MBOGAMBOGA, mmechanganyikiwa!
Tumeona propaganda zinazoenezwa na mwenezi wenu zikituhumu CHADEMA kupanga maandamano na vurugu. Huu ni uongo mtupu. Hakuna kikao chochote kilichofanyika kupanga jambo hilo. siku tukiamua kufanya hivyo, tutaweka wazi kwa umma bila kificho kwa sababu maandamano si jinai. Tunaelewa, huu ni mkakati wa kutengeneza visingizio ili kukamata, kuteka, na kupoteza vijana wetu kutokana na hofu mliyonayo baada ya kuona nguvu ya CHADEMA mtaani. Mnaogopa maandamano? Tangu lini ni haramu? Badala ya kuzuia haki za kiraia kwa nguvu, shughulikieni changamoto zinazowakabili wananchi. Sikiliza; you can’t heal diarrhea by stitching the anus. #freetundulissu #tundulissusiomhaini
Mkutano Mkuu Maalum BAWACHA Wilaya ya Ukonga Mkoa wa Ilala
Kukagua UHAI wa BAWACHA na Chama kwa ujumla
Na Maandalizi Oparesheni #KATIBAMPYA#FREETUNDULISSU
inayotarajiwa kuanza wakati wowote Kanda ya Pwani
WANAWAKE
CHIMBUKO LA MAENDELEO
#NOJUSTICENOPEACE#STRONGERTOGETHER
Mkutano Mkuu MaalumBAWACHA Wilaya ya Kibamba Mkoa wa Ubungo
Kukagua UHAI wa BAWACHA na Chama kwa ujumla
Maandalizi Oparesheni #KATIBAMPYA#FREETUNDULISSU
inayotarajiwa kuanza wakati wowote Kanda ya Pwani
WANAWAKE
CHIMBUKO LA MAENDELEO
#NOJUSTICENOPEACE#STRONGERTOGETHER
KWAKUWA NI HALALI KWA WAZANZIBARI KULINDA HAKI ZA WAZANZIBARI HAIWEZI KUWA HARAMU KWA WATANGANYIKA KULINDA HAKI ZA WATANGANYIKA.
Kwa yanayoendelea kujitokeza katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusu kujitanabaisha kwa misingi ya Uzanzibari na kulinda maslahi ya Zanzibar, je, si wakati sasa kwa Watanganyika nao kuzungumza kwa uwazi, kuhoji kwa uhalali na kujadili kwa kina masuala yanayohusu haki, hadhi na maslahi ya Tanganyika?
Je, Watanganyika hawana haki ya kuhoji na kulinda:
1. Bandari zilizopo ndani ya Tanganyika.
2. Misitu na rasilimali za mazingira za Tanganyika.
3. Rasilimali za asili zilizopo katika eneo la Tanganyika.
4. Hadhi, haki na umiliki wa ardhi ya Tanganyika.
5. Nafasi, haki na uwepo wa watu wasio Watanganyika katika idara na taasisi ambazo si za Muungano.
6. Uhalali wa viongozi wasio Watanganyika kuingia au kusaini mikataba inayohusu rasilimali za Tanganyika, hususan pale ambapo baadhi ya masuala hayo tayari yameondolewa katika eneo la Muungano kwa upande wa Zanzibar.
7.Kuhoji mchango wa Zanzibar katika kugharimia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano na Ulipwaji wa Deni la Taifa.
Ikiwa ni halali kwa Wazanzibari kujadili, kuhoji na kulinda maslahi ya Zanzibar kwa misingi ya utambulisho wao wa kisiasa na kikatiba, kwa mantiki hiyo hiyo haipaswi kuwa kosa kwa Watanganyika kuhoji, kujadili na kutetea maslahi ya Tanganyika.
Katika mfumo wowote wa haki, usawa na kuheshimiana ndani ya Muungano, haki ya kulinda maslahi ya Zanzibar haiwezi kutenganishwa na haki ya Watanganyika kulinda maslahi ya Tanganyika.
Haki hizo zinapaswa kutambuliwa kwa usawa, bila upendeleo na bila kuonekana kuwa ni tishio kwa Muungano, bali kama sehemu ya kujenga Muungano wenye misingi ya haki, uwazi na kuheshimiana.
UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI ndiyo Msingi bora wa kuliongoza Taifa kutoka katika vitendo vya Ukatili dhidi ya ubinadamu,ukiukwaji wa Haki za Raia na,Mauwaji na Utekaji vilivyofanyika kanla,wakati na Baada ya Tarehe 29 Oktoba 2026.
BAK MWABUKUSI.
Mafunzo kwa wajumbe Kamati Tendaji BAWACHA Taifa yanachoendelea leo tarehe 29/05/2026 Mkoa wa Dodoma
#FREETUNDULISUNOW#KATIBAMPYANISASA
$NOJUSTICENOPEACE
#STRONGERTOGETHER
WANAWAKEEEEE
CHIMBUKO LA MAENDELEO
M/Mwenyeki Mh @HecheJohn na Katibu Mkuu Mh @jjmnyika pamoja na viongozi na wanachama wengine wameshiriki ibada ya mazishi ya Dr. Mtungi aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA. Ibada hiyo imefanyika leo Kanisa R.C Parokia ya Mt. Maximilian Maria Koble iliyopo Mwenge Dar
Hii ni leo Kirando, Nkasi Kaskazini, Rukwa. Hakuna kiongozi wa kitaifa yeyote. Hapa alikuwepo AIDA KENANI na watu wake tu. Mnaweza kuwatoa roho wafuasi wote wa CHADEMA lakini hamuwezi kuondoa imani kwa watu. Kwa sasa, CHADEMA ni imani ya watu. CHADEMA kwetu ni lifestyle yetu.
Kuta za Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Rukwa zimeanza kutikisika kufuatia uamuzi wa kundi la wanachama wa chama hicho kujiengua na kujiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Wanachama hao wameamua kukabidhi kadi zao leo, Aprili 26, 2026, wakidai kutafuta mwelekeo mpya wa kisiasa wenye tija kwa
wananchi wa mkoa huo.
Tukio hilo limejiri katika Kata ya Kirando, Jimbo la Nkasi Kaskazini, ambapo Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Rukwa na Mbunge Mstaafu wa jimbo hilo, Aida Khenani, amewapokea na kuwakabidhi kadi za uanachama. Mapokezi hayo yamefanyika wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) kilicholenga kupanga mikakati ya uimarishaji wa chama mkoani humo.
Aida Khenani, akiwa ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA Kanda ya Nyasa, Paulina Mwaitalako, amesema kuwa kuingia kwa wanachama hao ni ishara ya ukomavu wa kisiasa na uchovu wa wananchi dhidi ya mfumo wa sasa.
“Leo tunawapokea ndugu zetu hawa walioamua kujiunga na jeshi la ukombozi. Hii ni thibitisho kuwa kule tunakokwenda ni kuzuri zaidi. Nkasi Kaskazini tunaanzia tulipoishia, na sasa jeshi letu limeimarika zaidi.
Waambieni majirani tukutane mzigoni,” amesema Aida Khenani huku akipigiwa vigelegele na wanachama.
Wanachama hao wapya wameeleza kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na kuvutiwa na misimamo ya CHADEMA katika kutetea rasilimali za nchi na haki za wananchi wanyonge.
Viongozi wa BAWACHA mkoani Rukwa wamesisitiza kuwa kuongezeka kwa wanachama hao ni chachu ya kuendeleza harakati za kura na maendeleo, huku wakiahidi kuendelea kugusa maisha ya wananchi kuanzia ngazi ya msingi ili kuhakikisha chama kinashika hatamu katika maeneo mengi zaidi mkoani humo.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amesema siasa zinapaswa kujengwa kwa hoja badala ya matumizi ya lugha chafu au matusi.
Akizungumza kufuatia malalamiko ya Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, kuhusu kusambazwa kwa namba yake ya simu na kupokea ujumbe wa matusi pamoja na kejeli, Heche amesema hakubaliani na tabia hiyo licha ya kuwepo kwa tofauti za kisiasa.
Heche alieleza kuwa katika maisha yake yote ya kisiasa, amekuwa akiamini katika demokrasia ya hoja, akisisitiza kuwa hajawahi kutumia matusi bali hujenga hoja zenye nguvu na kueleza ukweli bila upendeleo.
“Ninachosisitiza ni kwamba watu wanapaswa kutofautiana kwa hoja, si kwa matusi. Mimi husema ukweli kama ulivyo; kama ni nyeusi, nasema ni nyeusi,” amesema Heche.
#MillardAyoUPDATES
Kikao cha ndani cha Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Mkoa wa Rukwa kilichofanyika leo Aprili 26, 2026 katika Kata ya Kirando, Nkasi Kaskazini, kikiongozwa na Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Rukwa Aida Khenani.
ZABURI 1:1
Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
#TUMSIFU YESU CHRISTO
TEC hawajapeleka kabisa mwakilishi Wamekataa kuketi,
kusomewa uongo Kanisa moja,
Takatifu, Katoliki la Mitume Ni moja jana, leo, asili yake ni Yesu Kristo Ibada moja,
sheria moja ,
mapokeo yaleyale Kanisa limeenea pande zote ulimwengu mzima Kanisa Katoliki,TUNAJIVUNIA