Kesi ya MH LISSU kwa nilivyoelekezwa jana tupo PAZURI na natumia lugha nyepesi kukuelewesha na wewe ambae huelewi nini kinaendelea.
MPAKA SASA ni “NO CASE TO ANSWER” Jamuhuri wamemaliza kuleta Mashahidi wao (17) kuionyesha MAHAKAMA kuwa Lissu ni MUHAINI anatakiwa KUNYONGWA.
Kwa mwenendo mzima wa kesi na jinsi alivyoshughulika na MASHAHIDI FEKI WA JAMUHURI MH amesema kuwa “NO CASE TO ANSWER” kwamba “HAKUNA UHAINI HAPA”.
Sasa MAJAJI WA MAHAKAMA wanaenda kupitia ushahidi wa JAMUHURI na kisha 21/08 wanakuja kusema je MH LISSU “ANAYO KESI YA KUJIBU” au “HANA KESI YA KUJIBU”.
Ikiwa HANA KESI YA KUJIBU, basi anakuwa HURU hiyo 21/08.
Ikiwa MAJAJI wakaona ANAYO KESI YA KUJIBU basi nae MH LISSU atatakiwa kuanza kujitetea.
HAPO SASA NDIO PATAMU.
MH LISSU atatakiwa kuita mashahidi wake. Kumbuka alishatoa LIST YA MASHAHIDI WAKE kama mnakumbuka jina la kwanza la SHAHIDI WAKE NI SAMIA SULUHU HASSAN.
Kwahiyo akikutwa na KESI YA KUJIBU ataanza kuwaita mashahidi wake AKIANZA NA SAMIA kama ambavyo MKAPA alivyowahi kuitwa mahakamani kipindi chake cha URAISI huyu nae ataitwa na MAHAKAMA.
KWAHIYO kiuhalisia TUMEFIKA MWISHO, tukutane 21/08 kumkaribisha tena uraiani mweshimiwa RAISI WETU WAPENDA HAKI.
Na hii AMESHINDA MAHAKAMANI hatutaki kuanza kutuletea story za kwamba katoka kwa huruma za MTU, Nyie mlipanga KUMNYONGA huo ukweli utalindwa kwa wivu mkubwa sana.
Tuendelee kumuombea MH WETU WAKUU.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎