🇹🇿🇺🇾 NEW:
Tanzania and Uganda lock in deal to create East Africa’s new energy powerhouse.
The two countries have signed an MoU with Vitol Bahrain to transform Tanzania’s port of Tanga from just an export terminal into a full regional energy hub.
Maendeleo ni hatua. Katika Mkoa wa Mtwara hatua hizi zinaonekana kila eneo kupitia miradi ya kimkakati iliyotekelezwa na inayotekelezwa, ambayo imeboresha maisha ya wananchi wote.
Ninawashukuru sana wananchi wa Mtwara kwani, tangu mkutano wetu wa kwanza pale Nanyumbu hadi leo tulipohitimisha kwa Mkoa huu tumeona mwitikio na ukarimu mkubwa. Huu ni uthibitisho kuwa tumefanya kazi mliyotupa kwa mafanikio makubwa, matokeo mmeyaona, na sasa mko tayari kutuongezea kazi.
Ahsanteni sana. Mwenyezi Mungu awabariki sana.
Ahsanteni sana Pemba.
Wingi wenu ni uthibitisho wa upendo na imani yenu kwangu na kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kuitumika nchi yetu. Kama mlivyosema, mlitupa kazi, tumefanya kazi, na Oktoba mnakwenda kutuongezea kazi. Ahadi yangu na ya CCM kwenu ni kuendelea kufanya kazi kwa ubora, weledi na mafaniko makubwa zaidi.
Mwenyezi Mungu awabariki sana.
Leo nimepata wasaa kutazama Dabi ya Dar es Salaam. Hongera sana Klabu ya Yanga kwa ushindi wenu dhidi ya Klabu ya Simba katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii. Ulikuwa mchezo mzuri kwa pande zote. Ushindani wenu, ndani na nje ya uwanja ni burudani ya kipekee ambayo wakati wote inatuleta Watanzania pamoja.
Njombe, ahsanteni sana kwa mapokezi makubwa, ahsanteni sana kwa mwitikio mkubwa kwenye mikutano yetu, na ahsanteni kwa ahadi ya kura nyingi ifikapo Oktoba 2025.
Baada ya kuhitimisha mikutano yangu na wananchi katika Mkoa wa Mbeya leo, niliwasili Njombe na kuzungumza na wananchi katika Uwanja wa Sabasaba. Ninawashukuru sana kwa kujitokeza kwa wingi kuzungumza nami na kwa upendo wenu usiyo kifani.
Mwenyezi Mungu awabariki sana.
Asanteni sana wananchi wa Chamwino, Chemba na Kondoa kwa mwitikio wenu mkubwa kwenye mikutano ya kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM). Wingi wenu ni mwendelezo wa uthibitisho wa imani yenu kwetu kutokana na kazi kubwa iliyofanyika, na unaeleza matarajio yenu juu yetu, pindi mtakapotupa ridhaa ya kuendelea kuwatumikia.
Katika kipindi cha miaka minne, Dodoma imenufaika kwa miradi 3,093, yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 10, ikiwa ni kiasi kikubwa zaidi kuwahi kutumika kutekeleza miradi mkoani hapa. Mbali na miradi hii kuupa mkoa huu hadhi ya Makao Makuu ya Nchi, pia imeboresha maisha ya wananchi, hasa katika sekta za afya, maji, elimu, nishati, mawasiliano, kilimo na miundombinu.
Baada ya kuzindua Kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dar es Salaam jana, leo tumeanza kampeni zetu mkoani Morogoro. Baada ya kuzungumza na wananchi Ngerengere nilielekea Morogoro Mjini. Ninawashukuru kwa mapokezi makubwa na ya heshima. Hii ni imani kubwa kwangu na kwa chama chenu, Chama cha Mapinduzi.
Nimerejea Morogoro nikikumbuka ziara yangu ya Agosti 2024, ambapo nilikagua na kuzindua kazi kubwa za maendeleo zinazoendelea kuwanufaisha wananchi. Tumepiga hatua, na tumejipanga kupiga hatua zaidi. Miongoni mwa tutakayofanya kwa miaka mitano ijayo mkoani hapa ni kujenga vituo zaidi vya kutolea huduma za afya, kufikisha umeme kwenye vitongoji vyote, kwani tumekamilisha kazi ya kupeleka umeme kwenye vijiji vyote, kujenga masoko ya kisasa, kuvutia uwekezaji wa viwanda, kukuza kilimo, utalii na kuimarisha miundombinu.
Imani ambayo mamilioni ya wananchi wamekipa Chama Cha Mapinduzi, imetuwezesha kufanya mengi yenye umuhimu kwa nchi yetu, lakini pia kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa yenye umoja, amani na utulivu. Tunarudi kuomba ridhaa na imani hiyo kuendelea kwani tumeonesha nia, utayari na uwezo wa kufanya hivyo.
Leo ni Zamu ya Wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Viunga Vyake! Kumpokea Mgombea Urais CCM- Dkt Samia Suluhu Hassan na Kusikiliza Sera bora za CCM .
#kazinaututunasongambele#oktobatunatiki
Mapema leo Ikulu, Dar es Salaam nimepokea Nishani ya Heshima ya Juu ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (The Grand Cordon). Hii ni heshima kubwa kwangu, kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Tanzania kwa ujumla.
Tuzo hii ni matokeo ya kazi tunayoendelea kuifanya katika kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kushirikiana kimataifa katika maendeleo ya michezo ya majeshi na kusimamia misingi ya amani, mshikamano, urafiki, usawa, uadilifu na ushupavu.
Nchi yetu ni mwanachama wa baraza hili tangu mwaka 1973, ambapo sasa lina jumla ya nchi 142. Majukwaa haya ya michezo ya kijeshi ni nyenzo muhimu ya kujenga mshikamano wa kijeshi unaovuka mipaka ya kijiografia na tofauti za kimila na kitamaduni, sambamba na kuchochea urafiki na kuaminiana miongoni mwa vikosi vya ulinzi na usalama.
Ninampongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda kwa kufanikisha Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) uliofanyika nchini Tanzania na kushuhudia ushiriki wa wageni mbalimbali. Nitalifanyia kazi ombi la CISM la kuandaa mashindano ya kimataifa ya michezo ya majeshi nchini Tanzania.
Ninawashukuru wanachama wenzangu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wote wa Dodoma kwa mapokezi makubwa katika ofisi za chama, baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati utakapofika, tutakuja kwa wananchi kuzungumza nanyi na kuwaeleza yale tuliyofanya na tutakayofanya kwa miaka mitano ijayo, ili kuomba ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi yetu. Wito wangu kwenu, tuendelee kudumisha amani, umoja na mshikamano ili tuhakikishe ushindi wa kishindo kwa chama chetu na kuendelea kuwatumikia vyema wananchi kama yalivyo matarajio yao.
Kazi na Utu. Tunasonga Mbele.