BARUA YA LINCOLN KWA MWALIMU WA MTOTO WAKE!🙌
Mwanangu, Atapaswa kujifunza, kwamba binadamu wote hawapendi haki, binadamu wote si wakweli. Ila mfundishe pia kuwa kwa kila mwanasiasa mbabaishaji, kuna kiongozi anayejitoa.
Mfundishe, kwa kila adui kuna rafiki. Mfundishe, dola moja iliyovujiwa jasho ina thamani kuliko dola tano za kuokota.
Mwache ajifunze mapema kuwa waonevu ni rahisi kujikomba.
Shuleni, mfundishe kuwa ni heshima kubwa kufeli kuliko kufanya udanganyifu.
Jaribu kumpa mtoto wangu nguvu asifuate umati, pale kila mtu anapofuata mkumbo.
Mfundishe asikilize watu wote, lakini mfundishe pia kuchuja yote anayosikia.
Mfundishe kuziba masikio kwenye kelele za waombolezaji.
Mfundishe kwa upole, ila usimdekeze, kwa sababu ladha ya moto hukifanya chuma kiwe imara.
Mfundishe, jinsi ya kucheka akiwa na majonzi.
Na awe mwangalifu na utamu uliopitiliza😔
Kijiweni Leo na Mwalimu wa zamu @AziziKasese ✊Laptop bora wacheck @chandolaptop ��