USIJUTIE kamwe kuwa na MOYO MWEMA Kila WEMA unaoufanya hurudi KWAKO MARA nyingi zaidi inaweza isiwe LEO au KESHO ila ipo SIKU utakurudia. #Orucho_thoughts
Baadhi ya hisia ni za THAMANI kubwa na ni NZITO na za kweli kiasi kwamba hazijakusudiwa kwa KILA MTU. Ikiwa unamweka mtu moyoni mwako
Basi hakikisha ni MTU SAHIHI SANA. #Orucho_thoughts
Watu wanalipwa kwa sababu ya AJIRA ZAO(nafasi aliyopewa na MWAJIRI ili kutekeleza MAJUKUMU fulani kwa MALIPO)
lakini si kwa Sababu ya KAZI ZAO, Wengi wetu tuna AJIRA ILA HATUNA KAZI. (Rudia ×2)
#Orucho_thoughts
"Dakika TANO baada ya KUZALIWA wanaumua JINA LAKO, UTAIFA WAKO, DINI YAKO, Na DHEHEBU LAKO, na unatumia maisha yako yote UKILINDA vitu ambavyo HUKUVICHAGUA"
Arthur schopenhauer
#Orucho_thoughts
Kila UKARIBU wa KWELI hubeba uwezekano wa MAUMIVU MAKUBWA, kwa sababu watu walio karibu zaidi na MOYO wako ndio wenye uwezo mkubwa zaidi wa KUKUPONYA AU KUKUUMIZA. #Orucho_thoughts
kadri mtu anavyojua MAMBO YAKO MACHACHE ( specialist) ndivyo anavyozidi KUKUFAHAMU ZAIDI.
ILA kadri anavyojua MAMBO
YAKO MENGI (generalist) ndivyo anavyoanza KUTOKUKUFAHAMU KWA KINA. ✍️
#Orucho_thoughts
kadri mtu anavyojua MAMBO YAKO MACHACHE ( specialist) ndivyo anavyoanza KUKUFAHAMU ZAIDI.
ILA kadri anavyojua MAMBO
YAKO MENGI (generalist) ndivyo anavyoanza KUTOKUKUFAHAMU KWA KINA. ✍️
#Orucho_thoughts
Kama unajiwekea AHADI
mwenyewe na UNAZIVUNJA basi usitegemee kumpata mtu mwingine MWAMINIFU zaidi yako, siku ukianza kuwa mwaminifu KWAKO MWENYEWE Dunia itakuunganisha na waaminifu wengine. #Orucho_thoughts
Huwezi kutabili FURAHA, na Huwezi kuahirisha furaha hadi wakati ujao, ILA unaweza kuchagua kinachokuletea TABASAMU USONI na shangwe moyoni SIKU YA LEO na KUKIFURAHIA na siyo kusubiri hadi kesho kwani unaweza kupata fedha zaidi lakini hautowahi kupata siku kama ya LEO tena.
LOVE BOMBING
Kuna aina hii ya upendo unaitwa LOVE BOMBING ukikutana na mtu mwenye UPENDO huu atakuonyesha upendo wa kila namna,zawadi, muda na umakini wa kupindukia, lengo UMWAMINI haraka ila ndani yake SIYO upendo bali ni HASHIKI.
#Orucho_thoughts
Asiye taka UDUGU NA MUNGU hafai kuwa na UDUGU na Wewe.
"Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. Kwa maana yeyote anayefanya MAPENZI YA BABA YANGU ALIYE MBINGUNI, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu." (Mathayo 12:48–50)
#Orucho_thoughts
Kuna wakati watu WATAKUCHAFUA ila wakati huu ndiyo wakati wa kuambia kuwa
"Mungu si Mungu wa MACHAFUKO, bali ni Mungu wa AMANI" 1kor 14:33.
#Orucho_thoughts
Ni kweli unaweza poteza VITU au WATU wa muhimu, ila hakikisha HAUJIPOTEZI MWENYEWE au kupoteza uwezo wako wa kutengeneza kitu kwa AJILI YAKO mwenyewe.
#Orucho_thoughts
Ubongo una TABIA ya kuona kile unachouzoesha KUONA.
Ukiuzoesha KUONA mazuri ya watu katikati ya mapungufu yao, Basi UTAWAFURAHIA WATU, ila ukizoesha kuona makosa yao utaishia KUVUNJWA MOYO.
#Orucho_thoughts
Ilikuwa ni wiki nzito, yenye kutuacha tukiwa TUMECHOKA, huku tukiwa hatujatimiza malengo yetu, lakini
sasa tumefikia MASAA mazuri ya TABIBU MKUU kuponya akili, mwili na nafsi zetu, huku Akiijaza mioyo Yetu Tumaini Jipya. #Orucho_thoughts