Nimeshiriki kikao cha Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania jijinj Dodoma, kwa lengo la kuendelea kujifunza na kujiimalisha katika misingi bora ya kizalendo katika taifa letu.
MAKALLA: DKT SAMIA AMEINUA ZAO LA KAHAWA MKOA WA KAGERA
BUKOBA:KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi an Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi, CPA Amos Makalla amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mkombozi kwa kuinua zao la Kahawa mkoani Kagera.
Makalla ameeleza hayo leo Mei 18,2025 akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Bukoba Mjini mkoani Kagera akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku saba katika mikoa ya Kanda ya ziwa.
Makalla ameeleza kuwa wananchi ni mashahidi namna watu walivyokuwa wakihangaika na uuzaji wa zao hili katika mkoa huo na kwa busara za Rais Samia akasaidia kuinua kwa kuongeza bei ya zao hilo kutoka elfu hadi 6,500.
“Nyie mnajua historia ya kahawa katika mkoa huu watu wamehangaika, magendo ya Kahawa kwenda Uganda manakumbuka msako ulivyokuwa watu wanahangaikia kuuza kahawa amekuja rais, mama yetu kwa busara zake na uzalendo wake ametutoa kwenye bei ya 1000 mpama 6000 hadi 6,500,” amesema Makalla.
Makalla amewataka wananchi kuacha kuhadaika na maneno ya uongo yanayopelekwa na watu kwa lengo la kufanya uchochezi kwa kusema serikali haijafanya kitu chochote, huku wakiwa hawajua undani wa jambo hilo.
Ameongeza sio kahawa tu bali ni katika zao la Kokoa, Ufuta, mbaazi ambayo yameongezeka thamani ya mauzo yake kwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.
Hongera sana Prof Janabi kwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la afya Dunia (WHO) Kanda ya Afrika. Kura zilizopigwa ni 46 ambapo kimsingi ili kumpata mshindi alihitaji kura 24 na Dr. Janabi amepata kura 32.
"BUILDING A HEALTHIER AFRICA TOGETHER"
HOJA SITA JUU YA MARTHA KARUA KUZUIWA KUINGIA NCHINI
Leo, tarehe 18 Mei 2025, mawakili Martha Karua, Gloria Kimani na Lyn Ngugi wamezuiwa kuingia nchini wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kama wakili mwenye uzoefu na niliyeapa kutetea Katiba na uhuru wa mahakama bila kuegemea upande wowote wa kisiasa, nawasilisha hoja zifuatazo;
1.LSK Isitumike Kuendesha Siasa za Kuchagua
Miguna Miguna alipozuiwa Kenya, hatukuona msafara wa mawakili. Maandamano ya 2023 Nairobi yalipoacha vifo, LSK haikutoa mwitikio mkali. Damu ya raia bado inamwagika Mashariki mwa DRC na Uganda lakini hakuna “delegation” yoyote. Leo, ghafla Tanzania ndiyo dharura, tena kutoka LSK?
2.Mahakama Zetu Ni Huru, Si Majukwaa ya Kampeni
Mahakama ziko wazi kwa waangalizi na wafuatiliaji wanaofuata taratibu, mimi ni shahidi katika hili. Kugeuza kusikilizwa kwa dhamana ya kesho kuwa "show-off " ya kisiasa ni kujaribu kunajisi ile due-process makusudi kabisa.
3.Maafisa Uhamiaji Hawajakosea
Kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji, afisa ana mamlaka kumkatalia mtu anayetishia “utulivu au maslahi ya umma.” Haki ya Tundu Lissu kupata wawakilishi haijakiukwa, mawakili wa Kitanzania wapo, na TLS inaweza kuongeza wengine. Hata Mwasipu angeenda JKNIA angetumia grounds zipi kuzuia huu wajibu wa Uhamiaji?
4.Utawala wa Sheria Unakata pande zote mbili
Kuheshimu Katiba kunamaanisha pia kulinda Kifungu 147 (Utulivu na Maadili). Uamuzi wa mwisho juu ya dhamana upo kwa Mahakama Kuu, si wageni wenye umaarufu wa kisiasa or whatsoever!
5.Mahakama Iachwe Ifanye Kazi Bila Shinikizo
Kauli za kutoa presha kwa mahakama mtandaoni zinatishia uhuru wa wawatoaji haki. Kuna kauli huwa tunapenda kuitumia "Observers are welcome; orchestrated flash-mobs are not". Martha na wenzie waelewe!
6.Haki Lazima Iwe Haki Mahali kote
Tupime kwa vipimo vilevile yaliyotokea na hali ilivyo Kibera, Goma, Kampala na Dar, si Tanzania pekee inapogusa majina maarufu hasa ya wanasiasa basi tuone stunts za kinafiki mbele ya kamera, hii haitaleta uadilifu bali taswira ya kutafuta umaarufu binafsi kupitia makolido ya mahakamani.
Mwisho,
Nasisitiza kuwa kuzuiwa kuingia kwa Martha Karua na wenzake kumezingatia sheria, Tuheshimu kanuni na kuzingatia usawa kwa mambo tunayoamini kama wapigania haki na walinzi wa utawala wa sheria. Nitaendelea kutetea Katiba na uhuru wa mahakama, napinga shinikizo lisilofuata taratibu za kisheria au kutaka kutumia siasa kutatua jambo la kisheria!.
BREAKING: Prof. Mohamed Janabi, proposed by Tanzania🇹🇿, has been nominated as the next @WHOAFRO Regional Director during a Special Session of the WHO Regional Committee for Africa, held today in Geneva.
Prof. Janabi will be appointed by @WHO Executive Board, to be held on 28-29 May, and take office thereafter.