Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesema nchi si sehemu ya kufanyia majaribio au mazoezi ya uongozi, huku akibainisha kuwa uteuzi wa hivi karibuni wa Makamu wa Rais umezima rasmi kejeli za muda mrefu zilizokuwa zikitumiwa kuwabeza wapinzani kuhusu ukosefu wa uzoefu.
Akiandika Agosti 29, 2026, kupitia mtandao wa Facebook kwenye makala aliyoiita "Ukakasi na Uhaini Mamboleo", Askofu Bagonza ameeleza kuwa mtu yeyote awe kijana, mzee, mpinzani au msomi anaweza kuongoza vyema iwapo ana utashi wa dhati wa utumishi.
Akimtaja moja kwa moja Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, Askofu Bagonza amemshauri kutoangalia ujana wake kama mtaji wa kisiasa, bali autazame umakamu wa rais kama dhamana nzito aliyopewa katikati ya mazingira magumu na yenye miiba.
Kiongozi huyo wa kiroho amesisitiza kuwa heshima ya madaraka inapaswa kulindwa bila kujali umri au jinsi, akirejea uzoefu wake alipotawazwa kuwa Askofu akiwa na umri wa miaka 38 ambapo alikataa kuitwa "Askofu Mtoto" ili kuzuia watu kutumia utoto wake kulihujumu kanisa.
“Kinachosumbua vichwa vya wengi si umri wala makolokocho mengine. Ni namna ya kuingia na kutoka madarakani... Ufa kati ya matajiri na maskini ni mkubwa sana, ufa kati ya wananchi na serikali ni mkubwa mno. Haya mawili yanadai uongozi na si utawala,” alisema Askofu Bagonza.
Amehitimisha kwa kutoa tahadhari kuhusu dhana ya "uhaini mamboleo", akieleza kuwa upo uhaini unaoweza kutendwa na wananchi dhidi ya serikali, lakini pia upo uhaini unaotendwa na serikali dhidi ya wananchi wake pale inaposhindwa kuwasikiliza na kuwalazimisha kuonekana kama maadui.
UJUMBE WA ASKOFU KWA DR. NCHIMBI JUU YA USALAMA WAKE!
Mpendwa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi!
Pokea salaam kutoka kwetu sisi tulio Askofu.
Tunatambua kuwa wakati huu unapitia katika kipindi kigumu sana katika historia ya maisha yako ya kisiasa na utumishi wa umma.
Tumefuatilia sana mjadala ulio nyuma ya kile kilichoitwa 'kujiuzulu' kwako tumebaini ya kuwa watu wengi sana hawajadili juu ya haki zako za msingi. Watu wengi hawajui ya kuwa unaweza kuwa unapita kipindi kigumu cha kufinywa haki zako ambazo ni haki ya kujumuika (freedom of association) uhuru wa kutembea (freedom of movement), haki ya kutoa maoni (freedom of expression), haki ya kusikilizwa (natural justice) na haki ya kuishi ni haki zako za msingi ambazo sisi tutazipigania.
Ni wazi kuwa hiki ndicho kipindi ambacho watu ambao ni marafiki wako wa dhati watasimama pamoja na wewe bila kuogopa. Lakini ambao ni marafiki wa fursa wameanza kukukana na hata kukukimbia. Watajitokeza pia ambao pamoja na kuwa uliwahi kuwasaidia, wataongeza moto dhidi yako. Ikitokea hivyo, basi soma Zaburi 35.
Hakuna jambo lolote utakalotendwa kwa siri au kutendewa kwa siri litaweza kusitirika milele. Tunatoa wito kwa wenye mamlaka kulinda haki zako ikiwemo ulinzi. Ila sisi hatuwezi kupuuzia minong'ono inayozunguka ya kuwa kuna dalili kuwa usalama wako uko hatihati. Hii inatokana na ukweli kuwa kuna kauli nyingi sana za chuki dhidi yako kutoka kwa baadhi ya makada walio ndani ya UVCCM au CCM kwa ujumla.
Hatutarajii kuona yaliyomfika Balozi Humphrey Polepole yakufike na wewe. Hii ni kutokana na ukweli kuwa siku hizi mtu anayetofautiana na watawala, dawa yake inakuwa kumpoteza au hata kumuua.
Kama kweli watawala hawana mpango wowote ulio mbaya kwako, basi pia tunatarajia kukuona ukijitokeza hadharani na kuongea na vyombo vya habari na kutoa ufafanuzi hasa kuhusiana kujiuzulu kwako.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 28 Agosti 2026; Saa 6:45 usiku.
NB: Waione - Boniface Anyisile Mwabukusi Addo November Mwasongwe Askofu Lucas Judah Askofu Severine Niwemugizi Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza Askofu mteule Charles Lundu Prof. Joseph Mbele Mhe. Ezekiel Maige Mhe. Ado Shaibu
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Godbless Lema, amekosoa mwenendo wa ukarabati wa barabara ya Moshi kuelekea Arusha, akidai kuwa wananchi wanakabiliwa na usumbufu mkubwa kutokana na changamoto za njia mbadala (diversion road) wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
Kupitia maoni yake, Lema amesema safari yake kutoka Moshi kwenda Arusha ambayo ilipaswa kuwa ya kawaida iligeuka kuwa ya muda mrefu baada ya kufika Arusha saa 3:30 usiku, licha ya kuanza safari saa 12:00 jioni.
Amesema kinachokatisha tamaa si uwepo wa ukarabati wa barabara, bali ni maandalizi hafifu ya njia mbadala inayotumika wakati ujenzi unaendelea.
“Foleni, vumbi na usumbufu ni wa kiwango cha juu, huku kasi ya ukarabati ikiwa ya kusuasua,” amesema Lema.
Lema amehoji ubora wa utekelezaji wa mradi huo, akisema kasi ya kazi hiyo haiendani na umuhimu wa barabara hiyo kwa wananchi na shughuli za kiuchumi katika ukanda wa Kaskazini.
“Ukiona mwendo wa mradi huu, unaweza kudhani fedha zake zinatolewa kwenye VICOBA badala ya bajeti ya maendeleo,” amesema.
Amesema wananchi wanastahili kuona utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaoendana na thamani ya fedha zinazotumika, huku akitaka kuwepo kwa kasi zaidi katika kukamilisha ukarabati huo.
“Wananchi wanastahili barabara bora na utekelezaji wenye kasi inayoendana na umuhimu wa mradi wa ukarabati,” ameongeza Lema.
Inauma kuona kijana amenusurika kufa kwa kupigwa risasi, lakini maswali bado ni mengi kuliko majibu. Uchunguzi umefikia wapi? Ukweli utawekwa wazi lini? Wananchi tunahitaji uwazi, uwajibikaji na haki. Ukimya hauondoi maswali. #Haki#Uwajibikaji
@Whisperpicx@HecheJohn achana na tone tone tunataka acc yake ya bank kila mtu mwenye mapenzi na heche awake chochote kitu, plan ni awe na more than 1B kwa acc yake atumie atakavyo
Funzo kubwa nililojifunza kuhusu Tanzania ya sasa ni hili: Watanzania wengi wanaonekana kuchoshwa na hali ilivyo na wanatamani mabadiliko.
Katika mazingira kama haya, yeyote atakayejiweka au kuonekana kuwa kikwazo kwa matakwa ya wananchi anajiweka kwenye hatari ya kupoteza uungwaji mkono na uhalali wake wa kisiasa, bila kujali umaarufu wake, nafasi yake au historia yake.
Mungu awalinde na awapiganie!mawimbi baharini yanataisha lakini ndio yanasafirisha Meli
Ningeomba kila Mtanzania afikirie kwa kina na kisha tutoe mawazo yetu nini kibadilike kwa wanaharakati.
Mimi personally naona kama wanaharaki wengi harakati zao zinaharibu movement kuliko kupeleka movement mbele.
Just because tuko same side doesn’t mean tuangalie tu pale some of us kazi wanayofanya ni more damaging to the movement kuliko kusaidia movement.
Yani mpaka naona kama kunahitajika training ya wanaharakati kufanyika au labda kuwe na group la wanaharakati ambapo kabla mtu hajaposti upuuzi wowote ambao katumiwa DM anatuma kwenye group then wanaharakati wengine wanatoa mawazo.
Too much fake news na ukurupukaji wa habari kitu ambacho sasa kinafanya wanaharaki wote tuonekane waongo with zero credibility.
Yani wao kila kitu anachotumiwa DM wanaruka nacho without thinking.
Hakuna strategy ya mapambano hakuna matumizi ya akili, hakuna strategy ya kuondoa wananchi uwoga na kuwawekea safe space ya kukutana na wananchi wenye fikra kama zao. Hakuna effort ya kujenga sailoji ya wananchi ni kuposti upuuzi wanaokota okota huko.
Wanaharakti wengi are killing the movement instead of advancing it kwa sababu ya ukurupukaji.
Hawajui hata target audience yao ni nani na jinsi ya kuwatengenezea safe space kwenye platform zao. Wao wanadhani the whole of Tanzania is their target audience, hapana target audience ni Watanzania wanaodai ha tu.
Naomba tushauriane jinsi ya kudili na hili tatizo.
Mfano I saw 3 huge mistakes just this last week alone, tena wiki ya maandamano, Story ya kimama kukimbia nchi, then akajitokeza kuwaharibia credibility kwa wanancji, ile barua feki ya wanafunzi wa vyuo vikuu na mbaya zaidi ile ya jana usiku wa manane wanaharakati wanaposti na kuriposti habari ya kuwaarifu Watanzania kuwa wauwaji wa KMKM kutoka Zanzibar wameingia bara na kuvalishwa nguo za polisi, really, hii ndio message ya mwisho wanaharakati kuwapa waandamanaji??? So CCM wawape habari za kutisha na nyie pia muwape za kutisha.
Alafu naomba mnisamehe kwa ambao nitawakwaza. Sio kama nataka kuwa kiongozi wa movement au kujifanya mjuaji na wengine hawajui, hapana hakuna kiranja kwenye hii movement, wote tuko sawa ila lazma turekebishane la sivyo hakuna mwananchi atatoka kuandamana kwa kuhamasishwa na watu ambao hawana credibility!!!! THIS IS WHY NAONGEA!!!!!!!!! Bila kujenga credibility na uaminifu na u-seriousness na kujenga saikolojia za Watanzania hakuna Mtanzania atatoka kuandamana tena, watakuwa wanafanya maandamano ya kukaa ndani, which is not enough
Huyu alietoa wazo la Huyu mzee kutumbuliwa Daah Muumba anamuona, huyu jamaa kuna civilization flani hivi alikuwa anaileta 🥹🥹🥹
Thank you for that massage even if it's 2 minutes but we Learned something bitter, something better, something LOGIC
Kuna Muda mtu unatokwa na machozi ya Furaha ukimuona huyu Mzee akiwa na Furaha na ukakamavu wa kimwili Pamoja na Magumu anayopitia, Wachungaji na Ma-Shekhe nchi nzima Muombeeni sana Huyu mzee kila mtu kwa Imani yake Muombee sana huyu Mtu ni Hazina kubwa ya Taifa hili.
Wanaharakati, haswa mnaoposti Instagram na Tiktok tunawaomba mzingatie comments kwenye posti zenu.
Posti zenu zinakosa ushawishi sababu mnaruhusu comments za maboti wa wauwaji.
Wao wauwaji especially muuaji mkuu ana control comments kwa page yake sababu anaelewa uzito wa comments. Haya yule msemaji ana control comments, hata page ya CCM wana control comments.
Mnaharibu harakati zenu wenyewe kwa kuruhusu comments za kuvunja watu moyo. Mtu akiona posti cha kwanza ni kufungua comments ili kujua mawazo ya wengine. Ni kazi yako mwanaharakati kuhakikisha comments zoote kwenye posti zako zinatoa moyo wa maandamano.
Wananchi kutoka kuandamana is a psychological issue, msiruhusi comments zinachozesha na psychology ya binadamu.
Kama huwezi ku control comments ni bora hata usiposti harakati maana haina maana unapoteza muda. You have to control the comments.