Chuki mnayojenga mlipuko wake utakua wa kishindo kikubwa mno..
Mlipomteka Mdude, Soka , Ben Saanane na wengine mliamini kila mtu atajificha ndani na kunyamazaโฆ
Sasa wanaongea mpaka Wazee..
Kufikiria kwamba mtachukua watu mpaka wote wawapigie magoti ni kujidanganya mno..
Kama Hitler, na madikteta wengine hawakufanikiwa kwa mbinu hii, historia inatuambia kwamba hakuna anaeweza kushinda kwa kujaza watu hofu..
Muachieni huyu kijana Nicodemus Julius Loyore.
Hakuna wa kushindana na wewe &
Huwezi kufeli kama:
1. Utaishi kwa misingi.
2. Utatimiza wajibu wako kila siku.
3. Ishinde hofu na tenda kila siku.
4. Fanya tathimini ya maendeleo yako
5. Usiogope macho ya watu. Fanya.
7. Shindana na wewe ulivyokuwa jana.
8. Acha visingizio. Chapa kazi.
9. Usilalamike. Unapoteza muda bure.
10. Wajibika kwa matendo yako.
#Jeshilam2m1
Jinsi Ambavyo Kukosekana Kwa Fedha Kunavyoweza Kuathiri Mahusiano Yenu:
Kulingana na Utafiti Uliofanywa na Taasisi ya "Instute Of Divorce and Financial Analysis"
Umethibitisha kuwa, Asimilia 20% Ya Ndoa Zinazovunjika Sababu Kubwa ni MASUALA YAHUSUYO FEDHA.
Hii ni kusema kwamba, Fedha ina uwezo wa kuathiri mahusiano na ndio maana...
Nataka ujue namna ambavyo fedha ikikosekana inavyoweza kuleta athari Hasi (Negative Effect) katika maeneo yafuatayo;
1. Kutokutimizwa Kwa Mahitaji Muhimu.
Fedha inasaidia kupata chakula, mavazi na malazi.
Inasaidia kuhusika na gharama ,a matibabu pamoja na usafiri.
Hii ni kusema kwamba, kama ikikosekana basi itakuwa ngumu kutimizwa kwa hayo yoote.
2. Kukosekana Kwa Amani na Utulivu.
Hebu wafikirie wale wenzi ambao, wapo katika mahusiano na wanapendana sana.
Lakini...hawana fedha za matibabu, hawana fedha za nauli wala hawana fedha za chakula.
Swali....Kati Yao AMANI na Utulivu Vitakuwepo?
Jibu ni "HAPANA" Kwa Sababu Kisaikolojia Amani na Utulivu ni matokeo ya KUTIMIZWA KWA MAHITAJI MUHIMU.
Na Mahitaji Hayo Ili Kutimizwa YANAHITAJI FEDHA.
Hata kama watasema "Furaha Yetu sio pesa" lakini bado ukifuatilia utaiona tu athari ya kukosekana kwa fedha katika mahusiano yao.
3. Kumpunguzia mwanaume hali ya kujiamini
Katika ubongo, kuna eneo linaitwa "Rostral Cingulate Zone"
ni eneo hili ambalo mwanaume akiwa na fedha linatoa hormone ya kumfanya ajihisi comfortable na mwenye kujiamini.
Na asipokuwa na fedha anajihisi mdhaifu (Insecure)
Hii ni kwa sababu, kwa mwanaume fedha ni ishara ya nguvu na uimara (Strength Of Manhood)
Hiyo inatosha kabisa kumkosesha comfortability, furaha na hali ya kujiamini mbele za mwanamke wake.
4. Kukosekana kwa Tool mojawapo ya malezi.
Linapokuja suala la malezi ipo tofauti kati ya malezi ya mama na malezi ya baba.
Mama anahusika katika kusimamia ila baba anakusika na Kuhudumia.
Inabidi baba ahudumie ili mama asimamie huduma na kuhakikisha zinawafikia watoto.
Hivyo..fedha inapokosekana kunakosekana kwa tool mojawapo muhimu sana ya malezi.
Watoto hawatavaa vizuri, hawatakula vizuri, hawatapatiwa huduma bora za elimu na matibabu.
Kwa sababu FEDHA HAKUNA!
5. Kukosekana kwa Namna mijawapo ya kudhihirisha upendo katikati yenu.
Msemo mmoja ambao nina uhakika nao ni ule unaosema...
"Love is not about money, but money in love is a means though which love is manifested"
Yaani, mapenzi sio fedha, lakini fedha ni njia au namna ambayo kupitia hiyo upendo huweza kudhihirika.
Kuna wakati ambao wenzi watapaswa kwenda sehemu kutumia muda wao pamoja (quality time)
Huku wakipata vinywaji na chakula kizuri (fedha zinahusika)
Kuna wakati watatamani kusafiri na kwenda kutembelea maeneo fulanifulani (fedha zinahusika)
Kuna wakati ambapo kila mmoja anatamani kumuonesha kuwa anampenda mwenzi wake kwa kumfanyia kitu fulani (fedha zinahusika)
Ndio maana, kuna watu hukata tiketi za ndege kwajili ya wenzi wao.
Wengine huwanunulia zawadi ya vito vya thamani, wengine huwanunulia magari nk.nk
Yoote hayo ni kuonesha jinsi wanavyowapenda ila namna walivyowaonesha FEDHA IMETUMIKA.
So..kukosekana kwa fedha kunaondoa namna mojawapo ambayo kupitia hiyo mnaweza...
"KUONESHANA UPENDO AMBAO KILA MMOJA ANAO KWA MWENZAKE"
Na kwa sababu hiyo...Hamtayafurahia Mausiano Yenu.
Kumbuka, Mwandishi wa Kitabu cha Love and Money "Conversation To Have Before You Get Married" Anasema
"Love Does'nt Cost a Thing, But Lack Of Money Have a Potential To Destroy Relationship"
Yaani...Upendo Hauna Gharama Yoyote, Lakini Ukosefu wa Fedha Una Uwezo Wa Kuyaathiri Mahusiano"
Hii Manake ni Kwamba UPENDO PEKEAKE HAUJITOSHELEZI.
Ndio maana, mnapaswa kuwa na mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya NAMNA GANI MTAFANIKIWA KIFEDHA.
Ili muweze kuimarisha, kuboresha, kunogesha na kudumisha Mahusiano yenu.
Anyway....Nilikuwa Nawakumbusha Tu Nyie Mnaosema "Furaha yetu sio pesa"
Its Me *Isaack Nsumba.*
Expert and Competent Teacher In Love, Relationship and Marriage.
Cc @isaack_nsumba