"Siku ya maandamano ya Oktoba 29, 2025 waandamanaji walikuja mpaka kwenye kituo changu cha mafuta na mimi nilikuwa mpaka nimeshawaambia wafanyakazi wangu kwamba wakifika tu hapa acheni na milango wazi muondoke. Walipofika tu waandamanaji likatokea kundi la watu likawaambia waandamanaji hapa hamuwezi kuchoma kwani huyu ni mwenzetu kabisa anatusemea anatupambania."
"Nilikuwa na mabasi mapya 30 yalikuwa na picha ya Mama Samia yote na sikubandua lakini hawakuchoma hata moja hata juzi nimewaeleza serikali kwamba leo mtu amefanya kazi ya udereva ameshaihusisha leseni yake mara sita, ana wake wawili na watoto 20, unabadilisha ghafla taratibu kwamba madereva leseni zikiisha muda wake lazima ukasome kwanza wiki mbili kabla ya kuihuisha halafu alipe 380,000 wakati huo dereva anaishi kwa posho. Akimaliza kusoma asubiri miezi miwili kupata leseni maana yake haendi kazini, watoto hawali. Kuna kufeli pia, unamwambia arudi nyumbani wakati huo ameendesha gari miaka yote hiyo na hajawahi kupata ajali. Mimi hili suala nitalipigia kelele mpaka mwisho."
"Sheria ni zilezile, trafiki ni walewale na barabara ni zile zile si kwamba kuna barabara za juu sasa hivi, maana yake tunatengeneza kundi lingine la kutupiga CCM. Hivi ni vitu vidogo vidogo sana kwani serikali inashindwa nini kuingia gharama ikatoa mafunzo kikanda kwamba madereva wote njooni msome bure? Kwasababu alama za barabara ni zilezile, leo mtu ni dereva unataka kumkalishs darasani ni kama watu wa degree sasa hivi umwambie nataka turenew vyeti vyenu njooni darasani kusoma, mtafaulu?- Joseph Kasheku Musukuma, Mbunge wa Bunge la Tanzania akizungumza na M/S Podcast.