Hakikisha kila muda unawaza kua MWEMA mbele ya watu na MUNGU, Usisubiri kua ipo siku utabadilika na si sasa maana KESHO yako ni FUMBO. MUNGU ana mipango yake๐
The U.S. embassy in Tanzania will be closed on Friday, July 4, in observance of ๐บ๐ธ Independence Day. We will resume regular operations on Monday, July 7.
CHOZI LA POGBA AKISAINI MKATABA NA KUMBUKUMBU MBAYA ZA KUTEKWA KISA NDUGU, PAMOJA NA ADHABU YA KUFUNGIWA.
Anakabidhiwa karatasi za Mkataba kusaini ili aitumikie As Monaco msimu ujao, ghafla hisia kali zinamjaa moyoni, mtu mzima anaangusha chozi. Kila mtu anashikwa na butwaa anajiuliza inakuaje Paul Labile Pogba analia?
Ndipo hapo nakumbuka mistari ya nyimbo ya Msondo Ngoma; Ukiona mtu mzima, analia mbele za watu ujue kuna jambo - KILIO CHA MTU MZIMA
Kilio cha mtu mzima Pogba kinanikumbusha matukio yake 2 yanayomhusu, yaliyofuatana kuharibu career yake, Nitakurudisha mpaka mwaka 2022.
Pogba anatekwa na vijana 2 wenye bastola zenye risasi za moto, wanamueleza kuwa bila bilioni 29 hawamuachii. Watekaji wanamwambia Pogba, umepata umaarufu una pesa nyingi, ila husaidii ndugu zako. Pogba anawajibu bilioni 29 mnayotaka sina labda niwape milioni 280 tu ndio niko nayo. Pogba anatoa mpunga, watekaji wanamuachia.
Pogba ilibidi ashitaki tukio hilo na baada ya uchunguzi mbeleni inagundulika injinia wa mpango huu alikua brother wa Pogba aitwae Mathias. Inasemekana kuwa Mathias ana husda na chuki kwa Pogba, inakuaje Pogba ana mihela mingi ila anachowagaia wao ni kidogo sana? Mahakama inampa hukumu Mathias ya miaka mitatu jela - USALITI WA FAMILIA!
Sept 2023 - Pogba anagundulika kutumia madawa ya kusisimua misuli na kuongeza nguvu michezoni. Anatiwa hatiani na rasmi February 2024 anaadhibiwa kwa kufungiwa miaka 4. Baadae anakata rufaa CAS na kupungizwa adhabu na kuambiwa kuwa rasmi atarudi dimba kuanzia March 2025
Matukio haya ni sehemu ya kumuumiza moyo Pogba, kumshusha kisoka, kupitia usaliti wa ndugu wa damu, kuvunjiwa mkataba na Juventus, na kukata tamaa ya Maisha. Lakini kwa kuwa Mungu si mzee Magoma, Leo hii mwamba anainuka tena, As Monaco inamuamini na kumpa mkataba mpya wa miaka miwili. Chozi la Pogba linatokana na kupata hisia kali za matukio ya nyuma na sasa anajiona kama amezaliwa upya; IN LIFE, THERE IS ALWAYS A SECOND-CHANCE!