. @HecheJohn Keep standing with the people……….. WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE!!!!!!!!!!!!!
Wewe na Lissu mnashikilia ndoto zetu na matumaini yetu. Kila kitu tumeweka kwenye mikono yenu nyinyi wawili.
Please msituangushe,
Sisi hatutaki maridhiano na waliotuua kabla ya uwajibikaji na ukweli wa October 29. Hatutaki na hatutayatambua maridhiano ambayo hayatosimamiwa na International community. Na bila Tundu Lissu mezani kutuwakilisha Watanganyika hatutatambua maridhiano yoyote. Na wakimnyonga ndio wasahau kuna kitu kinaitwa maridhiano kitakaa kitokee Tanzania. THIS IS A PROMISE!!!!! Ni itakuwa mtifuko mpaka milele!!!!!!
@HecheJohn Sisi wananchi tuliopigwa risasi kama mbwa hatutaki kupeleka pole wala rambi rambi kwa shetani wa miguu miwili alietuua kama kuku.
Tuko tayari kuishi kwa chuki na mshike mshike mpaka haki itakopatikana ila katu hatutaki amani ya kinafki na waliotuua ili washikilie madaraka bila idhini yetu.
Na katu hatutokubali statement za ‘Let Love lead’ tunataka statement za ‘LET JUSTICE LEAD’. Love iliisha October 29 2025, sasa kinachotafutwa ni haki. Haki ikipatikana Love itakuja yenyewe.
Na katu hatutokubali kumtambua Samia Suluhu kama Rais wa Tanzania au serikali yake kama serikali halali.
Huu ndio msimamo wa wananchi, NAWASILISHA!!!!!!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 187
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi ASP Geofrey Lutufye.
Mhe. Lissu: Mnajifanya mapolisi mnawasingizia watu vitu vya bure haya itakushangaza hao mliowakamata baada ya kesi yao kuisha ni mashahidi wa kesi hii?
ASP Geofrey Lutufye : Hainishangazi.
Mhe. Lissu: haikushangazi kwasababu huo ndio utaratibu wenu mapolisi wa Tanzania.
Mhe. Lissu: Au unabisha nikufungulie ripoti ya Jaji Mkuu Othman Chande amesema mnawafungulia watu makosa ya uongo.
Sasa nikuulize swali lingine, umewahi kuona video mimi nikiwa nazungumza habari za huo uchaguzi mkuu?
ASP Geofrey Lutufye : amekaa kimya
Mhe. Lissu: Unajua kwanini nimeshitakiwa kwa Uhaini ASP geofrey lutufye? Unajua sababu.
ASP Geofrey Lutufye : Sababu ya ile kauli uliyotoa.
Mhe. Lissu: Ipi hiyo?
ASP Geofrey Lutufye : Ulisema utazuia uchaguzi wa mwaka 2025.
Mhe. Lissu: Ndio nakuuliza uliiona hiyo video?
ASP Geofrey Lutufye : Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Hawa ndio kesho watakuwa ma RPC siku inayofuata utashangaa anakuwa IGP,
Sina maswali mengine Waheshimiwa majaji.
Watu wanasonya tu hapa.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude kwa ajili ya Re-examination
Maelezo yako uliandika kama nani?
ASP Geofrey Lutufye : Kama shahidi.
Wakili: Unalizungumziaje kuhusu kujiandika mwenyewe?
ASP Geofrey Lutufye : naweza kujiandika mwenyewe au kuandikwa.
Renatus Mkude: Sina swali lingine. Re Examination imeishia hapo.
Jaji anamruhusu Shahidi.
Shahidi anatoka akiwa ameshika kipaza sauti.
Jaji Ndunguru: Unasahau maji yako hapo.
Shahidi: Hapana siyataki tena.
Jaji: Basi turudishie hiyo MIC tafadhali.
Anairudisha na kutoka nje akiwa anatikisa kichwa.
Watu wanacheka.😂😂😂
Kesi inaahirishwa watu wakale.
Tutaendelea baada ya lisaa limoja.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 12, 2026
Jana tuliishia Part 159 so leo tunaendelea na-;
Part 160.
Ni siku nyingine, karibuni tena leo kwenye Darasa la Sheria.
Mhe. Lissu tayari ameingia, kama kawaida Wananchi wamepiga shangwe ile ya Rais! Rais! Rais!
Majaji nao wameingia kama kawaida yao wapo watatu.
Naona Kizimba kimetobolewa kidogo upande wanaokaa Majaji ila kama shaidi ni mfupi hata Majaji hawawezi kumuona ila tuendelee.
Jaji Ndunguru anasema sasa tuendeleee.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude Wakili wa serikali Mkuu anasaidiwa na Ajuaye, Katuga, Ignas, Thawabu, Cathbert na Winiwa Kasawa tunaiwakilisha Jamhuri na mshitakiwa yupo hapa Mahakamani.
Shahidi P11 ana dharula lakini leo tumekuja na P5 leo kama atakuwa tayari tutaendelea.
Jaji Ndunguru anasema Mshitakiwa unasemaje?
Mh. Lissu anajibu anasema kimsingi niko tayari isipokuwa niliambiwa ni P11 sasa nipeni dakika 5 niyatafute maelezo ya huyo P5 niyapate kwanza hapa halafu tuendelee kushughulika nae mimi sina shida kabisa.
Ngoja nitafute hayo maelezo yake vizuri.
Jaji Ndunguru anasema sasa sisi tunakupa dakika 10 sio tatu na unaruhusiwa kukaa pia sio lazima usimame sana hapo.
Lissu anajibu hakuna shida kabisa Waheshimiwa Majaji.
Mheshimiwa Lissu ametafuta kidogo makabrasha yake hapa amepata hayo maelezo amekaa kuyasoma na amemaliza anasema tunaweza kuendelea Waheshimiwa majaji.
Jaji Ndunguru tunamuomba shahidi.
Anasimama Renatus anasema shahidi ataongozwa na Wakili Ajuaye Nzengeli Wakili wa Serikali.
Anasimama karani anateta jambo na Jaji anashuka chini kuongea na Mawakili wa Serikali.
Anarekebisha mitambo pale.
Tunasubiri kuona nini kinaendelea.
Anaingia askari mmoja kwenye kile kizimba, anapelekewa kipaza sauti huyo shahidi.
Kile kizimba kimefunguliwa kidizaini ambayo Majaji wao wanadai wanamuona.
Jaji anasema tutamuuliza kuhusu umri wake na dini yake kabla ya kutoa ushahidi wake.
Umri wangu ni miaka 33.
Dini yangu ni Muislamu.
Huyo ni Shahidi P5 Ambae ni shahidi wa nne (4) kwa maana ya (PW 4) lakini jina lake alilobatizwa ni P4.
Ajuaye anasimama anasema shahidi unanisikia hapo?
Unaishi Wapi?
Naishi Kibangu, Ubungo Mkoa wa Dar es salaam.
Shahidi ana lisauti fulani ningesema linafanana na la nani ila acha niache.😂
Anasema anafanya kazi ya Machinga, mjasiriamali, saa nyingine naosha magari.
Unauza bidhaa gani?
Nauza viatu, saa zingine nauza soksi.
Shughuli zangu nafanyia Mchikichini, Kariakoo, Posta ya zamani, Feri hadi Posta Mpya.
Ajuaye anaendelea kumuhoji hapa na shahidi anajibu kama ninavyowaeleza.
Elezea sasa bidhaa zako unachukulia wapi?
Shahidi wa kificho ; Ilala Boma, Sokoni..
Eleza tar. 04/04/2025 ulikuwa wapi?
Shahidi wa Kificho: Nilikuwa Posta ya zamani Garden eneo la NBC Bank nikiwa naperuzi mitandao ya kijamii kwenye simu yangu?
Ajuaye: Sasa eleza ulikuwa unaperuzi kwenye mtandao gani?
P5: Facebook, Whatsapp na Youtube, nilikuwa naperuzi kwa kutumia simu yangu aina ya smartphone sonny experior Galaxy
Sasa wataalamu wa simu mtatusaidia hapo hiyo aina ya sim sie wengine hatufahamu zaidi. Acha tuendelee kumsikiliza shahidi.
Anaendelea hapa.
Wakati naperuzi niliona video ndogo ikimuonesha Tundu Lissu, niliona video Facebook.
Ni kama Majaji wamechoka wanamshangaa Shahidi, sisi hatumuoni lakini sura za majaji ni kama wanakunja.
Niliingia faceebok kwanza lazima uwe na account na bando la kutosha. Mimi niliingia kwasababu nilikuwa tayari nina account yangu.
Maswali anayoulizwa shahidi na Wakili wa Serikali na Majibu yake ni kama anajibu kwa kusoma mahali maana kuna muda anajibu jibu ambalo haliendani na swali.
Video ilikuwa ya Tundu Lissu, mimi namfahamu kwa kutumia vyombo vya habari na mitandaoni.
Wakili wa Serikali : Na wewe binafsi unamfahamuje?
P5 : Na mimi namfahamu.
Basi nikubadilishie swali, Tundu Lissu ni nani?
Shahidi: Tundu Lissu ni mwanasiasa.
Part 161 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 156
Anaendelea Mhe. Lissu
Kifungu cha 282 cha CPA amekisoma Katuga hapa kwamba Mahakama inaweza ku regulate taratibu zake wakati wa kutekeleza wajibu wake wa jinai.
Msifungwe sana na hizi kanuni maana mnaweza kuregulate procedure zenu.
Sasa kifungu cha 282 sio kichaka cha kujificha ili kukiuka sheria na taratibu zilizowekwa wazi.
Utaratibu wa kulinda mashahidi umewekwa wazi kifungu cha 194 cha CPA na kanuni za ulinzi wa mashahidi.
Huu mualiko wa kwamba muache sheria inasemaje mtafute busara zenu nawashauri msikubali huu mwaliko wa Katuga wa kudharau sheria.
Anaendelea Mhe. Lissu.
Wakili wa Serikali anasema Haki itatendeka tu hata kama shahidi haonekani.
Sheria inasema amri yoyote ya kulinda mashahidi haipaswi kuathiri haki ya kusikilizwa kwa usawa.
Shahidi ambae wao wanamfahamu mimi simfahamu, wao wanamfahamu jina na taarifa zote mimi sifahamu kuna usawa hapo?
Mahakama itaeleza hatua za kulinda mashahidi kwa usawa wa pande zote.
Hiki wanachoomba kinakiuka kanuni ya 6(2) ya kanuni za kuficha mashahidi.
Waheshimiwa Majaji yote niliyosema nimeyazungumza kwa kulinganisha na Katiba ya Tanzania na sheria za Afrika na Dunia kote.
Nilieleza kwa kina namna sheria zote za kimataifa zimezungumzia suala hili ila wao hawajajibu hata moja.
Hawajajibu kwasababu hayajibiki Waheshimiwa majaji, na hayajibiki kwasababu ni ya kweli. Tuishie hapo.
Kuhusu kanuni kutumika retrospectively, imesemwa na Katuga kwamba kanuni zote za utaratibu zinatumika retrospectively.
Sasa waheshimiwa majaji kanuni za procedure ambazo haziathiri haki zina retrospective effect.
Kanuni za procedure zinapoathiri haki haziwezi kutumika retrospective.
Angalieni ukurasa wa 11 na 12 wa Hukumu aliyoleta Katuga inasema if the legislation affect substantive right it should not operate retrospective.
Sasa hapa tunajadili right to be heard na kanuni hizi mshitakiwa hawezi kumjua shahidi kuanzia majina na vingine.
Kanuni hizi zina affect substantive right.
Kanuni zinakiuka haki zangu za Kikatiba hatuwezi kuziacha hivi zilivyo zikatumika kama wao wanaona ni jambo dogo wamlete shahidi wao hadharani hapa tumenyane nae waone.
Anaendelea Mhe Lissu.
Hizi kanuni zenu mlitunga kwa ajili yangu na matakwa ya kisheria yanakataa.
Sio mnamkamata mtu, mnamfungulia kesi halafu baadae ndio mnaenda kutunga kanuni kwamba tumtungie sheria gani?
Wamepitisha hizo sheria zao ili waje kunishitaki nazo, hilo haliwezekani kabisa.
Huyu Katuga anapenda sana kusema mimi naitishia Mahakama labda hajui nashitakiwa kwa kosa gani?
Nisipojitetea kwa nguvu zangu zote itakuwaje?
If i dont defend myself to the best of my ability itakuwaje?
Nisipoibua yote haya consequences ni adhabu ya kifo.
Maisha ni matamu i am not ready yet to die kama kuna la kusema nitasema tu.
Nitatishaje majaji wa Mahakama Kuu niko Gerezani miezi 10 ila ninachotaka Majaji muyatizame mambo haya kwa kuangalia uzito wa kesi hii.
Naomba kumalizia kwa kusema yafuatayo:
Kwamba ile kesi ya Mahakama Kuu iliyokuwa mbele ya Jaji Mkwizu, Waheshimiwa Majaji mtajiridhisha wenyewe mtakaposoma hiyo kesi mtaona kwamba hiyo kesi haikuwa inahusu uhalali wa hizi kanuni, haikuwa inahusu uhalali wa mashahidi kutoa ushahidi kwa kificho. In fact iliishia kwenye PO (Pingamizi la awali) Jaji hakutaka kusikiliza.
Sasa imeletwa hapa ili iweje? Haina uhusiano wowote na constitutionality ya kanuni na suala la shahidi kutoa ushahidi.
Wameleta hapa ili muone kuwa walishinda hiyo kesi. Hawana kingine cha maana. In fact ilikuwa ni kesi ya cyber crime na sio kesi hii ya uhaini.
Naomba mtafakari hoja zangu na mkubali shahidi asiruhusiwe kutoa ushahidi kwenye hilo box kwasababu zote ambazo nimezieleza.
Nataka Majaji mumuone shahidi na mimi ambae wanasema ni muhaini nataka nimuone, nimuhoji na anijibu.
Part 157 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
@SimbaSCTanzania Kusurport simba na yanga kwa sasa ni kuhalalisha mauaji ya ndugu zetu waliouwawa Oct 29 na ni usaliti mkubwa.
Timu kubwa zenye mashabiki hazikuguswa na mauaji hayo huku wakiwemo mashabiki wa mpira.
Hatuungi mkono kitu chochote kinachohusu mpira wa Tanzania 🙌🙌
@SuluhuSamia umefanya propaganda wiki nzima kuwahadaa Watanzania kuwa Marekani inakusapoti mtu ambae umeua wananchi ili ubaki madarakani ila leo Trump kaiingiza rasmi Tanzania kwenye nchi zenye partial travel ban to the US. Na wewe na wenzio wooote mlioshiriki kuua wananchi waliokuwa wanadai haki zao mnapigwa full ban ya kuingia Marekani na soon Europe pia wanawapiga ban.
Mnahangaika kutafuta uhalali baada ya kuua watu?? Wewe ni Rais batili ulieua wananchi zaidi ya elfu 10 ili ubaki ikulu.
@SuluhuSamia kama jinsi mlivyofosi vyombo vya habari vyote Tz kuposti uwongo wenu kuwa mnasapotiwa na Marekani na UN wapeni ruhusa waposti na hii.
Alafu mnachekesha mnooo, nyie si mliwaambia hawa ‘who are you? , mbona sasa mnahaha kukubalika na kina ‘who are you?’ . Nyambaf roho zinawaenda mbio kukosa mikopo ya kununua ma Bugatti na kufanya anasa. NA BADO!!!!!
Mnataka kufunika uhalifu wa kiwango hiki?
Mnataka mauaji ya kutisha kama haya niliyoona kwenye video yanyamaziwe?
Nani alietoa amri kuua watu wengi kiasi hiki?
Ukiacha mauaji ya kwenye vita,
sijaona mauaji ya kisiasa makubwa kiasi hiki.
Hata makaburu hawakuua watu wengi kwa pamoja kiasi hiki..
Je hawa wauaji ni Watanzania wenzetu?
Watu walioingia na kukuta watu wanaangalia mpira na wakawaua wote kama kuku.
Hili halitaweza kufunikwa, lazima watu wawajibike
You can treason this man by what he spoke, he is so clever he can defend himself with facts and evidence, he can beat you with reality and use your weakness you didn't have addressed on your trap
Tell your kids, This man is innocent so they can't blame you 4 not doing anything.
Makaburu wa Afrika kusini walizuia watu weusi hata kutembeleana, miaka mingi baada ya Uhuru wa mtu mweusi serikali ya Samia inazuia watu wetu hata kutembeleana.
Serikali ya waoga.
Hili sio shambulio dhidi ya @JamiiForums hili ni shambulio dhidi ya uhuru wetu.
Watanzania mnaweza kufikiri hili ni la Melo na Jamii forums, lakini watawala madikteta wanataka msikie, msome na muone wanachotaka muone na kusikiliza..
Hawataki msikie , muone na msome mnachostahili, wanataka bongo ana akili zenu ziwe na taarifa wanazotaka wao.
Kwa kudhibiti habari wanaweza kutaka nyie muamini kwamba wao ni Mungu na pumzi tunayovuta ni mali yao.
Jamii forums inashambuliwa kwasababu ya kuwajulisha Watanzania ukweli kuhusu , kauli za kiongozi mkubwa wa ccm ambae kwa mtu mwenye akili huwezi kuzipuuza.
Huwezi kupuuza kauli za Polepole ambae amehudumu serikalini hasa anaposema siri za ndani ya vikao alivyokuwepo.
Kama kuna uongo ni kiasi cha watuhumiwa kutoka na kufanya ufafanuzi na kuonesha ukweli sio kufungia chombo cha habari.
Watanzania tusikubali kupelekwa shimoni na madikteta, hatari ni kubwa mno tusipokuwa makini.