Mzee @freemanmbowetz
Wanyama wa porini huua/kupigana kwa sababu zinazohusiana na mahitaji ya kuishi: chakula, kujilinda, kulinda watoto au eneo. Simba anawinda kwa ajili ya chakula siyo mateso, chuki, kisasi
Binadamu ni viumbe katili zaidi ya wanyama. Binadamu anaweza kumdhuru mwingine kwa sababu ya chuki, ubaguzi, tamaa, kulipiza kisasi, madaraka au kwa sababu anaona mwingine hafai kuishi
Kutoka Mikocheni kwenda ilipo Mahakama Kuu ya Tanzania ni umbali usiozidi 5KM. Kutoka Mikocheni kwenda Rufiji ulipo mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni umbali wa 260KM
Unaweza kusafiri kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya saa tano kuhudhuria shughuli za Serikali katili ya CCM lakini huwezi kutumia dakika 10 kutoka kwako kwenda Mahakama Kuu katika kesi ya TAL?
Huwezi kwenda safari ya 5KM kumuona Mwenyekiti wako wa chama, aliyerithi kiti chako katika uchaguzi HURU na HAKI lakini unaweza kwenda 260KM kuungana na watesi wa Mwenyekiti wako?
Nini muhimu zaidi kwako? Ni wewe ulitueleza miradi ya maendeleo haiwezi kuwa mbadala wa haki za binadamu. Leo kuna watu wanatekwa na kupotezwa, wanashtakiwa kwa ugaidi na uhaini. Hujui?
Lakini umechagua nini? Nimekusikiliza ukisema “mradi wa JNHPP usichukuliwe kisiasa kwa kuwa ni mradi unaokwenda kusaidia uchumi”. Umesahau ulitueleza nini kuhusu miradi ya MAGUFULI?
Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kwa sasa ni ‘mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya CHADEMA - ni kutokana na hiki kinachoitwa ‘ustaafu’ wa uenyekiti wa CHADEMA Taifa
Kwa maana kwamba, Freeman Mbowe yupo katika kundi sogozi la WhatsApp na mengine (kama yapo) ambayo wajumbe wa kamati kuu wanajadili kwa hisia zao tofauti masuala mbalimbali ya chama
Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu CHADEMA huwezi kwenda Mahakamani katika kesi ya kiongozi wa chama, lakini unaweza kwenda katika shughuli zinazoongozwa na mwenyekiti wa CCM
Freeman Mbowe umesahau, wakati ukishtakiwa kwa makosa ya uongo ya UGAIDI, Tundu Lissu alikuwa Belgium akijiuguza majera ya risasi. Aliomba kukutana na Rais alipokuwa Brussels
Pamoja na mambo mengine waliyokubaliana, alisema Mwenyekiti Freeman Mbowe aachiwe ndiyo tufungue ukurasa mpya. Tundu Lissu alitujulisha mwenyewe hayo alipozungumza na umma.
Tundu Lissu akiwa na siku 500 gerezani. Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe hujawahi kukanyaga Mahakamani kuanzia Kisutu hadi Mahakama Kuu hata kwa bahati mbaya.
Saa 24 baada ya Mahakama Kuu kusema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya UHAINI ya uongo na uzandiki, Freeman Mbowe unaibuka katika shughuli za Serikali ukiwa na MAWAZIRI.
Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA umekataa kabisa kuhudhuria shughuli zozote za CHADEMA lakini unaweza kuhudhuria shughuli unazoalikwa na WATAWALA KATILI wa CCM.
Unahudhuria shughuli za Serikali umeongozana na mawaziri wa Serikali katili ya CCM wakati ambao wanachama na wafuasi wa CHADEMA kwa mamia wamekamatwa na kushtakiwa kwa UGAIDI?
Mzee Freeman Mbowe umesahau haraka. Kuna watu walifungwa gerezani, wengine sasa ni walemavu, wengine sasa ni marehemu kwa sababu ya kupigania jina lako ukiwa kiongozi wa chama chetu.
Umesahau, wakati unakamatwa na Serikali katili ya CCM, 2021, wanachama wa CHADEMA walikwenda kuonyesha ‘solidarity’ na wewe pale KISUTU. Walikamatwa, wakashtakiwa, wakafungwa
Najutia zile siku nilisimama nawe, kukutetea na kunadi jina lako kwa nia njema kabisa nikifikiri unapambania uhuru, haki na mabadiliko ya kweli. Haikuwa hivyo. Ulitudanganya tukishindwa.
Nasema kwa kuwa kwa hiari yangu, niliamua kusimama nawe, kukunadi katika mazingira ambayo ilionekana ni kama kuuza kitimoto Mecca. Lakini sikutarajia tukishindwa, tuisaliti CHADEMA
Wengine sasa tumeelewa kwa kuchelewa sana. Hii chuki haiwezi kuwa ya kushindwa uchaguzi. Lazima kuna mafekeche mengine. Kuna kingine kimeujaza chuki moyo wako. Je, kuna mrija, umekatwa?
Najutia kumpa mtoto wangu jina lako, Freeman.
Leo tarehe 26 Julai 2026 mimi PETER MADELEKA natangaza rasmi KUACHANA NA SIASA ZA ACT WAZALENDO.Nafanya hivyo ili nipate MUDA WA KUTOSHA kuungana na WAPENDA HAKI wote katika KUPIGANIA HAKI na USTAWI wa nchi yetu.Tanzania yenye HAKI Inawezekana kama kila mtu ATATIMIZA WAJIBU WAKE.
WANAOSEMA KUWA KWA SABABU SHAURI LA MHESHIMIWA LISSU LIKO MAHAKAMANI, HAKUNA ANAYEPASWA KUMSHAURI Mhe RAIS ALITAFUTIE UFUMBUZI WANAKOSEA. Hapa inabidi tuelimishane zaidi na kwa uwazi. Tusichanganye dhana mbili tofauti: uhuru wa Mahakama na wajibu wa Serikali.
Mahakama zina wajibu wa kutoa maamuzi kwa uhuru, bila kuingiliwa na mtu yeyote hata Rais. Huo ni msingi wa utawala wa sheria na lazima uheshimiwe.
LAKINI NI SERIKALI KUPITIA VYOMBO VYAKE NDIYO HUANZISHA NA KUENDESHA MASHITAKA YA JINAI. Katika nchi nyingi zinazofuata mfumo wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth), mamlaka ya mashtaka yanaweza kupitia upya uamuzi wa kuendelea na shauri pale yanapoona kuwa maslahi ya umma au haki yanahitaji hivyo. Kwa hiyo, kumshauri mhe Rais ahimize Serikali yake kupitia upya uamuzi wa kuendelea na mashitaka ya jinai ambayo yanachukua muda mrefu au kuleta sintofahamu katika taifa si sawa na kuiamuru Mahakama iamue kwa namna fulani. Kusema vinginevyo ni kupotosha umma. Kuna wanaofanya hivyo kwa kutokujua. Kuna wanaofanya hivyo kwa hila ovu kama propaganda tu ya upotoshaji. Tusichoke kuelimishana.
Hata taarifa ya hivi karibuni ya Commonwealth Ministerial Action Group (CMAG) haikuitaka Mahakama imwachie huru Mheshimiwa Lissu. Badala yake, ilishauri suala hilo "lipatiwe ufumbuzi kupitia njia za kisiasa na kisheria." Hii inaonyesha kwamba hata katika demokrasia zilizoimarika, KUNA WAKATI SULUHISHO LA MIGOGORO YA KISIASA HUPATIKANA KWA KUTUMIA TARATIBU HALALI ZA KISHERIA PAMOJA NA BUSARA ZA KISIASA. Mimi ninaamini athari za kuendelea kumshikilia Kiongozi mkuu wa chama cha upinzani kwa shitaka ambalo kwa mwaka mzima sasa halijakamilika mahakamani haisaidii taifa hili hata kidogo.
Mhe Makamu Mwenyekiti wa CCM Stephen Wassira (MTANI) kweli tulidiscuss. Kwa kuwa umeweka wazi maongezi yetu basi uniruhusu na mimi niongezee ufafanuzi for the record. Kwanza “tulikubaliana kutokubaliana”. Rai yangu kwa mhe Rais siyo shinikizo kwake wala kuingilia Mahakama. Silazimishi chochote kwani ninajua sina mamlaka hayo. Ni ushauri na ombi kwa uongozi wa Taifa kwa ujumla wake kwamba swala la Lissu na wengine wa aina hiyo likamilike. Serikali ndiyo inashitaki huko Mahakamani. Ikiondoa shauri, kama ilivyofanya mara nyingi huko nyuma kwa busara, tutapiga hatua ya mengine yanayotusubiri kuponya majeraha kwa kutenda haki, kuridhiana na kuweza kuandika Katiba Mpya katika hali ya kuaminiana. Mamlaka ya kuondoa shauri mahakamani iko chini ya mhe Rais na Serikali yake kupitia ofisi ya DPP. Ni kwa kutambua hilo ninajielekeza moja kwa moja kwa Mhe Rais. Na ninaendelea kufanya hivyo kwa unyenyekevu mkubwa. The stakes my MTANI are too high. The difference is that some can see the danger, others cannot. The burden of knowledge.
I hope unatafuta engagement tu kwenye hili na sio serious question… 🤦🏾♂️
Mkuu wa Mkoa alitaka nini kutaka kupewa platform kwenye Bongoflava Honors ya Prof Jay?
Kwenye Simba Day na Yanga Day, wanafataga nini?
Serikali iliyokosa legitimacy, hadi Rais (haramu) anaenda kumuona Pacome hospitali for publicity, kweli unaweza kujiuliza WANATAKA NINI?! really…
100%. Hatuwezi kusapoti Chadema kwa maneno tu, lazma tutoe pesa.
Ngoja niwaambie kitu Watanzania, Chadema kukosa pesa ndio moja ya sababu kuu CCM wanawapata watu wa kufanya hizi press za kumchafua Heche.
Watanzania, hatutafika popote kama Chadema haina pesa .
Ni aibu kubwa sana nchi inayolilia haki leo ni siku ya 3 tumekusanya 50 million tu, ni aibu. Mtu ananunua bando ili aingie insta asome umbea wa nani kaachana na nani? Hizo buku 5 za bando la kufatilia umbea si ungetuma Chadema?
Reality is bila Chadema kuwa na pesa hakuna msaada mkubwa wataweza kutupa…….. Watu wanatupigania ila hata kuwasapoti na kufanikisha kazi zao kwa kutoa pesa tunashindwa??? Hii haki tunayoidai itakuja kimiujiza bila pesa kuwepo za kufanya movement ????
Kama unakubaliana na nilichosema basi, kabla huja Like hii posti, kabla hujareposti, kabla huja comment kabla hujamforwadia mtu hii link tuma pesa kwenye hii number.
vodacom: 0744 446969
Jina: Chadema HQ
Kingine nna swali kwa Chadema hawa wanachama wenu mamilioni, mna namba zao simu? Yani mna database ya wanachama. Je mnatuma messages kwa wanachama kuwakumbusha kuchangia? Mimi personally hapa Marekani huwa nasumbuliwa na message za chama mpaka natuma mwenyewe pesa. Maana message inakuja na link kabisa ya kutuma pesa, tena wanani address kwa jina.
Kwa wafuasi wote wa CHADEMA na mageuzi, wapenda haki, ukweli na demokrasia nchini.
Baada ya Katibu Mkuu wetu, John Mnyika, kutangaza maazimio ya Chama chetu, ikiwa ni pamoja na kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika siku sio nyingi , vilevile alizindua mpango maalumu wa uchangiaji wa fedha kupitia Tone Tone.
Kwa siku kadhaa sasa, kampeni hii imeendelea kwa nguvu kubwa mitandaoni, ikibebwa na viongozi wetu, wanachama, wananchi pamoja na wana harakati mbalimbali. Nawashukuru kwa dhati kabisa wote mlioamua kubeba jukumu hili; kuanzia anayehamasisha michango hadi anayetoa mchango wake. Kila mmoja wenu ni sehemu ya historia inayoandikwa.
Hata hivyo, pamoja na shukrani hizi, kuna ukweli ambao hatupaswi kuogopa kuusema. Wakati mwingine ukweli huwa ni sehemu muhimu ya kujitathmini kama taasisi na kama watu wenye maono ya pamoja.
CHADEMA ni Chama chenye wafuasi wengi kuliko Chama chochote cha siasa nchini. Wakati wa operesheni ya CHADEMA ni Msingi tulikuwa na kanzidata ya wanachama zaidi ya milioni saba. Kwa tafiti na tathmini zetu za sasa, si jambo la kupindukia kusema kuwa wapenzi wa demokrasia, haki na mabadiliko nchini wanafikia au hata kuzidi asilimia 65 ya Watanzania wazima. Kama tunakubaliana na ukweli huo, basi ni lazima tukubaliane pia na wajibu unaoambatana nao.
CHADEMA haipaswi kuwa na upungufu wa fedha za kuendesha shughuli zake. Kama watu milioni moja tu wataamua kuchanga shilingi 1,000 kila mwezi, Chama chetu kitakuwa kinapata zaidi ya shilingi bilioni moja kila mwezi. Katika kampeni hii ya kuhakikisha kikao cha Baraza Kuu kinafanyika, watu laki tano pekee wakichanga shilingi 2,000 kila mmoja, tayari watakuwa wamechangia takribani shilingi bilioni moja kwa Chama chao.
Hii ina maana kuwa changamoto yetu siyo idadi ya watu, bali ni kiwango cha dhamira yetu (commitment) katika kuwekeza kwenye kile tunachokiamini. Ni lazima tujifunze kwamba mapambano ya demokrasia yana gharama zake. Haki ina gharama yake. Mageuzi yana gharama yake. Hakuna taasisi inayoweza kuwa huru kama utegemezi wake unatoka mahali pengine isipokuwa kwa watu wake wenyewe. Vyama vikubwa vya siasa duniani vimejengwa kwa michango midogo lakini ya kudumu kutoka kwa wananchi wanaoviamini. Nasi tunapaswa kujenga utamaduni huo.
Tusifanye uchangiaji kuwa jambo la misimu au la kusubiri vikao maalumu. Uchaguzi wa mwaka 2025 ulipita na Chama chetu hakikushiriki. Hivyo, hatuna ruzuku tunayoitegemea. Tunachokitegemea ni imani, mshikamano na mchango wa wananchi wenyewe. Huo ndio mtaji mkubwa wa CHADEMA.
Ni jambo lisilo na mantiki kusema tuna mamilioni ya wafuasi huku tukishindwa kukusanya fedha za kuendesha shughuli zetu za msingi. Tukitaka kuwa Chama kikubwa, imara na huru, ni lazima tukubali kubeba gharama za ukubwa huo. Tusitarajie wachache wabebe jukumu ambalo mamilioni yetu yanaweza kulifanya kwa wepesi kabisa.
Ni rai yangu kwa kila mwanachama, mfuasi na mpenda mageuzi popote alipo, afanye jukumu hili kuwa sehemu ya maisha yake ya kisiasa. Elfu moja yako inaweza kuonekana ni ndogo, lakini inapoungana na elfu moja za wengine, hujenga taasisi kubwa. Michango yetu midogo ndiyo itakayolinda uhuru wa maamuzi yetu na uimara wa Chama chetu.
Tusichangie kwa sababu tunaombwa kuchangia. Tuchangie kwa sababu tunaamini katika Tanzania yenye haki, demokrasia na utawala wa sheria. Tuchangie kwa sababu tunaamini kuwa mageuzi tunayoyatamani hayawezi kujengwa kwa maneno pekee, bali kwa kujitoa kwetu kwa vitendo.
Your small donation can make a very big change.
Nawashukuru sana kwa upendo wenu, mshikamano wenu na imani yenu katika mapambano haya. Historia ya mageuzi huandikwa na watu wanaoamua kufanya zaidi ya kushangilia. Naamini tutafanya zaidi ya tuliyoyafanya jana.
Mungu akubariki , asanteni kwa wale wote mliochanga na mnaoendelea kuchanga na ni wito wangu kwa kila mtu kujali kwa vitendo jukumu hili muhimu , tena sio mara moja bali kila wakati.
Kwasasa mjadala ni watu kuichangia CHADEMA BRO (TUPO NJE YA MUDA).
Mimi nimeapa mbele ya watanzania kuwa lazima tufikie LENGO la kupata MILIONI 340.
Nilifungulia kampeni hii kwa kuchangia 1M na sasa tuna 50M ndani ya masaa 96.
Tukifikisha 100M—nitachangia tena 2M kuanzisha safari ya kuisaka 200M.
Tukifikisha 200M—Nitachangia tena 3M kuanzisha safari ya kuisaka 340M.
Bro inawezekana hii—kama ulichangia jana fanya tena jua hatujamaliza. Kila mtu aweke nadhiri yake kwenye kukamilisha hili tunaweza wanangu.
REPOST 200.
Tuma mchango wako sasa.
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
Habari niliyopewa usiku huu ni nzito sana.
Watanzania naomba mnisikilize, Heche is a DEAD MAN WALKING….
Huu mpango wa kumuondoa kama kiongozi wa Chadema kupitia kumchafua kuwa kaiba pesa za tone tone ukishindwa kumuondoa CCM watamuua ili waweze kuweka mtu ambae ataipeleka Chadema kwenye maridhiano na kimama.
Yani ni hivi, kimama anataka maridhiano na Chadema at any cost . Yani lazma yafanyike, wamemwaga pesa ndani ya Chadema kama zote ili Heche aondolewe Chadema waweze kuweka mtu wao. Unaambiwa kampeni ya kumchafua Heche ni kubwa na ndo kwanza imeanza, mnaambiwa mpaka kwenye kamati kuu ya chama wanamwaga hela ili aondolewe.
Sasa ikishindikana hiyo plan ya kumuondoa kwa kumchafua kimama yuko tayari kwenda kwenye plan B, to kill him…..
ile ticket and info alioposti Yericko sio Ai au edit it’s real. Kapewa na usalama wa taifa, although Heche hakusafiri. Ila hali ni mbaya kiasi hiko. Mombo anamstalk Heche kila anapoenda anasubiri go head ya kimama then amuue Heche.
Watanzania Heche na Lissu ndio watu wamwisho tulionao wenye msimamo mkali, tumlinde Heche kwa njia yoyote, yani hata ikibidi tupeane zamu kulala nje ya geti lake, au hata tuchange tulipie international security group waje kumlinda other wise HE IS DEAD…
BREAKING: VIDEO MPYA. NEW VIDEO EVIDENCE OF THE VIOLENCE THAT TANZANIANS ENDURED DURING THE INTERNET BLACKOUT UNDER SAMIA SULUHU ORDERS.
WATANZANIA AMBAO MLIKUWA MNAOGOPA KUACHIA VIDEO, PLEASE NITUMIENI ILI DUNIA IONE ILI TUPATE MSAADE WA NJE!!!!! WhatsApp +1 424 537 3057
Taarifa: Ili kumuunga mkono Mwenyekiti wetu Lissu na struggles zake gerezani, nimeamua kumuiga style yake mpya ya nywele…Sitachana wala kunyoa nywele zangu mpaka atoke jela akiwa HURU✌🏾✌🏾
#LiMwenyekiti#KatibaMpya#FREELISSU
“Msimamo wa mwanadamu haupaswi kuwa gereza la dhamira yake.
Kuna nyakati ambapo ukimya huwa mzigo kuliko maneno.
Sidai kuwa mimi ni mkamilifu, lakini nimeamua kutii dhamira yangu kuliko kuigiza consistency isiyo na ukweli. Si busara kushinikizwa kuonyesha “uanaume wa kisiasa” kwa kubaki sehemu ambayo dhamira yako haiwezi tena kutulia”
Natoa pole nyingi sana kwa Msaidizi wa Mheshimiwa Tundu Lissu, Ndugu Jumbe, kufuatia tukio baya na la kinyama lililomtokea. Huu si utamaduni wa Watanzania, wala si maadili yanayopaswa kupewa nafasi katika jamii yetu.
Tofauti za kisiasa zisigeuke sababu ya chuki, vitisho, au mashambulizi dhidi ya watu. Taifa lenye afya ya kisiasa hujengwa juu ya ushindani wa hoja, heshima ya utu wa binadamu, na kulinda haki ya kila mtu kuwa salama bila kujali itikadi yake.
Wananchi, wakati umefika wa sisi sote kupaza sauti na kukemea matukio ya aina hii bila kujali tofauti zetu za kisiasa. Ukimya mbele ya uovu unaweza kuupa nguvu uovu wenyewe.
Namtakia Ndugu Jumbe uponaji wa haraka na nguvu katika kipindi hiki kigumu. Pia naomba vyombo husika vifanye uchunguzi wa haraka, wa haki, na wa uwazi ili wote waliohusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.