โEntrepreneur. Political enthusiast. Love to read books๐. Footballโฝ๏ธ& basketball ๐ fun. Am Christian. A husband, father, brother, uncle, friend & neighbourโฆ,
Habari ndg zangu wana twita(X). Naitwa SIMON MWACHA nafanya marketing โMILLENNIAL CARGOโ Tunasafirisha mizigo kutoka China ๐จ๐ณ kuja Tanzania ๐น๐ฟ kwa njia ya maji. Siku 38 mzigo upo Godown. Ofisi zetu zipo LUMUMBA jengo la USHIRIKA TOWER ghorofa ya 8
Godown zetu zipo Banda la NGOZI
๐๐๐ซ๐๐ณ๐ ๐ฅ๐ ๐๐๐ฐ๐๐ณ๐ข๐ซ๐ข ๐ฅ๐ข๐ฅ๐ข๐ฅ๐จ๐ญ๐๐ง๐ ๐๐ณ๐ฐ๐ ๐ง๐ ๐๐ก. ๐๐๐ข๐ฌ ๐๐๐ฆ๐ข๐ ๐๐ฎ๐ฅ๐ฎ๐ก๐ฎ ๐๐๐ฌ๐ฌ๐๐ง
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
๐ Waziri - Mh. Ridhiwani Jakaya Kikwete
๐ฉโ๐ผ Naibu - Regina Ndege Kwarai
Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji
๐ Waziri - Prof. Kitila Mkumbo
๐ฉโ๐ผ Naibu - Pius Steven Chaya
Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana
๐ Waziri - Joel Nanauka
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
๐ Waziri - Mh. Mhandisi Hamadi Masauni
๐ฉโ๐ผ Naibu - Dkt. Festo Dugange
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu
๐ Waziri - Mh. William Lukuvu
๐ฉโ๐ผ Naibu - Ummy Nderiananga
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano
๐ Waziri - Mh. Deus Sangu
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Rahma Riadh Kisuo
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
๐ Waziri - Mh. Prof. Riziki Sailas Shemdoe
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Reuben Nhamanilo (Elimu)
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Dr. Jaffar Rajab Seif (Afya)
Wizara ya Fedha
๐ Waziri - Mh. Balozi Khamis Musa Omar
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Laurent Deogratius Luswetula
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Mshamu Ally Munde
Wizara ya Mambo ya Nje
๐ Waziri - Mahmood Thabit Kombo
๐ฉโ๐ผ Naibu - Dkt. Ngwaru Jumanne Magembe
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. James Kinyasi Millya
Wizara ya Mambo ya Ndani
๐ Waziri - Boniface Simbachawene
๐ฉโ๐ผ Naibu - Denis Lazaro Londo
Wizara ya Kilimo
๐ Waziri - Daniel Chongolo
๐ฉโ๐ผ Naibu Waziri - Mh. David Silinde
Wizara ya Maji
๐ Waziri - Mh Juma Aweso
๐ฉโ๐ผ Naibu Waziri - Mh. Kundo Andrew Mathew
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
๐ Waziri - Mh. Raymond Simon Nyansao
Wizara ya Ujenzi
๐ Waziri - Abdallah Ulega
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Godfrey Msonge
Wizara ya Uchukuzi
๐ Waziri - Prof Makame Mbarawa
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. David Mwakiposa
Wizara ya Viwanda na Biashara
๐ Waziri - Mh. Judith Salvio Kapinga
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Patrobas Katambi
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
๐ Waziri - Mh. Angela Kairuki
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Sweetbert Zakaria Mkama
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
๐ Waziri - Dorothy Gwajima
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Marry Mahundi
Wizara ya Afya
๐ Waziri - Mohammed Mchengerwa
๐ฉโ๐ผ Naibu - Dkt. Florance George Samizi
Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia
๐ Waziri - Prof. Adolf Mkenda
๐ฉโ๐ผ Naibu - Wanu Hafidh Ameir
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
๐ Waziri - Dkt. Leonard Akwilapo
๐ฉโ๐ผ Naibu - Kasper Kasper Muya
Wizara ya Mali Asili na Utalii
๐ Waziri - Mh. Asha Kijaji
๐ฉโ๐ผ Naibu - Hamad Hassan Chade
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
๐ Waziri - Prof. Palamagamba Kabudi
๐ฉโ๐ผ Naibu - Hamisi Mwinjuma
๐ฉโ๐ผ Naibu - Paul Makonda
Wizara ya Mifugo na Uvuvi
๐ Waziri - Dkt. Bashiru Ally Kakurwa
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Ngwasi Damas Kamani
Wizara ya Madini
๐ Waziri - Anthony Peter Mavunde
๐ฉโ๐ผ Naibu - Mh. Dkt. Steven Lemomo Kiruswa
Wizara ya Nishati
๐ Waziri - Mh. Deogratius Ndejembi
๐ฉโ๐ผ Naibu - Salome Makamba
Wizara ya Katiba na Sheria
๐ Waziri - Mh. Juma Homera
๐ฉโ๐ผ Naibu - Zainab Athuman Katimba
CCM NI NYUMBA YA MAFISADI.
CCM waliendesha harambee maalumu kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kampeni za chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2025
Harambee hiyo ilizinduliwa Agosti 12, 2025 jijini Dar es Salaam na dhamira ya CCM ilikuwa ni kupata kiasi cha Sh. bilioni 100. Walikusanya kiasi cha Sh. Bilioni 86
CCM walipoulizwa kwamba wataweza vipi kudhibiti fedha chafu wakati wa harambee hiyo โ walijibu kwamba CCM sio taasisi ya kudhibiti fedha haramu
CCM walimualika Sigh Seth katika hafla ya harambee hiyo ya kutafuta kiasi cha Sh. 100 bilioni kwa ajili ya kampeni za uchaguzi 2025. Nimekumbuka ESCROW.
Nitaandika kwa kifupi ili wengine wengi ambao hawajui kuhusu sakata la ESCROW waelewe. Ufisadi uliotikisa Bunge mwaka 2014 kuelekea uchaguzi mkuu 2015
Harbinder Sigh Seth alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ilianzishwa mwaka 1995 ikiwa na wanahisa wawili.
Kampuni ya Mechmar Corporation (Malaysia) Berhard ikiwa na hisa 7 sawa na (70%) na kampuni ya VIP Engineering & Marketing hisa 3 ambazo ni (30%).
Mechmar Corporation (Malaysia) Berhard walikana kutambua mchakato wa ununuzi wa hisa za kampuni hiyo ikidai mchakato huo wa ununuzi haukuwa halali.
Kwamba, mchakato ulikiuka mkataba wa makubaliano wa wanahisa, ulifanyika bila ridhaa ya Bodi ya Wakurugenzi kama ilivyokuwa katika mkataba huo.
VIP Engineering walikwenda mahakamani wakitaka IPTL ifutwe iwe (wind up the affairs of (a business) by ascertaining liabilities and apportioning assets.
VIP Engineering & Marketing waliondoa shauri mahakamani baada ya makubaliano na Pan African Power Solutions (PAP) ya PAP kununua IPTLโฆ
Mali zote ni pamoja na akaunti ya TEGETA ESCROW na pesa zote zilizokuwepo ndani ambazo zilikuwa zikiwekwa na TANESCO malipo gharama ya uwekezaji.
Pesa hizo ziliwekwa kusubiri kutatuliwa kwa mgogoro baina yake na IPTL. Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania ulitolewa kupitia Jaji Dkt. John Utamwa
Jaji John Utamwa aliamuru hisa za VIP kuhamishiwa kwa kampuni ya PAP na masuala yote ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kuwa chini ya PAP
Kwa nyaraka ambazo ziliwasilishwa TRA, Harbinder Sigh Seth na myoto wake wanamiliki 50% ya hisa za PAP na 50% nyingine zinamilikiwa na SIMBA TRUST.
Baada ya PAP kumilikishwa IPTL ilichukua fedha zote zilizokuwa ndani ya akaunti ya ESCROW kiasi cha Sh309,461,300,158.27 na US$22,198,544.60
PAP wakatumia amri hiyo ya Mahakama kujisajili Business Registrations and Licensing Agency (BRELA). Wakagawa hisa za ziada kwa makampuni mawili.
Kampuni mbili zilizopewa hisa hizo ni; Kampuni ya Hi-Tide Trade (hisa 1) ambayo ni asilimia 10. EURASIA Holdings Limited (hisa 1) ambayo ni asilimia 10.
Kuanzia hapo, Harbinder Sigh Seth (maarufu SingaSinga) akawa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL)โฆ
Wakurugenzi Watendaji wenza wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) walikuwa ni; Manraj Singh Bharya na Magesh Varan Subramanyan
PAP hawakuwahi kununua hisa 7 (70%) walizokuwa wanazimiliki katika IPTL. Harbinder Sigh Seth anadai kununua 79% kupitia Piperlink ya British Virgin Island
Standard Chartered Bank inaeleza ndiyo wamiliki wa hizo hisa 7. Pia warithi wa hisa za Mechmar katika IPTL kutokana na biashara ya ukopeshaji huko Malaysia..
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alisema hayakuwepo manunuzi. PAC pia katika uchunguzi wake walisema hayakuwepo hayo manunuzi.
PAP walifanya utapeli kununua hisa ambazo haikuwa inazimiliki. Mahakama Kuu ya Tanzania ikaingizwa mkenge katika utapeli huo na kubariki Biashara hiyo.
Makubaliano kati ya Serikali na IPTL kuanzisha mradi wa kufua umeme kuzalisha MW 100 yalifikiwa kukabiliana na tatizo la uhaba wa umeme miaka ya 1990.
Serikali ilialika sekta binafsi kuwekeza katika uzalishaji umeme kwa vile haikuwa na fedha za kugharimia miradi ya umeme. VIP Engineering & Marketing wakaingia.
Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd ya Tanzania (VIP) ilishawishi Serikali kualika Kampuni ya Mechmar Corporation ya Malasyia (MECHMAR).
Baada ya Mechmar Corporation (Malaysia) kuonesha kuwa inaweza kuzalisha MW 100 katika Jiji la Dar es Salaam, ilisaini makubaliano (MoU) na Serikali.
1994 MECHMAR na VIP kwa pamoja zilianzisha Kampuni ya IPTL, kama kampuni binafsi iliyokuwa inamilikiwa na MECHMAR kwa asilimia 70 na VIP kwa asilimia 30.
IPTL ilipewa leseni ya kujenga-kumiliki na-kuendesha (Build-Own-Operate) mtambo wa kuzalisha MW 100 za umeme wa mafuta mazito Tegeta-Salasala.
Waziri Sospeter Muhongo anasema; โMkataba wa kununua umeme kati ya TANESCO na IPTL (Power Purchase Agreement-PPA) ulisainiwa Mei 26, 1995.
Mkataba ulikuwa wa miaka 20, ingawa utekelezaji wake ulianza 2002. Katika mkataba wa PPA, TANESCO ndiye mnunuzi pekee wa umeme kutoka mtambo wa IPTL.
Independent Power Tanzania Limited (IPTL) walitakiwa kuiuzia TANESCO umeme usiopungua 85% ya umeme unaozalishwa kila siku, pamoja na mkataba huo,
Serikali ilisaini mikataba miwili ambayo ni Mkataba wa Utekelezaji (Implementation Agreement) na Mkataba wa Dhamana (Guarantee Agreement),
ilikusudiwa kuwa endapo TANESCO itashindwa kulipa gharama za kununua umeme, Serikali ichukue dhamana ya kulipa gharama hizo kwa niaba ya TANESCO.
CAG katika ripoti yake anaeleza Harbinder Sigh Seth anaidai TANESCO sh211 bilioni. TANESCO walipohojiwa wakaeleza wao ndiyo wanamdai Harbinder Sigh Seth.
CAG anasema September 2013 Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Werema alimuagiza Mwanasheria wa TANESCO, Godwin Ngwilimi kwenda Malaysia
Godwin Ngwilimi baadae alilazimika kujiuzulu, aliagizwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba pesa zilizopo katika akaunti ya ESCROW zilipwe PAP.
PAP walitakiwa kulipa kodi kwa TRA, lakini Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Werema aliagiza PAP wasilipe kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hajapewa mamlaka ya kutoa na kusamehe kodi. Hili ni jukumu ambalo limeachwa kisheria kwa Waziri wa fedha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, aliruhusu fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW kulipwa PAP bila kuwepo kwa uhalali wowote.
Matokeo yake, TANESCO ikapata hasara ya Jumla ya kiasi cha Sh306 bilioni kutokana na gharama ya tozo kutoka IPTL kati ya mwaka 2002 na mwaka 2012.
Kwamba, katika makubaliano kati ya Harbinder Sigh Seth na DPP, anatakiwa kurudisha fedha za ESCROW US$148 milioni. Hata akilipwa, atabakia anadaiwa.
Makubaliano ya Harbinder Sigh Seth na DPP yamesajiliwa Mahakamani akitakiwa kurejesha Jumla kiasi cha Sh. Bilioni 26.9. Alilipa Sh200 Milioni.
Novemba 29, 2014 Bunge, spika wa Bunge akiwa Anne Makinda liliketi hadi saa 4:30 usiku na kutoa maazimio nane kuhusu sakata hilo la ufisadi wa ESCROW.
Bunge liliazimia Harbinder Singh Seth achukuliwe hatua kali za kisheria na TAKUKURU na Jeshi la Polisi kwa kuhusika na vitendo vya kijinai katika ESCROW.
Bunge liliazimia Serikali ifanye utaratibu wa kuchukua mitambo ya kufua umeme wa IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.
Bunge liliazimia, Serikali itekeleze Azimio kabla ya kumalizika Bunge la Bajeti 2015/16, Serikali iwasilishe Taarifa ya Utekelezaji wa Mikataba ya Umeme;
Bunge liliazimia Serikali iwasilishe muswada wa Marekebisho ya Sheria iliyounda TAKUKURU, ili kudhibiti rushwa kubwa, ufisadi na uhujumu uchumi
Bunge liliazimia, Rais, aunde Tume ya Kijaji, kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa
Bunge liliazimia mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi kuitaja Stanbic Bank Tanzania Ltd kujihusisha na utakatishaji wa fedha za ESCROW.
Bunge liliazimia Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, KM Wizara ya Nishati na Madini na
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wawajibishwe na kuishauri mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao haraka.
Bunge liliazimia William Ngeleja, Victor Mwambalaswa na Andrew Chenge wavuliwe nyadhifa zao na wachukuliwe hatua za kisheria haraka iwezekanavyo
January 14, 2015 CCM walitoa taarifa kwa umma kuhusu sakata la ESCROW baada ya kamati kuu kuketi na kuazimia maazimio ya Bunge yatekelezwe
Rais wa wakati huo (Jakaya Mrisho Kikwete) kuhusu sakata hilo (siku anaongea na wazee wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee alisema;
Kikwete alisema; Pesa zilizokuwa ndani ya akaunti ya ESCROW siyo pesa za umma ni za IPTL kutokana na madeni IPTL inaidai TANESCO, tozo za uwekezaji.
Kikwete alisema; kama TANESCO wangeshinda kesi ya mgogoro na IPTL pesa hizo zingekuwa mali ya UMMA kama ilivyokuwa katika kesi ya mwaka 2001..
Kikwete alisema PAP walipelekewa deni la kodi ya serikali, CAG alikagua, pesa kwenye akaunti ya ESCROW hazikuwa na sifa za kuitwa pesa za umma
Kikwete akatengua uteuzi wa Profesa Anna Tibaijuka, kwa kukubali kuwekewa pesa kwenye akaunti yake binafsi huku akiwa ni mtumishi wa umma...
Kikwete akamsamehe Prof Sospeter Muhongo (licha ya kuatajwa na kamati ya PAC) akisema uchunguzi wake bado haukakamilika, akipata majibu atatoa maamuzi.
Kikwete alikanusha kufungwa kwa akaunti ESCROW hakukuwa na msukumo kutoka kwa maafisa wa serikali, alisema serikali ilifanya juhudi kwenye sakata hilo..
Kikwete akasema, mwanasheria mkuu (Francis Werema) alimwambia hakukuwa na makosa yeyote kwenye maamuzi ya mahakama kuu ya Tanzania.
Kikwete akasema hakuna hasara serikali imepata kutokana na ECSROW kwa sababu pesa hizo zilikuwa ni deni ambalo TANESCO ilikuwa inadaiwa na IPTL.
Kikwete akasema, Rugemalira alilipa kodi aliyokuwa anadaiwa TZS 38 Bilioni, kwa namna hiyo, RUGEMALIRA hana makosa kwenye hili, alilipa kodi zote.
Kikwete akasema fedha zilizochotwa Tegeta ESCROW hazikuwa zinafikia Sh306 bilioni, bali ni Sh202 bilioni na zilikuwa mali ya kampuni ya kufua Umeme ya IPTL.
Kikwete akasema, wabunge wa CCM na chama hicho kwa ujumla wake, kilikuwa imara kwenye sakata hilo la ESCROW.., na hakijayumbishwa kamwe!
Gazeti la Mwananchi la 21-06-2014 lilitaja baadhi ya wanufaika wa pesa za umma kitoka katika akaunti ya TEGETA-ESCROW kupitia benki ya Mkombozi.
Kyabukoba & Assoc 1.6 bilioni; John Chenge 1.6 bilioni; Anna Tibaijuka 1.6 bilioni; Eudes Ruhangisa 404.2 milioni; Rugozobwa Theophill 323.4 milioni;
Enos Bukuku 161.7 milioni; Placidus Luoga 121. 2 milioni; Emmanuel Ole Naiko 40.4 milioni; Aloyce Mujulizi 40.4; Paul Kimiti 40.4 milioni;
Rweyongeza Bitungwa 40.2 milioni; William Ngeleja 40.2 milioni; Daniel Yona 40.2 milioni; Philip Saliboko 40.2 milioni. Waliochukua Stanbik Bank hawakujulikana
Pia, SIMBA TRUST (kampuni iliyosajiliwa Australia) walichukua nusu ya pesa za TEGETA-ESCROW. Hadi sasa hawajawahi kujulikana kwa sura au majina.
Harbinder Sigh Seth ameishi gerezani kwa siku 1,458. Hiyo ni kama miaka minne (4) ya kuishi mahabusu ya gereza. Alikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi Na. 17 ya mwaka 2017 alikuwa akishtakiwa pamoja na wenzake wawili na walikuwa wakikabiliwa na jumla ya mashtaka 12.
Mashtaka hayo yalitokana na kashfa ya kuchota zaidi ya shilingi 306 bilioni kutoka katika akaunti ya TEGETA ESCROW iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania.
Mashtaka aliyopewa ni kula njama; kujihusisha na mtandao wa uhalifu; kughushi; kutoa nyaraka za kughushi; kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu..
Kutakatisha fedha; kuisababishia Serikali hasara ya dola za kimarekani 22,198,544.60 na Sh309,461,300,158.27, alihukumiwa kulipa fidia ya Sh26.9 bilioniโฆ
Harbinder Sigh Seth na wenzake waliunda mtandao wa uhalifu na kughushi fomu Na. 14 ya usajili wa kampuni kuonesha kuwa ni Mtanzania anayeishi Dar es Salaam.
Harbinder Sigh Seth katika fomu hiyo alionyesha ni mkazi wa Mtaa wa Mrikau, Kitalu Na. 887, Masaki, Dar es Salaam. Uongo huo aliufanya Oktoba 10, 2011.
Harbinder Sigh Seth alitoa nyaraka ya kughushi ambayo ni fomu Na. 14A ya usajili wa kampuni kwa ofisa msajili wa kampuni, Seka Kasera, kuonyesha ni Mtanzania.
Kwa ulaghai huo, alijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) US$22,198,544.60 na Sh309,461,158.27 kati ya Novemba 28 na 29 mwaka 2011 na Januari 23, 2014.
Ulaghai huo waliufanya wakiwa katika Makao Makuu ya Stanbic Bank mtaa wa Ohio, Kinondoni, Dar es Salaam na Benki ya Mkombozi katika Tawi la St. Joseph.
Harbinder Sigh Seth (singasinga) alitiwa mabroni akiwa Julius Nyerere International Airport (JNIA) akijiandaa kusafiri kwenda nje ya nchi akiwa na mke wake.
Harbinder Sigh Seth alipandishwa kizimbani Juni 19, 2017. Katika makosa yake alituhumiwa kuitia Serikali hasara ya Jumla ya Shilingi 358 bilioni..
Harbinder Singh Seth (singasinga) aliachiwa huru Juni 16, 2021 baada ya kulipa Tsh. 200 Milioni akiwa ameishi gerezani siku 1,458. Hiyo ni kama miaka minne.
Katika makubaliano kati ya Harbinder Sigh Seth na DPP, Harbinder Sigh Seth alikiri makosa yake na kukubali kulipa faini ya Sh200 milioni na fidia ya Sh26.9 bilioni.
Kiasi cha Sh200 milioni alilipa. Kiasi cha Sh26.9 bilioni alitakiwa kuzilipa kwa utaratibu maalum uliowekwa baada ya kuweka dhamana mitambo ya IPTL.
Pesa zilizobaki atalipa kwa awamu kwa makubaliano maalum baina yake na (DPP) ambapo alitakiwa kulipa kwa kipindi cha miezi 12 (mwaka mmoja).
Mwaka 2021, Mahakama ya Rufani ilitengua maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyofanywa na Jaji Dr. John Utamwa yaliyompa Harbinder Sigh Seth kumiliki IPTL
Maamuzi yaliyompa mamlaka Harbinder Sigh Seth kuchota US$22.19 Milioni zilizokuwa Benki Kuu (BoT). PAP wakaondolewa kuwa wamiliki wa IPTLโฆ
Uamuzi ulitolewa na Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani; kiongozi wa Jopo, Jaji Augustine Mwarija, Jaji Dkt. Gerald Ndika, Jaji Mary Levira.
Hii ni kufuatia maombi ya mapitio yaliyofunguliww na kampuni ya Mechmar Corporation (Malaysia) dhidi ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji John Utamwa.
MECHMAR ilikuwa inapinga uamuzi wa Mahakama na amri zake wa September 05, 2013 ambapo Mahakama ilikabidhi masuala yote ya IPTL mikononi kwa PAP
Kutokana na mgogoro katibya TANESCO na IPTL Mahakama ya migogoro ya kimataifa (ICSID) iliamuru Serikali kulipa US$185.4 milioni (TZS 426 bilioni)
Malipo hayo ni kutokana na kukiuka mkataba. Makubaliano hayo, IPTL ilitakiwa kuzalisha 100MW katika mitambo yake Tegeta, Dar es Salaam na kuuza TANESCO.
IPTL ilikopa fedha kutoka taasisi tofauti za kifedha zikiwepo benki kutoka Malaysia kwa ahadi ya kurejesha kutokana na mapato itakayolipwa na TANESCO.
Baada ya muda madeni yote ya IPTL yalinunuliwa na benki ya Standard Chartered tawi la Hong Kong. Benki inanunua deni kama mteja anataka kukopa tena.
Makubaliano hayo kati ya Standard Chartered na IPTL TANESCO Ilipotaka kutoa dhamana ya mkopo endapo itashindwa kulipwa Serikali ichukue jukumu hilo
Makubaliano hayo yaliafiki kufunguliwa kwa akaunti ya ESCROW Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambako TANESCO ingelikuwa inapeleka marejeshi ya mkopo.
Akaunti ya TEGETA ESCROW ilifunguliwa Benki Kuu (BoT) kuweka fedha za tozo ya uwekezaji, ili pande mbili kushughulikia tofauti zao (TANESCO na IPTL).
Akaunti ya ESCROW ilifunguliwa Benki Kuu (BoT) baada ya mkataba wa ESCROW kusainiwa na Serikali (kwa niaba ya TANESCO), IPTL na BoT, Julai 5, 2006.
Kufunguliwa kwa akaunti ya ESCROW kulitokana na ushauri wa Mkono and Co. Advocates in association with Denton Wilde Sapte. Ushauri wa Juni 30, 2004.
Mkataba wa ESCROW ulitokana na Mkataba wa Ununuzi wa Umeme kati ya TANESCO na Independent Power Tanzania Limited (IPTL) uliosainiwa Mei 26, 1995.
Endapo pande mbili za mkataba hazikubaliani na gharama za umeme, fedha zilipwe kwenye akaunti ya ESCROW hadi mgogoro wa malipo utakapotatuliwa.
Fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya ESCROW zilikuwa zinalipwa na TANESCO kutokana na mgogoro wa gharama za malipo kati ya TANESCO na IPTL.
TANESCO ilikuwa inalipa gharama za juu kutokana na IPTL kutumia mkopo kama mtaji, kukokotoa gharama za umeme wakati mtaji wa IPTL si zaidi ya US$1,000.
Akaunti ya TEGETA ESCROW ilifunguliwa Julai 05, 2006 na kufungwa rasmi September 05, 2013 na kuamriwa shughuli zote za TANESCO zikabidhiwe IPTL...
Miaka nane (8) baadae Mahakama ya Rufani Tanzania imeridhika kwamba uamuzi huo wa Mahakama Kuu kuikabidhi IPTL kwa PAP haukuwa sahihi.
DPP alisema hauwezi kuathiri makubaliano ya Seth na Serikali. Masharti ya kuachiwa huru ni kulipa fidia na akishindwa ndani ya miezi 12 watamrudishia mashtaka
Ipo GN inayowaalika wadau wote ambao wanahusika na IPTL kwenda Mahakamani kama wanalo jambo lolote kuhusiana na mchakato wa kufutwa kwa IPTL.
Hili ni tangazo la Serikali (GN) limetolewa April 25, 2025; Lakini Harbinder Sigh Seth amebadilisha wanahisa wa kampuni ya IPTL nyaraka za BRELA.
Harbinder Sigh Seth ameshindwa kuheshimu amri ya Mahakama ya Rufani. Ameshindwa kutekeleza makubaliano yake na DPP. Nani yupo nyuma yake?
Hakuna sehemu yoyote ambayo Harbinder Sigh Seth amekwenda na kutengua amri ya Mahakama au kubatilisha makubaliano yake na DPP (Plea Bargain).
Tuliwahi kujiuliza, Harbinder Sigh Seth anapata nguvu hizo wapi wakati Mwaka 2021, Mahakama ya Rufani ilitengua maamuzi yaliyompa umiliki wa IPTL..
Lakini katika usajili wa kampuni BRELA kuna kampuni mpya ambayo ndiyo mmiliki mpya wa IPTL inaitwa KARENGA HEWITT PTY LTD imesajiliwa Australia.
Hii kampuni ni mali ya Harbinder Sigh Seth na binti yake. Umejiuliza BRELA wamekubali vipi kufanya hayo mabadiliko wakati kuna amri ya Mahakama ya Rufani?
Bahati mbaya, watawala waliotakiwa kumuona SINGASINGA kama mhalifu, wao wamemkaribisha kukusanya pesa za kampeni za uchaguzi 2025.
CCM imeshindwa kulinda mali za umma na sasa bila aibu imeamua kuwaalika watu wenye harufu na hatia ya kufanya ufisadi katika shughuli zao za kukusanya pesa.
Kwa lugha rahisi zaidi; CCM imechangiwa na Harbinder Sigh Seth ambaye ana hatia ya Mahakama ya kutwaa kitapeli hisa 70% za kampuni ya kufua Umeme ya IPTL
Na kuchota zaidi ya TZS 306 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT) na kuhukumiwa kulipa fidia ya TZS 26 Bilioni kwa kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa udanganyifu
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Mikataba ya MANGUNGO katika jina la UWEKEZAJI
1.Waarabu wa familia ya kifalme Dubai, (DP WORLD) wamepewa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kwa mikataba ya kiduanzi unaotajwa miaka thelathini
2.Waarabu wa familia ya kifalme ya Dubai (Blue Carbon LLC) wamepewa kusimamia na kuhifadhi misitu ya Tanzania. Hii ni hekta milioni 8.1 (8% ya ardhi yote)
3.Watu kutoka Russia, (ROSATOM) wamepewa ardhi yenye tani milioni 139 wachimbe madini nadra ya kimkakati ya uranium huko Namtumbo, Ruvuma.
4.Watu wa Australia (URANEX) wamepewa ardhi nzuri wachimbe madini nadra ya kimkakati na graphite Mkoa wa Lindi. Kampuni zao tatu zitauza madini nje
5.Watu wa Canada (BARRICK GOLD) wanaondoka na dhahabu. Hawajajenga hata smelters moja. Wanaacha mashimo na watu wetu kupigwa risasi nyingi.
6.Waarabu familia ya kifalme Dubai (OBC) wameongezewa ardhi 1,500kmยฒ kutoka 4,000kmยฒ zilizokuwa kwa Maasai wao wamebaki na 2,500kmยฒ
7.Watu kutoka Netherlands (SHELL) na Norway (EQUINOR) wamepewa kuchimba gesi asilia katika bahari kuu kusini, eneo la Likongโo, Lindi, Tanzania
8.Waarabu wa Dubai, Emirates National Group (ENG) wamepewa kuendesha huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART), Jiji la Dar es Salaam.
9.Watu wa France, Maurel & Prom, wanazalisha gesi asilia, 641 billion cubic feet, Mnazi Bay, Mtwara, ambayo ni 48% ya pato la gesi asilia Tanzania kwa sasa.
10.Kandarasi ujenzi Bwawa la Nyerere (JNHPP) alipewa Egypt. Kandarasi ya ujenzi wa SGR alipewa China na Turkey. Waswahili mtapewa Kanda Bongoman.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
1.Wafuasi na wanachama wa CHADEMA hatusambazi kazi za chama mitandaoni kwa kiwango cha kutosha. Tumejazana Facebook, Twitter, Instagram, TikTok na kwingine huko, lakini hatubebi kazi za chama.
2.Wafuasi na wanachama wa CHADEMA hatutembelei ipasavyo akaunti rasmi za chama katika mitandao ya kijamii. Mfano Twitter na Instagram, akaunti ya chama inazidiwa nguvu na akaunti za watu binafsi.
3.Wafuasi wa mbogamboga na vyama shikizi wanavamia kurasa za CHADEMA kutoa matusi na kejeli, tusiwaache, twendeni tukaweke kambi katika kurasa hizo, tusimame kutetea chama chetu dhidi ya Interahamwe..
4.Tumejazana makundi ya WhatsApp lakini hatushambulii. Ni watchdogs tu. Tunasoma na kupiga kimya hata tukiona mwenzetu ameshambuliwa na tunatakiwa kujibu kwa nguvu. Hatufanyi hivyo.
5.Tuwekeze katika matumizi ya mitandao. Sera za chama tunatakiwa kuzipata kupitia mitandao ya kijamii, na ukizipata, usipige kimya, sambaza, ukiweza hodhi mjadala, wajumbe wajadili sera za CHADEMA.
6.Tuwaogopeshe MaCCM kwa kutinga sare zetu, na kutupia mitandaoni kwa kasi, na ikiwezekana, kurasa rasmi za CHADEMA zichague picha kali, na kuโpost katika kurasa hizo. Hii ni njia ya kuishi karibu na UMMA
7.Admins wa kurasa za CHADEMA, wahakikishe kurasa hazilali, contents hazipungui. Wasisubiri hadi matukio, wanaweza kuanzisha hata mijadala, au wakaweka polls pale, watu wapige kura zao, au kumbukumbu.
8.Wafuasi na wanachama wa CHADEMA, twendeni tukaโ follow kurasa rasmi za CHADEMA katika mitandao yote ya kijamii. Tuhamasishane wote, iwepo kampeni ya kuโ follow kurasa hizo kwa nguvu ya pamoja..
9.Tusisambaze porojo za MaCCM kuliko ambavyo tunastahili kusambaza vipeperushi vyetu vinavyoishughulikia serikali yao. Watu wetu wanapiga spana, tuchukue content zao, tusambaze.
10.Tuanze kuvaa sare za chama. Tusiogope kuvaa sare za CHADEMA. Sare ni njia kubwa ya uenezi wa chama. Ukivaa sare utashawishi na wengine wavae. Sare za CHADEMA zinavutia kuzivaa. Usiogope. Vaa sare.
TRA wanataka kukusanya kodi katika biashara za mtandaoni wakati wamefungia mtandao wa ๐, Telegram, Clubhouse.., kuingia huko ni lazima uwashe VPN.
TRA mtakuwa mnawasha (VPN) Virtual Private Network (ambalo ni kosa kisheria) kupiga doria hapa na pale ili kukagua aliyeโ post biashara yake mtandaoni?
Oktoba 13, 2023 (TCRA) ilieleza ni kosa kwa anayetumia VPN bila kibali na faini ni Sh5 milioni au kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja.
TCRA waliweka katazo hilo kwa kuzingatia kanuni ya 16(2) ya kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni ya mwaka 2020.
Wahuni waliketi chini na kuamua kutengeza kanuni kuzuia spana kutoka ๐ kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2020.
Lakini hata watengeneza maudhui mitandaoni (content creators) hamjaachwa katika rungu hili. Mnatakiwa kujisajili na kulipa kodi ya Serikali. Mjipange piaโฆ
Serikali ya CCM inataka kukusanya kodi kwa kutangaza biashara mitandaoni; Serikali imetengeneza mazingira gani kwa watumiaji? Serikali imewezesha nini?
Serikali inatoa free Wi-Fi? Wananchi wanapewa bundles? Wananchi wanatumia Serikali inawawezesha kuwepo online? Serikali inagawa vifaa vya kielektroniki?
Ni UTAPELI kutoza kodi katika kitu ambacho hujatengeneza au hutumii gharama kuendesha kama huduma. WhatsApp siyo mali ya CCM. WAPUUZI.
Lakini TRA hawajakurupuka. Ni hoja kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Neema Lugangira, aliyehoji sababu za biashara mtandaoni kutotozwa kodi.
Alihoji biashara ikifika mauzo ya Sh4 milioni TRA wanatoza kodi na biashara inapofika mauzo ya Sh100 milioni wanasajili kodi ya (VAT) na kutozwa kodi.
Mamlaka ya Mapato (TRA) ilifafanua kuwa, kila mtu anayefanya biashara ndani ya Tanzania , zikiwemo Biashara za mtandaoni anapaswa kulipa kodi.
Dkt. Faustine Ndugulile alipinga akisema โTanzania bado tupo nyuma katika biashara ya mtandao, tunahitaji kuikuza na kuilea, vijana wengi wamejiajiri hukoโ
Tanzania kuna gesi asilia, bandari, mipaka, mbuga za wanyama, maporomoko, mabonde, mito, maziwa, bahari, madini, Mlima Kilimanjaro, ardhi yenye rutuba..,
Bado (TRA) wanafikiria kukusanya kodi kwa kutangaza biashara mitandaoni? Halafu, mtawazuia vipi wakitumia WhatsApp status kutangaza biashara zao huko?
Kundi litakalo-athirika na kodi hii ni wapambe wa CCM mitandaoni. Kazi yao kubwa ni kuwapongeza na kuwasifu watawala. Hapa, wataonja sumu kwa kuilamba.
Nauza mayai, kwa bei ya jumla. Pia, nalipa kodi zote za Serikali. Katika biashara hiyo, nikitangaza katika ukurasa wangu wa Instagram, natozwa kodi nyingine?
Hapo bado hujalipa kodi ta zuio (withholding tax) 10%. Kodi jengo Sh1,000 (via LUKU). EWURA 1% (via LUKU). REA 3% (via LUKU). VAT LUKU 18%. Maji VAT 18%..,
Vilio kila kona vitasikika. Mawinga kama nawaona. Mmefikiwa wanangu. Tulipe kodi. Kuna baadhi ya maeneo nyeti, baiskeli na pikipiki bado hawajapata.
At 18, she has choices.
At 18, you have nothing.
At 25, she looks for love.
At 25, youโre chasing goals.
At 28, she slows down.
At 28, youโre just getting started.
Women are born with value.
Men have to build it.
Remember that.