Mwenyezi Mungu alimwambia Nabii Daud (a.s.):
“Unikumbuke katika nyakati zako za furaha na neema, nami nitakukumbuka katika nyakati zako za huzuni na shida.”
"Ishi vizuri na watu, zungumza na watu wengi, jisomee maudhui mbalimbali, sikiliza kadri unavyoweza, fungua pazia na ikibidi vunja kuta za imani,dini, jinsia,kabila na mbari (race) ili kujifunza mengi usiyoyajua na kuthamini unayoyajua.Kuna mengi ya kujifunza kwa usiofanana nao."
"Utakaopata shida kuwashawishi wakukubali na kukuheshimu ni wale uliokua nao, uliosoma nao au kusota nao. Wengi wao watakumbushia madhaifu yako ya nyuma na si kutambua mafanikio yako ya leo. Usiwakasirikie. Wathibitishie tofauti." ~Togolani Mavura.
"Kuliko tukose wote bora tupate wote. Tupatapo wote hata kama ni kidogo, tunapata sababu tena ya kesho kutafuta wote. Ukitaka leo kupata vyote peke yako, kesho jiandae kukosa vyote. Kukosa kuna shari, kupata wote kuna kheri." ~Togolani Mavura.
"Kwenye maisha kuwa pia na yule rafiki katika maisha ambaye hakubishii wala hakufanyi ujisikie mjinga, yeye hukuunga tu mkono. Huyo ni muhimu sana unapokuwa umeshakusanya ujasiri na kukata shauri." ~Togolani Mavura.
"Kabla hujalaumu watu kukutenga jiulize na tafakari ikiwa katika maisha ya watu wewe ni kile kisoda ambacho huwekwa kuisimamisha meza sawasawa isiyumbe au wewe ni ule mguu mfupi wa meza unayeifanya meza icheze?" ~Togolani Mavura.
"Wafurahie wale wanaokukwepa ukiwa na shida maana wanakupa fursa ya kukutana na wale wenye uwezo na utayari wa kukusaidia. Ni bora wanaokukwepa kuliko wanaokupa matumaini ya uongo na kukuchelewesha kuwafikia wale wenye msaada kwako." ~Togolani Mavura.
Last year, my wife, friends and I had this 'brilliant' idea: drive our 30+ years Mercedes from Tanzania all the way to the southernmost tip of Africa.
36 days, 13,663 kilometers and 7 countries later;
Here is the story of our epic road trip:
Dear organizers of awards shows,
Don't tell people they're nominated for an award & then ask them to pay to attend the ceremony. Sounds like extortion to me. Nominees should receive complimentary tickets. If you can't afford that then don't have a show. Deliver awards to them.
“Kwanza tafuta nafasi, ukipata nafasi onesha uwezo, ukionesha uwezo utajenga jina na kuaminika, ukiaminika utaanza kupata hela. Katika kupitia hatua hizi ni lazima ukubali maumivu ya mchakato wa lazima.” - Ruge Mutahaba