#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 312
Katibu Mkuu wa Chadema anaendelea kutoa ushahidi wake.
Mnyika : Matendo aliyotuhumiwa nayo hayajawahi kutokea na DPP alipeleka hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo na kesi ilifutwa na Mwenyekiti Mbowe alikutana na Rais Ikulu. Toka kuwa mtuhumiwa wa UGAIDI hadi MAPOKEZI IKULU.
Watu wanacheka.😂😂😂😂😂
Na Lissu anasema kwa kejeli kwamba na Mimi itakuwa hivyo hivyo?😂😂😂
Mhe. Lissu: Hayo makesi yote na hii yangu vina uhusiano gani?
Mnyika: Hizi kesi zote ni mwendelezo wa kupambana na Chadema kwa kutumia Mahakama kukwamisha mapambano ya kudai demokrasia ya kweli na mabadiliko katika mifumo ya Uchaguzi. Haya ni matumizi yasiyo ya haki dhidi ya wapinzani ambao ni CHADEMA kutoka kwa Chama dola ambao ni CCM. Lengo lao ni kukwamisha mabadiliko tunayohitaji. Hivyo huu ni mwendelezo wa mambo mabaya ambayo yamekuwa yakifanywa na hawa serikali dhalimu.
Anataka kusimama Ajuaye.
Mhe. Lissu: Subiri namaliza muda sio mrefu. Umenifahamu lini?
Mnyika: Toka 2003 tukiwa wote kwenye sekretarieti, baadae Kamati Kuu na Baadae Bungeni miaka 23 nakufahamu.
Mhe. Lissu: Huyu mtu ni mtu wa aina gani ambae umemfahamu kwa miaka 23?
Mnyika: Toka mwaka 2003 tulipoenda kule Kwembe, nimekufahamu kama mtaka mabadiliko, ni mtu mkweli ambae siku zote umekuwa ni mtu unayetaka mabadiliko. Mimi naamini MASHITAKA HAYA NI GHARAMA UNAYOLIPA KWA KUWA MKWELI NA KUTAKA MABADILIKO NDANI YA TAIFA HILI.
Mhe. Lissu: Mheshimiwa Jaji nimemaliza kwa shahidi huyu.
Maneno aliyomalizia JOHN JOHN MNYIKA yamewafanya akina Mama waliopo humu MAHAKAMANI WATOE MACHOZI.
Yamekuwa ni maneno mazito sana na yenye ujumbe mzito, watu wamesikitika sana.🥹
Majaji wanaandika na kwa muda tulionao. Tutakwenda break na kurudi kwenye Cross Examination ya upande wa Jamhuri.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 305
Mnyika anasema na Katika mazungumzo hayo akaeleza kuwa upande wa Chadema uliwasilisha kwa mazungumzo na kwa maandishi mapendekezo ya maeneo ya marekebisho na mabadiliko ya Kikatiba ya kuwezesha Uchaguzi huru na Haki. Na namna ambavyo mwaka mmoja wa mazungumzo upande wa CCM na Serikali ulijibu kwa mdomo na maandishi kukataa mapendekezo yote ya CHADEMA ya marekebisho ya KATIBA
Mhe. Lissu: Mapendekezo hayo yalikuwa yanahusu nini?
Mnyika: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025. Kwa kifupi ni mapendekezo ya kubadilisha sheria za uchaguzi huo.
Mimi nilikuwa sehemu ya timu ya watu 10 iliyokutana na Rais mwezi 22 Mei, 2022 na Katika Timu yetu na mazungumzo na Rais mapendekezo ya kukwamua Mchakato wa Katiba Mpya yaliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wakati huo. Freeman Mbowe.
Anaendelea Mnyika.
Mapendekezo tuliyokuwa nayo ni pamoja na marekebisho ya kisheria na Kikatiba niliwasilisha mimi uchaguzi wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025. Iwapo Mchakato
Jaji Ndunguru: Shahidi kuna maji kidogo. Wenzako tunaandika kuna muda midadi inakupanda unaongea mfululizo.
Mnyika: Nashukuru ngoja ninywe sasa.
Watu wanatabasamu.
Mapendekezo tuliyoyatoa ni kwamba kutokana na muda uliokuwa umebaki basi tufanye marekebisho katika maeneo mahsusi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki na tuliziita ni Minimum Reforms.
Mhe. Lissu: Kikao cha Rais alisemaje sasa?
Mnyika: Alisema nimeyapokea na kwa mazungumzo zaidi na akaahidi timu ya watu watano kutoka CCM ambayo iliongozwa na Abrahaman Kinana na sisi Mwenyekiti Mbowe alisema ataunda Timu ya Watu watano ambayo na mimi nilikuwa sehemu ya watu hao.
Mhe. Lissu: Mazungumzo hayo kati ya Timu ya CCM yakiongozwa na Kinana na Timu ya CHADEMA yaliishia wapi na matokeo yake yalikuwa nini?
Mnyika: Yaliendelea kuanzia Mwezi June, 2022 mpaka tarehe 31/05/2023
Hadi kipindi hicho walitujibu mchakato wa Katiba Mpya usubiri hadi uchaguzi mkuu wa 2025 na pili marekebisho yoyote ya Katiba yanayohusu Uchaguzi na yanayogusa Katiba hata kama ni muhimu vipi lakini yasingewezekana kwa kipindi hicho.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi waeleze Waheshimiwa Majaji.
Anasimama Ajuaye: Waheshimiwa Majaji muda sio rafiki na tumepokea concern kutoka watu wa usalama kuwa saa 11 imefika.
Wanateta Majaji kule juu. Na wanamchungulia Mh. Lissu kwenye miwani kuona anataka nini?
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa unasemaje?
Mhe. Lissu: Wamesema masuala ya Ulinzi na Usalama mimi nitajuaje.
Jaji basi tukutane Jumatatu saa tatu kamili asubuhi tukutane hapa. Ahsanteni.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 219
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross Examination Shahidi wa Jamhuri Coplo Amani.
Coplo Amani.: mimi sijalisema tu kama wewe umelisema basi ndio umesema.
Mhe. Lissu: Ni kweli kwamba P3 alikwambia kuwa ni mwanachama wa CHADEMA, kweli au si kweli
Coplo Amani : sio kweli
Mhe. Lissu: Wewe ndio uliandika maelezo yake kielelezo D12
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: Sasa ngoja nikusomee… “mimi pia ni mfuasi na mwanachama wa CHADEMA” kweli si kweli.
Coplo Amani : kweli
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama kwenye maelezo yako uliyasema hayo
Coplo Amani : sikuyasema
Mhe. Lissu: Alikuonyesha kadi yake cha chama
Coplo Amani : sikutaka anionyeshe
Mhe. Lissu: alikwambia wafuasi wa chadema wana alama gani?
Coplo Amani : sikumuuliza mm
Mhe. Lissu: ndo maana nasema huyu ni askari wa kitengo cha intelijensi halafu mnasema ni shahidi.
Mhe. Lissu: Turudi kwa Inspekta Jorum, ni kweli polisi inapopokea watu waliofanya uhalifu , Polisi wanafungua investigation register?
Coplo Amani : ni sahihi
Mhe. Lissu: waelezze majaji kama kwenye maelezo yako polisi walifungua investigation register
Shahidi: sijui
Mhe. Lissu: Waeleze majaji baada ya maafa yote hayo ya October 29 kama mmemchukulia hatua yoyote huyu baada ya kusema atapiga watu mawe?
Coplo Amani: Simfahamu chochote kuhusu swali lako
Mhe. Lissu: inaingia akilini hii
Coplo Amani : Mimi sifahamu chochote kwa kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama unajua mashahidi wote wa kificho walisema waliona hiyo video yangu maarufu tarehe 4 april
Coplo Amani : Mimi sio mpelelezi wa mafile yote
Mhe. Lissu: Na unahabari wote waliokuja hapa ni boda boda na machinga hakuna afisa wa serikali au n.k
Coplo Amani : sina habari
Mhe. Lissu: Ulipomuachilia P3 kwa dhamana ulichukua hatua gani kuhakikisha aendelei na kupiga watu mawe na uasi?
Coplo Amani : sikupewa hilo jukumu
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji mimi sina maswali ya ziada.
Serikali: Kwa leo tulikua na shahidi huyu tu mmoja, tunaomba ahirisho kwasababu hali ya hewa ya Dar es salaam imebadilika na zimebaki dakika 20.
Kwasababu za kiusalama tunaomba ahirisho hadi siku ya Jumatatu ili tuje kuendelea kusikiliza juu ya notice tuliyoileta
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kwa dakika 20 kwangu si haba, mimi ninaomba hizi dakika 20 kwasababu nilishasema nina mapingamizi, naomba niongee juu ya hayo leo ili tusiathiri muda wa mashahidi wengine Jumatatu.
Naomba nipate hizi dakika 20 kwasababu mimi niliyepo Gerezani ndiye ninayepata shida, kwahiyo naomba tutumie hizi dakika jambo lifanyike.
Wakili wa Serikali: Waheshimiwa sisi tunaomba ahirisho lakin vilevile kama mnavyojua dini zote mbili tupo kwenye mfungo kwahiyo tunaomba ahirisho.
Lakini vilevile PO yake haijasajiliwa bado kwahiyo kama ataweza kuisajili na kuisikiliza basi aisajili na sisi tupewe nafasi ya kuiona ili tu-submit
Mhe. Lissu: waheshimiwa majaji sikutarajia kwamba hili litakua na kubishana namna hii, nililetewa hii notice jana na nikatoa notice ya mdomo kwamba naipinga tena immediately nilipopatiwa tu notice hii.
Naijua sheria, sasa wanaposema tuahirishe ili niendelee kukaa gerezani ni sawa tukutane Jumatatu ili tuzungumzie PO yangu niliyoileta jana.
Na jana nilisema kabisa PO ni ya kisheria na itaenda na kifungu icho icho cha 308(1) cha CPA, mimi nakaa gerezani kwasababu ya michezo hii mnayoleta mawakili wa serikali kila siku.
Jaji Ndunguru anasema shauri litaendelea siku ya Jumatatu, tunatarajia serikali mlete mashahidi, tutaanza na hoja ya notice, tukimaliza tutaendelea na mashahidi wengine.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 195
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi
Mhe. Lissu: Kwanini umepewa Jina la P7?
Shahidi wa kificho P7 : Kwasababu ya usalama wangu.
Mhe. Lissu: Si umesema hakuna aliyekutishia.
Shahidi wa kificho P7 : Ndio hivyo sasa.
Mhe. Lissu: Sina Maswali mengine.
Jaji: Karibu upande wa Serikali kwa Re Examination.
Wakili wa Serikali: Hatuna maswali kwa shahidi huyu.
Upande wa Serikali walisema wana shahidi mmoja tu kwahiyo kesi itaendelea kesho saa tatu asubuhi bila shaka.
Majaji wanaandika kidogo pale mbele.
Wakili wa Serikali: Renatus Mkude anasimama anasema kama tulivyosema asubuhi naomba tuahirishe hadi kesho asubuhi.
Jaji: Tafadhali tukutane hiyo Kesho Tarehe 19 saa tatu asubuhi.
Inapigwa high court
Watu wote tunasimama,
Majaji wanaondoka,
Watu wanaanza kutawanyika.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 189
Wakili wa Serikali anaendelea kumuongoza shahidi wa kificho P4
Wakili: Nini kingine?
Shahidi wa kificho P4 : Tulivyoenda kuripoti Tarehe 17/04 tuliambiwa tusubiri tuandikwe maelezo, nikaandikwa hayo maelezo.
Wakili: Unamfahamuje huyo Tundu Lissu?
Shahidi wa kificho P4 : Namtambua kama Mwanasiasa Mkubwa kwenye hii Nchi.
Wakili wa Serikali Winiwa Kasawa anasema Waheshimiwa Majaji ni hayo tu.
Jaji Ndunguru: Maswali ya Dodoso Karibu Mshitakiwa.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi jibu maswali kama hujui sema hujui sema najua kama unajua na kama umesahau sema nimesahau.
Mhe. Lissu: Umesema unakaa Arusha?
Shahidi wa kificho P4 : Kweli
Mhe. Lissu: Wambie Majaji umekuja Dar es salaam lini?
Shahidi wa kificho P4 : Leo nina siku ya pili.
Mhe. Lissu: kwahiyo umekuja Jumapili ya juzi?
Shahidi wa kificho P4: Ndio.
Mhe. Lissu: Nani alikwambia uje Dar es salaam
Shahidi wa kificho P4 : Hiyo nashindwa kusema hapa.
Mhe. Lissu: Utasema tu. Mimi sikuoni na watu hawakuoni. Wambie majaji ndio wanaokuona pekee kuwa nani alikwambia uje Dar es salaam
Shahidi wa kificho P4 : Nilipigiwa simu.
Mhe. Lissu: Na nani alikupigia simu.
Shahidi wa kificho P4 : Mtu alijitambulisha kuwa ni Wakili wa Serikali.
Mhe. Lissu: Alikwambia jina lake?
Shahidi wa kificho P4 : Ninazo sababu binafsi
Mhe. Lissu: Kwahiyo majaji waandike kuwa umekataa kusema sababu kwanini hutaki kumtaja aliyekuita Dar es salaam sawa muraaaaa
Shahidi wa kificho P4 : Ndio.
Mhe. Lissu: wapo wakurya wenzako humu.
Mhe. Lissu: Ieleze Mahakama kama ulipata summons ya Mahakama?
Shahidi wa kificho P4 : nilipigiwa simu nikaenda kituoni nilipata barua ya Mahakama.
Mhe. Lissu: Nani aliyekulipia nauli ya kutoka Arusha Kuja Dar es salaam?
Shahidi wa kificho P4 : Nilikuja na nauli nililipa mwenyewe maana nilikuja kwenye shughuli zingine binafsi.
Mhe. Lissu: Una nyumba hapa?
Shahidi wa kificho P4 : Sina.
Mhe. Lissu: Nani anayelipa gharama za kula na kila kitu?
Shahidi wa kificho P4 : leo nimekuja na gari ya wanasheria
Mhe. Lissu: Tarehe 03/04/2025 ulipelekwa kituo cha Polisi mjini na kabla ulikuwa kituo cha Muriet
Shahidi wa kificho P4 : Ndio
Mhe, Lissu: Hayo maelezo yalikiwa yanahusu kosa gani?
Shahidi wa kificho P4 : Walisema tuna kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi.
Mhe. Lissu: umewahi kupelekwa Arusha kwa hilo kosa ulilokamatwa nalo?
Shahidi wa kificho P4: Sikuwahi kupelekwa Mahakamani.
Mhe. Lissu: Hiyo kesi iliishia wapi?
Shahidi wa kificho P4 : Mimi sijui.
Mhe. Lissu: Hayo maelezo ya Tarehe 03/04 yako wapi?
Shahidi wa kificho P4 : Sijui.
Mhe. Lissu: Nilikwambia kwamba ulikamatwa bure tu hukuwa na kosa lolote we utasemaje?
Shahidi wa kificho P4 : Sijui mimi.
Mhe. Lissu: Siku hiyo ya Tarehe 03/04 wewe na wenzako mlikuwa mnazungumza juu ya maneno mlioyaona kwenye mtandao na wengi mliyaunga mkono
Shahidi wa kificho P4 : Ndio.
Mhe. Lissu: Je hilo lilikuwa kosa nyie kuunga mkono na kuzungumza kauli hizo.
Shahidi wa kificho P4 : Sijui
Mhe. Lissu: Maelezo yako ya 17/04 ukionyeshwa unaweza kuyatambua?
Shahidi wa kificho P4 : Naweza
Shahidi wa kificho P4 ameyatambua maelezo yake na Mh. Lissu anamsomea Maelezo ambayo shahidi aliyaandika pale Polisi.
Mhe. Lissu: Niliyosoma hapa ni sawa na maelezo uliyonayo hapo.
Shahidi wa kificho P4 : Ndio
Mhe. Lissu: Sasa shahidi nataka kukuhoji kuhusu hayo maelezo.
Shahidi wa kificho P4 : Sawa.
Mhe. Lissu: Maeneo hayo ni
1. Uliperuzi kwa simu yako
2. Nilisema tutakinukisha
Anamtajia maeneo kama 8 hivi ambayo atamuuliza maswali.
Mhe. Lissu: Je ungependa yawe sehemu ya ushahidi?
Shahidi wa kificho P4 : ndio.
Jaji: Jamhuri mnasemaje?
Wakili Renatus: sina pingamizi.
Jaji: Hiyo itakuwa ni D9 upande wa utetezi.
Part 190 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 15, 2025
Part 16.
Mahakama imejaa watu kama kawaida ila sasa hivi naona watu nyuso zao zimechangamka tofauti na asubuhi maana wote ni kama tulikuwa kwenye Hali ya simanzi baada ya Polisi kutumia nguvu kuzuia watu kuingia Mahakamani.
Kuna watu wengi wameumizwa wengine wamekamatwa wapo Central akiwemo Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Wakili Mahinyila.
Sasa tuendelee
Tayari Mawakili wa pande zote wameingia Mahakamani.
Mhe. Lissu pia na yeye ameingia.
Imepigwa ile Cooooooort ya kikakamavu sana bila Shaka huyu jamaa wa leo atakuwa amepigwa Lunch inayoeleweka.😂
Waheshimiwa Majaji wote watatu wameingia na kuketi kwenye viti vyao.
Sasa Mahakama imeanza rasmi
Anasimama Wakili wa Serikali Katuga anasema ikupendeze mheshimiwa jaji upande wa Jamhuri Coram iko kama ilivyokuwa awali na mshitakiwa yupo tayari kizimbani.
Shauri linakuja kwa ajili ya mshitakiwa kusomewa mashitaka na kwa upande wetu tuko tayari.
Jaji Nduguru anamuita Mhe. Lissu
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa majaji nina mambo mawili kabla ya kuendelea.
Jambo la kwanza wiki jana wakati naomba nyaraka kama nilivyoomba leo nilipewa ikiwa imebakia dakika 8 turudi mahakamani.
Leo tangu tumeahirisha kesi asubuhi nimepewa nyaraka saa nane na dakika 9 na saa hizi ni saa nane na dakika 30.
Sasa waheshimiwa majaji hii kesi ni ya uhaini sio kesi ya kesi ya kuuza mbege bila kibali cha kuuza mbege.
Watu wanacheka 😂😂😂😂
Jaji Nduguru anasema tuwe watulivu, tuheshimu Mahakamana.
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa sitaki tuahirishe kesi kwa sababu hiyo ila naomba wanaotoa nyaraka wapewe onyo na wajue hii ni kesi kubwa.
Jambo la pili Tar 4/9/2025 niliandika barua kwa msajili nikiomba kesi hii irushwe live kwa sababu ni kesi kubwa lakini mpaka sasa sijajibiwa.
Naomba kesi hii irushwe live kwa sababu ya ukubwa wake ni hayo tu waheshimiwa majaji.
Kuna ukimya hapa mahakamani ni ingekuwa enzi zetu za utoto tungesema shetani kapita.😂
Naona majaji wanajadili kidogo.
Jaji Nduguru anaita upande wa jamhuri?
Anasimama tena Katuga anasema waheshimiwa majaji tumesikia tukianza na hilo la kupewa nyaraka saa nane na dakika 9 ambapo amesema licha ya hilo hana nia ya kuahirisha.
Waheshimiwa majaji sisi tuko tayari kuendelea lakini kwa kuzingatia maelekezo yenu wakati tunatoka.
Na kwa kuzingatia pia kuwa kwenye ile notice of Motion ambayo anaonyesha kuna mapingamizi mawili ikiwemo hili la kupinga hati ya mashtaka.
Sasa hoja yetu ni kwamba kwa kuwa imeingia kwenye rekodi kuwa amepewa nyaraka hizo saa nane na dakika 9 na muda huu ni saa nane na dakika 40 je muda huu unatosha yeye kuwa amesoma na kujiandaa?
Ni rai yangu kwa kuwa mahakama ilitaka chini ya kifungu cha 266 cha sheria ya mwenendo wa makosa.
Tunaona muda huu kwa minajiri ya fair trial
hivyo tunaomba apewe muda ili akasome na kuandaa utetezi wake kwa muda wa kutosha.
Japo kuwa hakuna muda maalumu umewekwa na sheria wa yeye kujiandaa the law is silent lakini ni busara kuwa apewe muda wa kutosha ili akajiandae vizuri.
Kwa maneno mazuri mahakama ione busara kumpa muda wa kutosha ili akajiandae vya kutosha.
Huyu Katuga ni kama alifanya makusudi kuchelewa kumpa Mhe. Lissu Nyaraka ili apate sababu ya kuomba kesi ihairishwe ngoja tuone mwisho Majaji wataaamua nini?
Haya tuelendelee na kesi yetu
Anaendelea Katuga
Waheshimiwa majaji kuhusu hili ombi la pili sisi tunakiri kupewa nakala (copy) ya kuomba live streaming lakini ni mahakama hii ndio ina mamlaka ya kuamua juu ya hili.
Waheshimiwa majaji hili ni ombi linatakiwa lifanywe wakati kesi inapoanza kusikilizwa "trial"
Part 17 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 7
Anaendelea Mhe. Lissu
Hichi kinachoonekana intended to deceive me.
Sasa niendelee nafikiri hiyo hoja tumeiweka vizuri.
Wakili Kiswaga samahani Wakili Katuga.
Watu wanacheka. 😂
Nimelelewa na one among the best state attorney naomba nisamehewe.
Sio Wakili Kiswaga ni Wakili Katuga. Naomba niendelee ni rafiki zangu hawa.
Ni kama Katuga alisema unalalamika nini wakati sisi ndio tulikuombea.
Kwahiyo huna ulichonisaidia.
It was My own expozeeee🤣 nililiibua mimi sio Katuga. Asijipe umuhimu kwenye hili.
Hoja ya tatu ya Katuga juu ya maahirisho.
Naomba kuna kitu niseme kidogo kwenye forgery zipo proceedings za Tar. 13 hazijawahi kuonekana. Hazipo.
Anasimama Katuga anasema hayo ya Tar 13 hakusema.
Lissu anasema nilisema hayo na mahakama iangalie kama sikusema basi naomba niendelee na nyie angalieni huko.
Sasa nirudi kwenye maaahirisho.
Sasa kwamba sheria kuhusu adjournment haikufuatwa basi ni grievances yaani malalamiko tu na hapa sio mahala pake.
Sasa namjibu kwamba kweli I was aggrieved by the adjournment. Sikufurahishwa nayo kabisa. Hilo la kwanza.
Na my grievances zipo kufungu cha 265(1) cha CPA kinaleeza utaratibu wa kuahirisha kesi wakati wa committal.
So of course I'm aggrieved kwasababu sheria imekiukwa at my expense.
S. 265 ya CPA inasema anaisoma.
Tafsiri yake ni kwamba kila kesi inapoahirishwa wakati wa committal lazima sababu zitolewe.
Na zile kesi za akina Kapufi zilisema mahakama ya ukabidhi lazima ifuate sheria za ukabidhi.
Kwanini sheria inataka sababu za msingi ziwepo na sababu hizo ziandikwe?
Mimi naishi gerezani kwenye maximum security prison. Najua nini maana ya kuishi kule.
Nafikiri Katuga hajui labda amwambie haya maneno naona hayasemi hapa.🤣
Sasa sheria inasema labda sababu za msingi ziwepo pale unapoamua kumpeleka gerezani uwe na sababu za msingi. Na hizo sababu ziandikwe. Hiyo ni sheria inasema sio Katuga.
Katuga anakuna kinywa Kama mtu mwenye mba ule unaochoma choma hasa ukisuka nadhani hapa wadada wenzangu mnanielewa vema, nyie kaka zangu hamuwezi kuelewa hii.😂
Haya tuendelee na Mhe. Lissu
Katika mara 13 ambazo kesi iliahirishwa ni mara tatu tu ndio ilitoa sababu mara 10 walikaa kimya.
Kama nilivyoonesha kwenye rekodi ilipigiwa kelele na mawakili wangu na baadae nilipoamua kujitetea mwenyewe. Hatukuacha kupiga kelele.
Na Hakimu Kiswaga ali ignore concern zetu na hata hakuandika sababu za kuahirisha.
So I paid for those adjournments sasa anaposema sijaonesha namna gani nimeathiriwa na maahirisho hayo.
Sasa unahitaji kuwa katili kiasi gani? An innocent man as per Constitution living with condemned prisoners
Halafu anatokea mtu anasema eti ameumiaje?
Amesimama Katuga anasema hakusema kama aliathirikaje kwahiyo asiende huko.
Lissu anasema nilisema Mhe jaji siku kadhaa. Anarudia maneno aliyosema.
Jaji Ndunguru anasema hayo ni kweli ulisema.
Katuga anasema sasa jaji hakusema aliathirika vipi?
Watu wanazomea.😁😁😁😁
Jaji anasema nafikiri alisema Tundu Lissu hebu endelea.
Waheshimiwa majaji wanaoahirisha kesi na wanaotakiwa kutoa sababu ni mahakama ya kisutu na Wakili wa serikali Katuga akiwa hapa Mahakama kuu.
Haya aliyosema wakili wa serikali Katuga yalipaswa yaonekane kwneye rekodi za mahakama. Iseme mahakama yenyewe.
Hakuna mahali kwenye rekodi zinasema tunaahirisha kwasababu mtuhumiwa hayupo. Haipo.
Sasa yeye aliyokuwa anasema kuwa eti kuna siku mtuhumiwa hakuwepo. Hayo tunayapata wapi? Ukurasa wa ngapi? Hajaonesha na haipo.
Nimesema ni mara tatu tu mahakama imewahi kuahirisha kw kutoa sababu na hizo sababu haijawahi kutolewa kuwa ni mtuhumiwa hayupo kwenye hizo mara tatu.
Hili jaribio la to shift the burden with the committal Court wanataka tushare dhambi. Mimi siko tayari. Labda Katuga na Kiswaga ila mimi hapana siko tayari kushare hiyo dhambi.
Part 8 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
@Ntobi_@Magundujunior@tanpol@TunduALissu Kwa mara ya kwanza natambua siasa ni ajira kama ilivyo shamba na biashara,Kuna muda biashara hufa mtu huamua kuwa mvuvi Kwa nini nyie vijana msibadirike!!!