NIMJUAVYO mimi Mnyika, ukimuona mtu anatuhumiwa kutafuna fedha ndani ya Chadema, ikiwamo kuingiza madeni hewa, halafu yeye akagoma kumtetea, basi fahamu haraka kwamba tuhuma hizo ni za kweli. Msihangaike kutafuta mchawi.
Ninakipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar kwa kufanya mazungumzo na kufikia maridhiano. Hii ni hatua muhimu inayozidi kuimarisha amani, umoja, utulivu na mshikamano miongoni mwa Watanzania. Maridhiano si ishara ya udhaifu bali ni alama ya ukomavu wa kisiasa unaoweka mbele maslahi ya Taifa badala ya maslahi ya vyama au ya mtu binafsi.
Wananchi hawahitaji vurugu wala mivutano ya kisiasa isiyoisha. Wanahitaji amani, usalama, huduma bora za kijamii, ukuaji wa fursa za kiuchumi na ajira. Ili kufanikisha hayo, serikali itaendelea kusimama imara katika kulinda usalama wa raia na mali zao, pamoja na kudumisha heshima na hadhi ya nchi yetu.
Kwa pamoja, tutafakari umuhimu wa maridhiano kama yanavyohimizwa pia katika vitabu vitakatifu:
Qur'ani Tukufu Sura Al-Hujurat 10: "Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu; basi patanisheni baina ya ndugu zenu na mcheni Mwenyezi Mungu, (msipuuze jambo la kupatanisha) ili mrehemewe."
Biblia Takatifu – Mathayo 5:9: "Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu."
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Sheikh Rashid Hamad Othman, Mlezi wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Mhe. Othman Masoud Othman, anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam. Akiwa hospitalini hapo Mhe. Rais Dkt. Samia pia alijulishwa kuhusu kuwepo kwa Mchezaji wa Timu ya Yanga Pacome Zouzoua katika chumba jirani, ambapo alipata muda wa kumtembelea na kumpa pole kufuatia majeraha aliyopata katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo hivi karibuni.
Mwaka huu Tanzania inaadhimisha miaka 50 ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba). Kwa upekee, maonesho ya mwaka huu yamefunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Daniel Francisco Chapo, jambo linaloonyesha uhusiano imara kati ya nchi zetu na hadhi ya kimataifa ya maonesho haya.
Kwa miaka 50, Sabasaba imeendelea kuwa jukwaa muhimu la biashara, uwekezaji na ubunifu, likipanua masoko, kuvutia uwekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi. Maonesho haya, yamechangia fursa za biashara zenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 129 na kutoa ajira zaidi ya 624,380.
Serikali itaendelea kuyatangaza maonesho haya kimataifa ili yaendelee kuwa daraja madhubuti linalounganisha sekta za uzalishaji na masoko, kutangaza bidhaa zetu na kuvutia fursa zaidi za uwekezaji nchini.
Ninaipongeza Klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo. Mafanikio haya ni ushahidi wa juhudi, nidhamu na kujituma kwa wachezaji, benchi la ufundi, uongozi pamoja na mashabiki.
Aidha, ninazipongeza klabu zote zilizoshiriki Ligi Kuu msimu huu kwa ushindani mzuri uliofanya mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania kuendelea kukua, kuvutia na kuongeza hamasa kwa mashabiki pamoja na wadau wa mchezo huu.
Mwaka 2025 nikipokea gawio na michango kutoka taasisi na mashirika ya umma nilitoa maelekezo ya uboreshaji zaidi. Nina furaha kuona maelekezo hayo yamefanyiwa kazi, na gawio la serikali mwaka 2026 limeongezeka kwa asilimia 30, kufikia shilingi trilioni 1.32. Siku ya Gawio si siku ya kusherehekea mafanikio ya kifedha pekee, bali ni fursa ya kutathmini maeneo yanayohitaji uboreshaji zaidi ili mafanikio tuliyoyapata yaendelee.
Mafanikio hayo ni uthibitisho kuwa, taasisi na mashirika ya umma yanaweza kutoa huduma na kuwa sehemu ya ujenzi wa uchumi wa taifa letu. Tunapoelekea kuanza utekelezaji Dira ya Taifa 2050, ni muhimu tufahamu kuwa hatutaweza kujenga uchumi shindani kwa taasisi zinazofanya kazi kwa mazoea, ni lazima tujipime kwa matokeo, na si takwimu. Haya ndiyo maono na mwelekeo wa taifa letu.
Pamoja na hayo, ninazipongeza taasisi na mashirika yote yaliyotoa gawio kwani hii ni sehemu ya lengo letu la kuongeza mapato ya ndani katika kugharamia shughuli za maendeleo. Hata hivyo, pongezi hizi zisiwe sababu ya kuridhika na kubweteka, kwani hatutasita kuchukua hatua tunapobaini uzembe na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.
"Hatushtuki... lakini tunasikitika!" 😂
Kauli ya Chadema mchana dhidi ya CCM, lakini usiku wanaharakati wao wanatupa ramani kamili ya jinsi wanavyotaka kufunga shule za msingi na sekondari. Hivi mnapanga mapinduzi au mnasaka kiki ya kisiasa? Shika adabu yenu!
@HildaNewton21@Gibson44178359 Hii ndio shida ukiwa mwanaharakati alafu huna chanzo cha kipato, unategemea ufadhili wa Nje. unakua huna nzuri lolote kwa nchi yako
Ninawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Eid Al Adha. Tusherehekee kwa moyo wa amani na upendo, huku tukiwakumbuka ndugu zetu wenye uhitaji, na kuendelea kudumisha utu na ukarimu katika jamii.
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema apokee dua na sadaka zetu na aendelee kulibariki Taifa letu.
Eid Al Adha Mubarak.
Leo, Ikulu jijini Dar es Salaam, nimempokea Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame, aliyewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Tanzania na Rwanda si tu ndugu na majirani, bali pia ni washirika wa kimkakati wenye uhusiano unaoendelea kukua kwa kasi. Takribani asilimia 70 ya shehena ya Rwanda inapitia katika bandari za Tanzania. Biashara kati ya nchi zetu mbili imefikia shilingi bilioni 644 mwaka 2025, na uwekezaji kutoka pande zote mbili unaendelea kuchochea ajira na ukuaji wa uchumi kwa wananchi wetu.
Katika mazungumzo yetu, tumekubaliana kuongeza kasi ya ushirikiano kwa kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi, kuimarisha biashara na uwekezaji, na kuwekeza zaidi katika miundombinu ya usafiri na usafirishaji, mawasiliano, pamoja na nishati ya uhakika. Aidha, tutaimarisha ushirikiano katika masuala ya ulinzi, usalama na ajenda za kikanda na kimataifa.
Karibu tena Tanzania, Mheshimiwa Rais.
@zittokabwe@NgomeyaVijana Kweli 73% ni Vijana lakini Kusema CCM Imechoka ni sawa na kufumba macho alafu useme husikii! Benki ya Vijana si jengo, ni mfumo. Na mfumo huo CCM inaujenga kwa sera, sio ahadi. CCM inatambua Vijana ndio wengi na Kuna uhitaji mkubwa wa kuwezeshwa kiuchumi.
Nawatakia Watanzania wote Pasaka njema, yenye furaha na baraka tele. Tunapoadhimisha ufufuko wa Bwana Yesu Kristo, tuyakumbuke na kuyaenzi mafundisho na matendo yake ya huruma, upendo, msamaha na kujitoa kwa ajili ya wengine.
Pasaka hii itukumbushe umuhimu wa kudumisha amani, kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa, ili tuendelee kujenga Taifa lenye fursa kwa wote, ustawi na maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Heri ya Sikukuu ya Pasaka!
#TaifaKwanza#KataaVurugu
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndani ya siku 100 amezindua Bima ya Afya kwa wote kwa ajili ya wananchi wote kumudu gharama za afya nchini. Tumuunge mkono. Rais wetu Anaweza na Anasonga mbele. Tuwakatae Wanaharakati Uchwara.
#HakiNaWajibu
Karibu Tanzania Mheshimiwa Rais.
Ikulu, Dar es Salaam leo nimempokea Kaka yangu, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni. Ziara yake hii nchini ikiwa ni siku chache tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Uganda inaonesha namna Uganda inavyothamini ushirikiano wake na nchi yetu, ambao umejengwa katika misingi ya udugu, ujirani na kuheshimiana.
Tumejadili maendeleo ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Mradi huu ambao ni moja ya vielelezo vya uhusiano wetu, unatarajiwa kuanza kufanya kazi Julai mwaka huu. Vilevile, tumejadili mpango wa kuunganisha reli (SGR), ujenzi wa mabomba ya kusafirisha gesi asilia na mafuta, kukuza matumizi ya bandari za Tanzania, ulinzi na usalama, pamoja na namna bora ya kukuza biashara baina ya nchi zetu kwa kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi.
Mambo kadhaa wanaharakati wanaweza jifunza sasa;
1. Mitaani kila mtu ni balozi wa mwenzie kuhusu amani kwa sasa. What happened 29 October ni nightmare ambayo kila mtu anasema that should NEVER EVER HAPPEN AGAIN
2. Elimu kwamba watu hulipwa billions of money kufanya harakati against the state, kwamba wanakaa sehemu kwenye viyoyozi nje ya Nchi, full protected na kwao kila number ya casualties means HELA imefika hadi kwa watu ambao maybe hawakuwahi kufahamu hizi patterns
3. Mitaani watu wanataka their casual unapologetic life, bila sababu wala haja ya kuwa tokens za kifedha za kundi dogo la watu covered katika jina la harakati. Na what happened on 29 October gave them back a sense ya kuheshimu “maisha ya kitanzania”
4. Mngeshauriwa sawa sawa, mnge stick na outcomes za 29 October ku push narratives zenu maana zilikua zinabeba credibility kwa upande wenu ila kwa sababu ya tamaa na haraka mka jump into a fool/shaddy 09 December plans na leo D25 ambazo kwa vyovyote vile zimewapa matokea ya aibu na ziada ya;
a) Kuwalazimisha kutumia uongo ili ku justify UONGO (ikiwemo kupost picha/video fakes)
b) Uongo ambao pia unatoa justifications 3 muhumu sana;
-Ninyi ni waongo na si wa kuaminika kwa lolote
-Ninyi ni wanufaika wa machafuko Tanzania na ndo sababu mpo tayari kwa lolote hata kuongopa ili ku justify baadhi ya mambo
-Huenda hata numbers/data mnazosema kuhusu Oktoba 29 ziko fabricated kwa sababu una nia ovu fulani.
As of the latest briefings, Tanzania ni salama, maandamano ya kubumba mlotaka ili ku justify some of your payments yamefeli, yamepuuzwa, na yanefungua ukurasa mpya wa namna watu wetu wanawatazama, wanawaskiiza, wanafikiri kuwahusu.