Maombolezo ya Ndugu Baada ya miezi 9 ya MAUAJI ya kutisha Dada anafamnyia ibada mpendwa wake alieuwawa Tarehe 29.10.2025, wauaji walipoteza mwili wake Mpaka sasa familia inaishi na picha ndani.
Mdogo wake Humphrey Polepole anaendelea na kampeni yake ya kuwataka wageni WOTE wanaopanga kutembelea Tanzania wasitishe safari zao kwani Tanzania kwasasa kuna ugaidi na magaidi 51 wapo Gerezani.
Vile wanasoma uamuzi wa Mahakama ya Rufani leo, kwamba mali irudi kati tuwapepete au waweke kwapani refa atupatie point tatu. Kazi anayo yule muuwaji na watu wake.
Hiyo Kesi ni Uthibitisho kwamba; “KUNA TOFAUTI KATI YA ELIMU NA AKILI”. Lakini pia, TUNDU LISSU amethibitisha kwamba; “AKILI HAZIFUNGWI PINGU”. Kajipigia KAVU KAVU.😂😂
‼️MAHAKAMA YA RUFANI YATUPILIA MBALI MAOMBI YA MAREJEO YA DPP KATIKA KESI YA TUNDU LISSU‼️
Mnamo tarehe 18 Februari 2026, Jamhuri iliwasilisha Notisi ya Nyongeza ya Ushahidi (Notice of Additional Substance of Evidence) chini ya kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), ikikusudia kuwasilisha ushahidi wa ziada kupitia shahidi ACP Amini Mahamba.
Hata hivyo, tarehe 24 Februari 2026, Mahakama Kuu ilitupilia mbali notisi hiyo baada ya kubaini kuwa kifungu hicho hakiruhusu shahidi ambaye tayari alishatoa ushahidi kurejeshwa ili kuwasilisha ushahidi wa ziada. Kufuatia uamuzi huo, tarehe 3 Machi 2026, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliwasilisha maombi ya marejeo katika Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu. Maombi hayo yalisikilizwa tarehe 3 Julai 2026.
Leo, tarehe 30 Julai 2026, Mahakama ya Rufani ya Tanzania imetupilia mbali maombi hayo ya marejeo na kuthibitisha uamuzi wa Mahakama Kuu. Mahakama imeeleza kuwa Mahakama Kuu ilitafsiri kwa usahihi kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ambacho hakiruhusu upande wa mashtaka kumrejesha shahidi ambaye tayari alishatoa ushahidi ili kuwasilisha ushahidi wa ziada.
Uamuzi huu unaweka mwongozo muhimu kuhusu tafsiri na matumizi ya kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na unasisitiza umuhimu wa kuzingatia taratibu za kisheria katika uwasilishaji wa ushahidi wakati wa mwenendo wa kesi za jinai.
Wakili @Advocate_Kisabo
Julai 30, 2026.
Top Lawyer, Top Leader, Top Character!
Umeshinda hujuma za dola kuongeza ushahidi wa ziada ktk kesi ya uhaini.
Jaribio hilo lilikuwa afterthought, baada ya kupiga chini 100% ya ushahidi wao.
ONYO: Muachieni au njooni awavue nguo tena!
Free Tundu Lissu Now!
I'm really proud of this dude. He's a rare gem in our ongoing liberation struggle. He's gone above and beyond, and he keeps pushing forward with incredible perseverance. Mungu linda huyu mwana mwema. Sisi tunakuamini Wewe na ahadi zako. Na hakika zitatimia!
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Sheria, Wakili Gaston Garubindi, kimetangaza ushindi mwingine muhimu wa kisheria baada ya Mahakama ya Rufaa Tanzania kutupilia mbali maombi ya marejeo yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) dhidi ya Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 30 Julai 2026 kwa njia ya mtandao katika shauri la marejeo ya jinai (Criminal Revision No. 7203216/2026).
Akifafanua kuhusu uamuzi huo, Garubindi ameeleza kuwa maombi hayo ya Jamhuri yalitokana na nia ya DPP kutaka Mahakama ya Rufaa ifanye marejeo dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu iliyokataa taarifa ya kuongeza ushahidi mpya wa shahidi Amin Mahamba katika kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu.
Itakumbukwa kuwa Tundu Lissu aliweka pingamizi dhidi ya nia ya Jamhuri kuingiza ushahidi huo mpya.
Mahakama Kuu ilikubaliana na pingamizi hilo na kukataa ushahidi huo kuingizwa jaladani.
Aidha, Garubindi amebainisha kuwa Mahakama ya Rufaa, baada ya kusikiliza maombi hayo tarehe 3 Julai 2026, imejiridhisha kuwa Mahakama Kuu ilikuwa sahihi kabisa kutupilia mbali taarifa hiyo ya Jamhuri iliyowasilishwa chini ya Kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
"Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali maombi yote ya DPP na pia imekataa hoja yake iliyodai kuwa hakupewa fursa ya kusikilizwa. Hii ni hatua kubwa ya kusimamia haki na misingi ya sheria," alisema Garubindi.
Kufuatia uamuzi huo wa Mahakama ya Rufaa, Garubindi amethibitisha kuwa kesi ya msingi ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa sasa inapaswa kuendelea katika Mahakama Kuu ikiwa bila ushahidi huo uliokataliwa na Mahakama zote mbili.
Kwa kuwa, maamuzi ya maombi ya marejeo (Revision) yaliyofunguliwa na DPP dhidi ya Tundu A.M Lissu, katika mahakama ya rufaa Tanzania yamesoma na Tundu A.M Lissu AMESHINDA.
Upande wa Jamhuri una machaguo mawili; turudi mahakama kuu kuendelea na tulipoishia katika kesi ya uhaini wa mchongo, au waifute hiyo kesi (nolle prosequi) na kumuachia huru Tundu A.M Lissu.
Huko Mahakama Kuu ndiyo kuna wale mashahidi wao wa siri kwenye kichumba cha joto, na wamewamaliza na walitaka kuingiza mashahidi wengine wapya. Ushahidi wao wa msingi ulikataliwa mapema.
Kama upande Jamhuri wakiamua kuendelea na kesi hiyo, tunakwenda kwenye hatua ya ‘No Case To Answer’ na Tundu A.M Lissu akikutwa na kesi ya kujibu anatakiwa kuanza kujitetea mara moja.
Mashahidi wa TAL unawakumbuka? TUONDOKEEE….
‼️NYONGEZA‼️
Hii “maadili ndogo” nimefuatilia kumbe ni kuhojiwa na Wasira 😁
Sasa Wasira ana bifu la kufa mtu maana anadai Nchimbi alipokuwa katibu mkuu alimkata mwanae ubunge akampa Esther Bulaya! Pambanenii! 👊🏽😁
Alafu sasa kumbe kosa la Nchimbi ni kumsingizia Rais kuwa ana nia ya kuleta katiba. Clearly kimama hana mpango huo na ndiyo maana kataka Nchimbi apelekwe maadili ndogo - very good!
Acha inyeshe na dhoruba juu
Sisi yetu macho hadi #TutaelewanaTu
Mpaka zero brain la taifa linatoa milio na bado.
Alafu mimi nayashangaa yanavyoongelea 2030 as if kuna uchaguzi ulifanyika 2025.
Kinachochekesha yanawaza yenyewe kupeana Urais 2030 na sio kutoa haki kwa Watanzania ili waweze kuchagua Rais wanaemtaka. Alafu wanaita wananchi wanaodai haki magaidi. Hiki kinachofanywa na kina Bashite ndio ugaidi wenyewe.
Mnasimama hadharani na kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa kwamba kuna hali ya hatari na usalama ni mdogo. Siku chache baadae mnatangaza kwamba wanaharakati ni magaidi. Mnakwenda kuwakamata watu zaidi ya 60 kwa uongo. Mnawapa mashtaka ya uongo ya ugaidi. Mnasahau kwamba mnatakiwa kuandaa AFCON ifikapo Juni 2027 na mnatakiwa kuendelea kupokea watalii na wakati huo mnatakiwa kuwavutia wawekezaji na mnatakiwa kuwaaminisha mababeru kwamba mnalinda demokrasia ili wafungulie mikopo na misaada. Hayo yatafanyika vipi katika ardhi yenye magaidi wengi kiasi hicho? Hivi nani ni mshauri wenu?