Leo kaa chini kisha jiulize βni vitu gani vitatu vikuu vinavyonizuia kutengeneza milioni 100 kwa mwaka ndani ya miaka 2 kutoka sasa?β! Inawezekana unaona una vitu 10 vinavyokuzuia lakini hapa focus na 3 vikubwa kuliko vyote; mfano;
1) Mtaji Wa Milioni 10 ndio Unanikwamisha?
Cha kufanya; Listi down vitu 5 unavyoweza kuvifanya kujaribu kukupa mtaji wa milioni 10;
Mfano; Mkopo wa milioni 10 kutoka kwa marafiki 10 tofauti (kila rafiki akupe 1 million?)? Kuapply Milioni 100 TZS grant kutoka @Funguo_Tz ? Kutafuta wawekezaji kama @baobabnetwork?
2)Ukosefu wa Watu sahihi mfano software developers ndio wananikwamisha?
Cha kufanya; listi down vitu vinavyoweza kuongeza chance ya kupata developer mzuri;
Mfano; Kushinda @bunihub na kukutana na developers mnaoweza kuendana mawazo kisha akawa Co-founder mkaanza kufanya kazi bila kumlipa? Kujiunga Whatsap groups za developers? Kwenda vyuoni kutafuta best developers walio mwaka wa 2 au wa 3 ambao unaweza kuwafanya kama intern kwenye kampuni yako?
3) Leseni kutoka Mamlaka kama Benki Kuu ndio inanikwamisha?
Cha kufanya; Listi down jinsi ya kupata leseni;
Mfano; We mwenyewe kuomba leseni benki kuu? Kama ni gharama na hauna pesa vipi kuhusu kuanza kutumia leseni ya watu kama @TemboPlus Plus huku unasubiri leseni yako yako?
Niligundua kwa kiasi kikubwa changamoto za kupiga hatua mbele sometimes sio kubwa kama tunavyodhani lakini shida huwa ni hatuna Clarity ya changamoto hizo. Ukizivunja vunja changamoto zako kwa kuziandika vizuri chini unakuwa kwa 50% umeanza kuzitatua.
Akili ya binadamu inapojaribu kutatua tatizo kubwa lisilo na umbo au muonekano inazunguka bila mwisho na haijui pakuanzia, lakini ukiliweka tatizo kwenye karatasi linakuwa ni kitu unachoweza kukishughulikia.
Ukubwa Ni Swala La Muda Tu.