THE LAW SCHOOL OF TANZANIA:
Iko hivi; yaani pale LAW SCHOOL OF TANZANIA, hawaangalii wewe ni WAZIRI, MKURUGENZI au MENEJA. Ukiwa ni KICHWA PANZI, UWAKILI utausikia kwenye BOMBA. SHERIA siyo GAZETI ambalo kila mtu anaweza KUSOMA.😂😂
serikali haina mamlaka ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, na katazo la katambi halina msingi wowote wa kikatiba au kisheria; ni katazo batili.
🎥: @BoniphaceEric:
The One and Only Tundu Lissu 🔥🤣
Yaani ye sasa akisema “haliishi mpk liishe” ndo unatakiwa kuelewa! No retreat! No surrender 💪🏽
Leo kimama kitalala na viatu na liroho lake chafu lenye husda!
Rais! Rais! Rais!
Kimama kitaugua kabisa leo maana watanzania Rais wetu ndo huyu Tundu Lissu 👊🏽
Mungu atasimama na kudhihirisha Ukuu wake muda si mrefu!
Tuseme AMEN 🙏🏽 #FreeTunduLissu
"Mpaka jioni ya leo tarehe 02 Julai 2026 zoezi la postmortem ya mwili wa marehemu Suez Dani Maradufu, aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche halijaanza." - Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bara, Amani Golugwa.
🔥🔥👊🏽 Tundu Lissu ‘s spirit 🔥🔥
Mkisikia Aluta Continua ndo hii!
Madhulmat wanakaribia kutema bung’o msidanganyike! Lissu kawaambia wamwachie ni haki si fadhila! Hawezi kupiga magoti!
One day we will learn to appreciate this man! Amechagua njia ngumu ili sote tupone!
Mungu amlinde 🙏🏽🫡
#FreeTunduLissu
Hadi Zanzibar pamechangamka!🔥
Kwa mujibu wa mkazi huyu jana watanganyika waliandamana huko Stone town wakipinga kubaguliwa na wazanzibari
Tanganyika AMKA 🔥👊🏽
Muda ndo huu kuwekana sawa tupate #KatibaMpya bora kwa pande zote
#77Tunatoka wote hakuna namna!
Mbona #TutaelewanaTu ?
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kimefungua kesi dhidi ya viongozi saba wa serikali kwa madai ya kushiriki njama za ubadhirifu wa fedha za umma, matumizi mabaya ya ofisi na kuhujumu uchumi, katika kashfa ya mafuta.
Mwanaharakati na Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka, ameweka msimamo mzito wa kisheria kuhusu utendaji wa vyombo vya dola nchini, akibainisha kuwa mtendaji yeyote wa Jeshi la Polisi anayetekeleza maagizo ya viongozi yaliyo kinyume cha sheria hana mwavuli wa kujitetea, bali anakuwa anashiriki uhalifu wa kuvunja Katiba.
Wakili Madeleka ameongea hayo leo, Jumatatu, Juni 29, 2026, wakati akizungumza kwenye mahojiano maalum na Royal TV jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mwendelezo wa mwangwi wa kisheria kufuatia malumbano yanayoendelea nchini kuhusu mipaka ya maelekezo ya viongozi wa Serikali na utekelezaji wa sheria.
Mwanaharakati huyo amefafanua kuwa nchi haiwezi kuendeshwa kwa maelekezo ya mifukoni mwa viongozi bali kwa mujibu wa sheria na Katiba, huku akionya kuwa kuvaa magwanda au kuwa na vyeo vya "manyota" hakumfanyi askari kuwa juu ya sheria anapotekeleza amri haramu.
"Kama waziri anatoa tangazo anatoa maelekezo ambayo yako kinyume na sheria, halafu yule ambaye kapewa aende akasimamie au wakatekeleze matakwa ya sheria anatekeleza kitu ambacho kinyume cha sheria... yaani hapo hakuna excuse (utetezi). Wote wamevunja sheria, aliyetoa hayo maelekezo na aliyekwenda kuitekeleza, kwa sababu hii nchi haiendeshwi kwa maelekezo, inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kwa mujibu wa katiba," amesisitiza Wakili Madeleka.
Mwanasheria huyo ameshangazwa na utamaduni wa viongozi wanaosimama mbele ya kamera na kudai wanalinda Katiba wakati vitendo vyao viko kinyume, akibainisha kuwa changamoto kubwa ya sasa nchini si kusoma sheria, bali ni uwezo wa kuzitafsiri sheria hizo kwa vitendo bila kuleta mkanganyiko unaowafanya wasomi kufanana na watu "walioishia darasa la pili."
Katika hatua nyingine, Madeleka amewatwika mzigo wa lawama waandishi wa habari kwa kuwa "wasikilizaji watazamaji" badala ya kuhoji kwa kina, akiwataka wanapomsikia kiongozi akisingizia Katiba, wambane ataje kifungu na sheria mahususi inayompa mamlaka hayo ili kuona kama anachokisema kinaendana na vitendo vyake.
Mzee wa Minyama @mshambuliaji akiwa Mjini Atlanta , Marekani anatupitisha kwenye Gari inayojiendesha yenyewe bila Dereva.
Fuatana naye toka mwanzo wa safari yake mpaka mwisho.
#KitengeUpdates