Tunachokijua ni kwamba wewe ndo uliyeua ndugu zetu October 29.
Na kwamba umepoteza uhalali wa kuunda Tume yoyote ya kuchunguza mauaji yaliyotekelezwa mikononi mwako.
Na kwamba hata ungeteua watu kutoka juu Mbinguni waje kuchunguza tungekupinga kwa nguvu zetu zote.
Wewe majibu yako tunayo tayari, kwamba nguvu iliyotumika kuua kwa RISASI na kujeruhi ilifanana kabisa na nguvu waliyoitumia waandamanaji. Kwamba jeshi la Polisi lilifanya kazi nzuri na linahitaji pongezi,na kwamba wazazi hawakutimiza wajibu wa kuwazuia watoto wao wasiende kuandamana hivyo wasikulaumu kwa lolote, haya ya kwako tunayajua tayari, na haya ndo majibu ya kila utakayempendekeza na kumteua hata ashuke Malaika kutoka mbinguni.
Tume tunayoitaka sisi ni Tume shirikishi, Tume ambayo UN, AU, SADC na Commonweath watatuma wawakilishi ambao watanzania tutawaridhia, Tume ambayo haitahitaji kibali chako kuandika ama kuchunguza chochote, Tume itakayoanza kukuchunguza wewe na Jeshi lako la Polisi kabla haijawachinguza wananchi.
Hiyo ndo Tume tunayoitaka sisi sio hizi YADAYADA ZAKO...
UNATUCHOSHA, SISI SIO VIKATUNI VYAKO KUTUCHEZESHA VILE UNATAKA.
Nafikiri nitaeleweka kirahisi.
Tujadili kuhusu; Commission of Inquiry into the Post-Election Violence (CIPEV), chini ya Jaji Philip Waki,
Waki Commission (Tume ya Waki) iliundwa kwa tangazo la Gazette Notice ya Rais Mwai Kibaki,
Terms of reference (ToR) zake zilitangazwa katika Kenya Gazette Notice No. 4473 ya 22 Mei 2008
Tume hiyo ilikuwa na jukumu la:
1. Kutafuta na kuchunguza chanzo na mazingira yote ya ghasia zilizofuata uchaguzi mkuu wa 2007.
2. Kuchunguza vifo, ukiukwaji wa haki za binadamu na uharibifu wa mali uliotokea wakati wa ghasia.
3.Kuchunguza mwenendo wa vyombo vya usalama, ikiwa ni tuhuma za matumizi ya nguvu kupita kiasi.
4.Kubaini watu waliobeba jukumu kubwa katika kupanga, kuchochea au kutekeleza vurugu.
5.Kutoa mapendekezo ya namna ya kuzuia vurugu kama hizo zisijirudie katika chaguzi zijazo tena.
6.Kupendekeza namna ya kuwawajibisha wahusika wa makosa makubwa yaliyofanyika katika vurugu.
Hii tume yenu ya jana, majaji wa Uganda;
ToR zake zimetangazwa gazeti la Serikali au zinatoka tu kwa mtu aliyeunda tume na kuteua wajumbe?
Kwanini hii tume yenu haitaki kabisa kuweka ToR ya kuchunguza mwenendo wa vyombo vya usalama?
Au, matumizi ya nguvu yalikuwa kidogo tu? Nafikiri, waliopiga watu risasi, wanatakiwa kuchunguzwa.
Tume hiyo chini ya Jaji Philip WAKI iliundwa katika mazingira ya National Accord ya mwaka 2008,
National Accord iliyofikiwa baada ya mgogoro wa uchaguzi kati ya Mwai Kibaki na Raila Odinga,
Lakini kitu cha muhimu zaidi katika mchakato huo, usuluhishi huo ulifanyika chini ya Kofi Annan.
Ripoti yake, iliyojulikana kama Waki Report, ilipendekeza mambo mengi hadi kufikia muafaka
Baadaye, suala hilo lilihusishwa na kesi zilizofikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Ripoti ya Waki iliwasilisha majina ya wahusika wote wa vurugu na nyaraka nyingine kwa Koffi Annan,
Baada ya Serikali ya Kenya kushindwa kuanzisha mfumo wa ndani wa kuwawajibisha wahusika,
Koffi Annan aliwasilisha nyaraka za tume kwa Mwendesha Mashtaka wa ICC, Luis Moreno Ocampo,
Mahakama ya ICC iliidhinisha rasmi uchunguzi kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya.
Kenyatta, William Ruto, Francis Muthaura, Henry Kosgey, Joshua Sang na Hussein Ali, wakashtakiwa
Uhuru alikuwa upande wa PNU/Kibaki, wakati Ruto alikuwa mshirika muhimu wa ODM/Raila Odinga.
Hata hivyo, ICC iliwahusisha wote wawili na wenzake katika makundi tofauti ya madai kuhusu ghasia hizo.
Henry Kiprono Kosgey alikuwa Waziri wa Viwanda (Minister for Industrialization) Serikali ya Kenya.
Mohammed Hussein Ali alikuwa Commissioner of Police (Mkuu wa Jeshi la Polisi Kenya) 2004 - 2009.
Francis Kirimi Muthaura alikuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Baraza la Mawaziri - Kenya.
Hapa kwenu kabla hata ya usuluhishi, mnatengeneza tume na kuweka ToR za kushughulikia msiowapenda.
Kwanini hamtaki kuweka ToR za kuwachunguza waliotoa amri na kutekeleza amri za mauaji ya raia?
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
VIDEO:
Saa chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuzindua Tume Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTZ2 Bara, John Heche @HecheJohn ametoa msimamo mkali wa kuikataa tume hiyo, akiitaja kuwa ni mbinu ya kutaka kutengeneza picha isiyo halisi mbele ya jumuiya ya kimataifa.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika wilaya ya Rorya mkoani Mara leo Agosti 07, 2026, Heche amesema kuwa CHADEMA haitambui tume hiyo na matokeo yake yoyote yatakayotolewa yatakuwa ni "feki". Heche ametumia mfano wa ujenzi wa ghorofa juu ya tope kuelezea kutokuwa na imani na tume hiyo, akisema kuwa haiwezi kupata ukweli ikiwa inaongozwa na ripoti ya tume iliyopita.
Heche amekosoa vikali uamuzi wa kumjumuisha jaji kutoka Namibia, na Jaji kutoka nchini Uganda akidai kuwa nchi hiyo ina rekodi mbovu ya haki za binadamu na uhuru wa mahakama. Heche amesisitiza kuwa msimamo wa chama chake ni kuendelea kudai Katiba Mpya na msuluhishi wa kimataifa anayekubalika na pande zote.
Hata hivyo, Rais Samia ameelezea imani yake kuwa majaji wote waliopo kwenye Tume hiyo, watatumia uzoefu wao wa miaka mingi kutekeleza majukumu yao ndani ya miezi mitano ijayo kwa kwa “weledi, umakini, na uadilifu mkubwa”.
ALERT: Watu watatu walipelekwa Russia kwenye mafunzo maalum. Taarifa za ndani kwamba washarudi, lengo ni kuondoa vikwazo ndani ya CCM wakiongozwa na Nchimbi.
Balozi Nchimbi, kuna watu ndani ya mfumo na Jeshi wanakuamini. Omba ulinzi mpya. Hawa watu wanasimamiwa na TISS Kizimkazi
‼️MAFEDHULI WAMEPANIC‼️
Mdau huyu amenikumbusha ule mpango wa kulisha sumu upo palepale na wamepanga kuutekeleza muda wowote kuanzia sasa ila sasa focus ni Lissu na Nchimbi huku Heche wanamwinda nje na hatakiwi kabisa kukaa mwenyewe
Muda wote @HecheJohn hakikisha umezungukwa na watu na wananchi MLINDENI!
Haya si matani au maneno tu - na mkithubutu kumsogelea Lissu gerezani hata usiku wa manane tutajua - komeni!
Nchimbi najua atawaweza mko naye kwenye mfumo na ana taarifa zenu!
Acheni kupanic nyie wauaji! Muda wenu umefika!
#FreeTunduLissu #TutaelewanaTu
Tatizo la upinzani ni njaa na tamaa ya pombe za bure. Watu wangekuwa na misimamo pasipo kujali maslahi binafsi, kuna mahali tungekuwa leo.
Ukiendeshwa na njaa wenye pesa watakufanya tissue paper.
Katika historia ya sheria, katiba zinazoanzishwa na kutolewa na watawala pekee bila ridhaa ya kwanza ya umma hujulikana kama octroyed constitutions. Katiba za namna hii hazina nafasi katika karne ya 21; tunadai Katiba inayotokana na tamko thabiti la "Sisi Wananchi" #KatibaMpya
VIDEO:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Magharibi, Wakili Dickson Matata ametoa wito na rai kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu kutumia mamlaka yake ya kikatiba kufuta kesi za ugaidi zinazowakabili wanachama na viongozi wa CHADEMA pamoja na Watanzania wengine katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza leo Jumapili Agosti 02, 2026, Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam, Wakili Matata amesisitiza kuwa katika kukamilisha hilo kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DPP anapaswa kuwa na nia ya kutenda haki, kuzuia matumizi mabaya ya taratibu, miongoni mwa mwambo mengine.
Akitolea ufafanuzi taarifa za kukamatwa kwa watuhumiwa wa makosa mbalimbali ikiwamo ugaidi hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alikanusha vikali kuwa kuna mkakati wa kiserikali wa kulenga kundi fulani, wanataaluma, au taasisi ya kisiasa.
Aliwataka wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuacha kupotosha umma na badala yake kuziachia mahakama zifanye kazi yake kwa mujibu wa misingi ya kisheria na Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayomtambua mtu kuwa hana hatia hadi mahakama itakapothibitisha vinginevyo.
#TANZANIA: KESI YA LISSU KUANZA KUUNGURUMA AGOSTI 10, "NJONI KWA WINGI MAHAKAMANI"
Katibu Mkuu wa @ChademaTZ2, @jjmnyika leo Agosti 03, 2026 akizungumza na Wanahabari amesema kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wao wa Taifa, Tundu Lissu itasikilizwa kuanzia Agosti 10, 2026 katika Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar Es Salaam na kuwasihi wananchi kuhudhuria kwa wingi kusikiliza mwenendo wa kesi hiyo.
Zaidi: https://t.co/aiTgdhroEh
KIUFUPI SANA: Madereva wa CROWN wanamatatizo ya afya ya AKILI.
Baada ya kusoma comments za wanangu kwenye ile post ya Crown kuovertake LC300 wanangu wengi wanasema vijana wanashida vichwani umeme mdogo.
Yani bora utembee na demu wa dereva wa Crown atakusamee sio KUMUOVERTAKE.😂
VIDEO:
Mwanaharakati na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Martin Maranja Masese (MMM) amewashukia wale wote wanaowatuhumu viongozi na makada wa chama hicho kuwa wananufaika na kufurahia uwepo wa Mwenyekiti wao wa Taifa Tundu Lissu gerezani, akiwataka kumuachia mara moja ili kile wanachonufaikanacho mrija wake ukate
Kupitia chapisho lake aliloweka kwenye mitandao yake binafsi ya kijamii, MMM amedai kuwa uzushi huo unaenezwa na watu aliowaita kuwa ni 'Ma-CCM' ambapo ameenda mbali kabisa na kuwataka kutekeleza kile kilichopo ndani ya uwezo wao ikiwemo kumuachia Tundu Lissu, au la wawaze namna bora ya kuendelea kukabiliana Mahakamani
Katika historia ya sheria, katiba zinazoanzishwa na kutolewa na watawala pekee bila ridhaa ya kwanza ya umma hujulikana kama octroyed constitutions. Katiba za namna hii hazina nafasi katika karne ya 21; tunadai Katiba inayotokana na tamko thabiti la "Sisi Wananchi" (We the People). #KatibaMpya