"Tanzania hakuna upinzani wa Kweli". Ili Chama cha Upinzani ki-survive ni lazima kuwe na mkono wa serikali. Tumeona kwa NCCR, TLP, CUF, na sasa ACT. Hata CDM imefanya hivyo miaka yote kwa siri chini ya FAM. Anachojaribu kufanya TAL ni kuunda Chama cha Upinzani Huru, je, ataweza?
@EduTalkTz Ifike hatua tuweke sheria, mtu yeyote aliyewahi kutunukiwa shahada yoyote ya taaluma ya juu asiruhusiwe kuingia kwenye siasa. Na kama akiruhusiwa anyang'anywe kwanza shahada alizotunukiwa ndipo aingie ili kutozinajisi taaluma zetu na vyuo vilivyotutunuku shahada hizo.
@Mwatexi@Roma_Mkatoliki Umeiweka kitaalamu ila wasiojua taaluma hii hawawezi kuelewa, na wataona umalazimisha kutafuta makosa. Ndio maana tasnia ya filamu Tz ni ngumu sana kutoboa kimataifa. Makosa kwenye kazi zetu ni mengi, ila sisi tunaangalia tu touching story na kuona kwamba huo ndio ubora.
@ccm_tanzania Doa la "kupotea" kwa aliyekuwa msemaji wa chama, mjumbe wa kamati kuu, balozi mstaafu Ndg Polepole, na hakuna kauli yoyote ya chama kutolewa ni dhahili haliwezi kufutika, na hivyo mahubiri yote yanayohubiriwa sasa kuhusu amani, umoja na mshikamano yanabaki kuwa uhuni mtupu.
@rollymsouth Ushauri wangu: Hiyo dhambi kubali kwenda nayo kaburini. Hata ukiisema mbele ya watu hakuna itakayomsaidia.
Kosa lako siyo kusema mlikula pesa, wala sisi hatutaki kujua mlikuwa wangapi.
Kosa lako ni "Kwanini ulipokea pesa kwa ajili ya kuikomboa nchi yako mwenyewe?"
@rollymsouth Sisi tutasimama na wanaharakati halisi, ambao wengine wamepoteza maisha na wengine haijulikani walipo kama wakina Polepole. Hao ndio tunaowatambua, na kutambua mchango wao ktk taifa hili. Na kama ni kuwaunga mkono, hao ndio wenzetu, siyo nyinyi mnaolipwa kwasababu ya majina yenu.
@rollymsouth Tunajua Activism kwa wengine ni ajira, hasa maenfluencers ambao hawana chimbuko la uanaharakati. Tunajua mpo wengi mliolipwa, ila pia tunajua wapo wengi waliojisacrifices bila senti moja. Nyinyi mliongia kwenye harakati kibiashara msiwaharibie wanaharakati waliojitoa sadaka.
Ushauri wangu kwa CHADEMA:
Ikiwa kweli msingi wa chama ni nguvu ya umma, basi umma upewe mamlaka ya kuamua nani arudi au asirudi chamani. Kuwepo mijadala ya wazi na kura za wazi zipigwe kwa kila anayeomba kurejea chamani.
Asante.
@HecheJohn@godbless_lema@IAMartin_@ChademaTZ2
@IAMartin_@Reye79395081 Kikubwa imarisheni sana intelligensia ya chama. Hili ninawaomba sana, huko mbele ni kugumu zaidi ya mnavyofikiria kama mkienda hivi mnavyoenda.
@EduTalkTz Kati ya wizara ngumu na yenye ukata wa kutupwa ni hii ya huyo jamaa. Ndio maana inabidi mtu aje na project ya namna yoyote ile ilimradi keki itafunwe. Na waliomtupia huko walijua hilo, na wanajua kuwa hakuna kazi ya kufanya.
@earadiofm Kitu nilichojifunza: Kama unataka nafasi za juu za uongozi hakikisha uwe una "akili". Kama unajijua ni bumunda usigombee wala usitamani kuwa kiongozi, utaaibika.
Uongozi ndio mahali pekee ambapo ukweli kuhusu upunguani wa mtu au maarifa ya mtu huonekana.
Opposition politicians are behind bars. The media remain muzzled. Outsiders are unlikely to help. A pall of fear hangs over Tanzania. Samia Suluhu Hassan is taking her country down a ruinous road https://t.co/DWNrZp0MPH
Photo: Xinhua News Agency/Eyevine
@salmakorosho Inawezekana. Watakaosajiri magari yao kwa kazi hiyo wanaondolewa baadhi ya ushuru/kodi na baadhi ya tozo za serikali. Magari hayo yanakuwa rasmi kwa ajili ya wanafunzi, nauli 200/.
@TZMsemajiMkuu Humphrey Polepole alikuwa ni msemaji wa Chama. Baadae mfumo ulimkataa. Mazuri yake yote yalifutika. Jitihada zake zote zilifutika. Alidhani alikuwa anatimiza wajibu wake kama vile unavyodhani wewe leo. Kumbe alikuwa anajichimbia shimo lake mwenyewe. Kuna siku mfumo utakukataa.
@AllyAssed13070 Watu kama hawa ndio wanaziweka familia zao ktk wakati mgumu pindi wanapokufa. Kipindi ndugu, jamaa na familia zinaomboleza, maelfu ya raia washangilia na kusherehekea. Chanzo kikuu huwa ni ujinga kama huu uliofanywa leo.