attorney General threatened to request her extradition from the USA!
*Vitenguzi vya uislamu*
الأول: الشرك في عبادة الله تعالى
Kitenguzi cha Kwanza: Shirki katika ibada ya Allah Mtukufu.
قال تعالى:
﴿إن الله لا يغفر أن يشرك به ويغفر ما دون ذلك لمن يشاء﴾ (النساء: ٤٨)
“Hakika Allah hasamehi kushirikishwa, na husamehe yasiyokuwa hayo (ya shirki) kwa amtakaye.”
📚 (Surat An-Nisa’: 48)
وقال تعالى:
﴿إنه من يشرك بالله فقد حرّم الله عليه الجنة ومأواه النار وما للظالمين من أنصار﴾ (المائدة: ٧٢)
“Hakika anayemshirikisha Allah, basi Allah amemharimishia Pepo, na makao yake yatakuwa Motoni; wala madhalimu hawatakuwa na wa kuwanusuru.”
📚 (Surat Al-Ma’idah: 72)
ومنـه الذبح لغير الله كمن يذبح للجن أو للقبر
Na miongoni mwa shirki hiyo ni kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allah, kama anayechinja kwa ajili ya majini au kwa ajili ya kaburi.
➡️ Hii ni kufundisha kwamba kuabudu asiyekuwa Allah, kuomba msaada kwa asiyekuwa Allah, kuomba ulinzi kwa asiyekuwa Allah, kuomba uokovu kwa asiyekuwa Allah, kuchinja kwa ajili ya kiumbe mwingine yeyote kinyume na Allah — iwe ni kwa ajili ya majini, mizimu, au walioko makaburini — ni aina ya shirki kubwa (shirk akbar), inayomtoa mtu katika Uislamu kama akifanya kwa nia ya ibada.
Kwa sababu ibada ya kuchinja na zinginezo ni maalum kwa Allah peke yake.
Mama zetu enzi hizo wakisikia unalia huko nje, walikuita na kutaka kujua nini kimekusibu. Kwikwi sana lakini unajua nafasi ndio hii ya kucheua maumivu. Unalalamika. Unasemea wenzako. Unashitaki. Mama mwema angesema, “Pole” na kukunyooshea kiganja chake, “Tema puu nikamchape.” Kesi inaishi hapo.
Wazazi wetu hawakusoma mambo ya ‘empathy’ lakini walielewa mama ndiye mtu wa kwanza kuonesha utu kwa mwanae anayepitia misukosuko ya kihisia. Mama alikujua anawajibika kuelewa malalamiko ya mtoto, kuonesha anamhurumia na ndiye mfariji wake nyakazi za maumivu.
Kesho yake ilikuwa ukichokozwa huko michezoni, ukatokea mtafaruku, ulijua ukikimbilia kwa mama atakuelewa. Imani uliyonayo kwa mama iliondoa haja ya kugombana na wenzako. Tulikimbilia kwa mama zetu.
Tuliogopa sana vile vijamaa vilivyolelewa na mama asiyejua kusema hata pole. Hawa walikuwa wakikimbilia kwa mama zao waligeuziwa kibao, “Unapigwa? Wewe ulikuwa wapi? Hebu niondokee hapa!” Hawa jamaa walikuwa wakatili sana kwenye michezo. Ukipishana naye kidogo anamalizana na wewe pale pale maana anajua kukushitaki kwa mama yake ni kupoteza muda.
Hatari sana kuwa mzazi usiye na uwezo wa kumfundisha mwanao utu kwa vitendo lakini anajua kumbebesha lawama kwa kuamua kushughulikia matatizo yake mwenyewe. Utu tunajifunza kwa wazazi wanaojali hisia zetu. Utu tunajifunza kwa wazazi wanaosikiliza maumivu yetu.