Na Mwandishi Wetu, Songwe
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wameendelea kufanya mapinduzi makubwa katika kuinua ubora wa elimu nchini, hususan katika masomo ya sayansi.
Hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano maalum yaliyosainiwa kati ya pande hizo mbili, yakilenga kuboresha miundombinu ya elimu kwa kujenga na kukarabati maabara za sayansi katika shule mbalimbali za mikoa ya Songwe, Kigoma na Tabora.
Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe ni moja kati ya wilaya zilizonufaika na mapinduzi haya ambapo shule mbili zimenufaika na umaliziaji wa ujenzi wa maabara nne za Sayansi. Umaliziaji ujenzi na ukarabati wa maabara hizo unafanyika kwa ufadhili wa Serikali ya Canada, ambapo takribani shilingi milioni 132 zimetumika.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Afisa Miradi kutoka TEA, Bi Atugonza David, alisema shule zilizonufaika ni Shule ya Sekondari Itumba, iliyopokea ruzuku ya shilingi milioni 78.3 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa vyumba viwili vya maabara, na Shule ya Sekondari Bupigu, iliyopokea ruzuku ya shilingi milioni 54 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa maabara mbili za Kemia na Fizikia.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Itumba, Mwl. Didiye Paul, alieleza kuwa ufadhili huo umekuwa wa neema kubwa kwa shule yake ambayo awali haikuwa na maabara hata moja.
“Awali wanafunzi wetu walikuwa wakifanyia mazoezi ya sayansi darasani, jambo lililokuwa likipunguza ufanisi wa ujifunzaji. Kukamilika kwa maabara hizi kumetoa hamasa kubwa na idadi ya wanafunzi wanaojisajili kusoma masomo ya sayansi imeongezeka kwa asilimia 75 kutokana na mazingira kuwa rafiki na ya kuvutia,” alisema Mwl. Paul.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Bupigu, Mwl. Shuhudia Mbembela alisema, kilio cha kukosekana kwa maabara ni cha siku nyingi kwa walimu na wanafunzi shuleni hapo hivyo ufadhili walioupata umekuwa mkombozi wao.
“Hadi sasa tumeshakamilisha ukarabati wa maabara moja na nyingine ukarabati unaendelea umefikia asilimia 95,” alisema Mwl. Mbembela.
Mwl. Mbembela aliongeza kuwa kukamilika kwa maabara hizo ni kutimia kwa ndoto ya muda mrefu ya shule hiyo, kwani hapo awali wanafunzi na walimu walikuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo katika mazingira magumu na yasiyo salama.
“Sasa tunaamini ufaulu katika masomo ya sayansi utaongezeka kwa kiwango kikubwa,” alisisitiza.
Kwa ujumla, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na UNICEF inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 3 katika mikoa ya Songwe, Kigoma na Tabora. Miradi hiyo inalenga kuinua ubora wa elimu, kuboresha mazingira ya kujifunzia, na kupanua fursa za elimu bora na salama kwa kila mtoto wa Kitanzania.
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wameendelea kupanua wigo wa utekelezaji wa miradi ya kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule mbalimbali nchini. Kupitia ushirikiano huo, kiasi cha takribani shilingi bilioni 1.4 kimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa matundu ya vyoo na vyumba vya madarasa, hatua inayolenga kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira salama, rafiki na yenye kuchochea ujifunzaji.
Katika kikao kilichofanyika Novemba 19, 2025 katika Makao Makuu ya TEA jijini Dodoma, pande zote mbili zilijadili maendeleo na mpango wa utekelezaji wa mradi huo. Wawakilishi wa UNICEF wakiongozwa na Mtaalamu wa Elimu, Dkt. Ayoub Kafyulilo, walitoa shukrani kwa TEA kwa usimamizi thabiti na ushirikiano mzuri unaowezesha miradi kukamilika kwa wakati. Dkt. Ayoub alisisitiza kuwa ufanisi huo ndiyo umewezesha kuongeza miradi mipya ya ukarabati wa matundu ya vyoo na madarasa ili kunufaisha shule nyingi zaidi.
Akiutambulisha mradi Dkt. Ayoub amesema, fedha hizo takribani bilioni 1.4 zitatumika kwenye shule zaidi ya 75 katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Songwe. Ukarabati huo unatarajiwa kuongeza ubora wa mazingira ya kujifunzia, kupunguza changamoto za utoro na kuwawezesha wanafunzi kupata fursa sawa za elimu bila kujali hali ya mazingira wanayotoka.
Akizungumza kuhusu dhamira ya miradi hiyo, Afisa Elimu kutoka UNICEF, Bi. Sonia Preite, alisema malengo makuu ni kuhakikisha watoto wote wanasoma katika mazingira bora, salama na ya kujenga ari ya ufaulu. Alibainisha kuwa changamoto za miundombinu zimekuwa zikiathiri upatikanaji wa elimu bora, hivyo uwekezaji katika miundombinu ni hatua muhimu katika kuhakikisha usawa na ubora wa elimu kwa kila mtoto.
Kwa upande wa TEA, Kaimu Mkurugenzi wa Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi ya Elimu, Bw. Masozi Nyirenda aliahidi kuwa, TEA itaendelea kushirikiana kwa karibu na UNICEF ili kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa ufanisi na kukamilika kwa wakati. Alisisitiza kuwa TEA imedhamiria kuendeleza ubora na usimamizi wa miradi ili kuleta matokeo chanya kwa jamii na sekta ya elimu kwa ujumla.
Awali, TEA na UNICEF walitia saini makubaliano maalumu ya kutekeleza miradi ya ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa miundombinu ya elimu katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Songwe. Kupitia makubaliano hayo, kiasi cha takribani shilingi bilioni 2.5 kimetumika kutekeleza miradi 48 hadi kufikia sasa, hatua inayoonesha dhamira ya dhati ya kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia hapa nchini.
Katika kuendeleza ushirikiano na wadau wa Sekta ya Elimu nchini, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF Tanzania) wamefungua rasmi milango ya utekelezaji wa miradi ya elimu visiwani Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA), kwa lengo la kuboresha miundombinu ya elimu.
Kupitia ushirikiano huo, TEA na UNICEF wametenga jumla ya shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa, maabara za sayansi pamoja na matundu ya vyoo katika shule 20 ambapo, shule 11 zipo kisiwani Unguja na shule 9 kisiwani Pemba.
Akizungumza wakati wa kikao kazi maalum cha kujadili utekelezaji wa miradi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha alisema, utekelezaji wa mradi unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari na kukamilika kabla ya mwezi wa sita mwaka huu.
Dkt. Kipesha alibainisha kuwa lengo la mradi huo ni kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora, salama na rafiki kwa afya zao. Aliongeza kuwa TEA ni taasisi ya Muungano hivyo utekelezaji wa miradi ya elimu Zanzibar ni sehemu ya majukumu yake ya msingi.
Aidha, alisisitiza kuwa ushirikiano uliopo kati ya TEA na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar umekuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya miradi mbalimbali ya elimu inayotekelezwa na ambayo imekamilika.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Said, aliishukuru TEA kwa mchango mkubwa kwenye uboreshaji wa miundombinu ya elimu huku akieleza kuwa miradi hiyo imekuwa kichocheo cha wadau wengine kujitokeza kusaidia maendeleo kwenye sekta ya elimu.
Bw. Said aliongeza kuwa ukarabati na ujenzi wa miundombinu hiyo umefika wakati muafaka kwani majengo mengi ya shule hizo ni ya kizamani na yako katika hali isiyoridhisha. Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutachangia kuinua kiwango cha taaluma kwani wanafunzi watapata motisha ya kusoma katika mazingira ya kisasa.
“Wizara inatoa shukrani za dhati kwa TEA kwa ushirikiano mkubwa mnaoendelea kutupatia katika kuboresha miundombinu ya elimu na tunawaahidi kusimamia utekelezaji wa miradi yote kwa ufanisi ili ilete tija kwa maendeleo ya sekta ya elimu,” alisema Bw. Said.
Kwa sasa TEA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya miundombinu ya elimu Zanzibar kama taasisi ya Muungano. Awali, jumla ya shilingi bilioni 3.2 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya mafunzo ya amali ambayo utekelezaji wake bado unaendelea huku shilingi bilioni 2.5 zikitengwa kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa madarasa, maabara za sayansi na matundu ya vyoo.
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo Januari 13, 2025 imeshiriki katika maonyesho maalum yaliyoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA) kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Wataalamu wa Uhasibu. Maonyesho hayo yamefanyika katika viwanja vya jengo la Mhasibu Posta, jijini Dar es Salaam.
Ushiriki wa TEA katika maonyesho hayo ni sehemu ya jitihada za Mamlaka katika kutangaza shughuli zake pamoja na kuimarisha uhusiano na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu kutoka taasisi tofauti.
Kupitia maonyesho hayo, TEA ilitumia fursa hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka hiyo pamoja na mchango wa mfuko huo katika kusaidia jitihada za Serikali za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia nchini.
Akizungumza wakati wa maonyesho hayo Afisa Mawasiliano wa TEA Bi. Eliafile Solla, amewahimiza wadau wa elimu kushirikiana na Mfuko wa Elimu wa Taifa kwa kutoa michango mbalimbali itakayoongeza uwezo wa mfuko huo kufadhili miradi ya elimu katika maeneo mbalimbali nchini.
Bi. Solla amesema kuwa, lengo kuu la Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na TEA ni kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu bora na kwa usawa bila kujali mazingira au hali ya kiuchumi anayotoka.
Kutokana na ushiriki wake mahususi na mchango wake katika maonyesho hayo, Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA) imeitunuku Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) cheti maalum cha shukrani na utambuzi.
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ni taasisi ya umma iliyo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inayosimamia Mfuko wa Elimu wa Taifa wenye lengo la kukusanya rasilimali fedha na vifaa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu, ikiwemo ujenzi wa madarasa, mabweni, maabara za Sayansi na nyumba za walimu, ili kuongeza upatikanaji wa elimu bora kwa usawa nchini.
Baadhi ya wanawake wa TEA wameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa, yaliyofanyika, Machi 8, 2025, jijini Arusha. Tukio hili limewakutanisha wanawake wa sekta mbalimbali likiwa na kauli mbiu "Wanawake na Wasichana 2025; Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji."
Watumishi wanawake wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Machi 7, 2025 wametembelea Kituo cha Kulea Watoto Miuji Nyumba ya Matumaini Jijini Dodoma kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
https://t.co/YhNdXRjAOV
Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Dkt. Leonard Akwilapo pamoja na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Erasmus Kipesha leo Machi 7, 2025 wameshiriki matembezi ya hisani kuadhimisha miaka 50 ya TET. Matembezi hayo yaliongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa Mgeni Rasmi.
Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Dkt. Leonard Akwilapo pamoja na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Erasmus Kipesha leo Machi 7, 2025 wameshiriki matembezi ya hisani kuadhimisha miaka 50 ya TET. Matembezi hayo yaliongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa Mgeni Rasmi.
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ina jukumu la kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kusaidia uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora na kwa usawa kote nchini. #educationforall
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dkt. Leonard Akwilapo, amekabidhi vyeti kwa shule tatu zilizonufaika na miradi ya Mfuko wa Elimu wa Taifa baada ya kukamilika kwa ujenzi wake katika Halmashauri za Wilaya ya Mtama na Masasi. #eduationforall
Karibuni kwenye maonesho ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023, yanayoendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma. TEA ipo tayari kutoa elimu kuhusu miundombinu ya mitaala iliyoboreshwa
https://t.co/ZbeC5MYuwc
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ametembelea banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika maonesho ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre.
https://t.co/bCfDoR6AqT
Kheri ya Siku ya Kuzaliwa Mhe. Dkt. @SuluhuSamia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) itaendelea kusimamia uboreshaji wa miundombinu ya Elimu ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu bora na kwa usawa.
https://t.co/o5kYoJm2uV
Ufadhili wa UNICEF kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) umewezesha Shule ya Msingi Kazaroho kuboresha mazingira ya kujifunzia, hatua ambayo imechangia kupunguza utoro.
https://t.co/lv0nXchEHK