LEO, Hatua Yetu inalenga katika kujifunza kuhusu kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuimarisha umoja sehemu za kazi.
Tutakuwa na Komba Muhili, Mkufunzi wa Mafunzo ya Uelewa Sehemu za Kazi, ambaye atashiriki nasi maarifa muhimu katika eneo hili.
Saa 10:00 jioni hapa 92.1 TBC Arusha
Leo katika hatua yetu, tutajadili kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.
Tutakuwa na Mwalimu Joseph Pole kutoka Elerai Sekondari, akitupa mtazamo wake kuhusu sera hii na utekelezaji wake kwa vitendo.
Usikose!
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini Boniface Kikumbi Mwanza Mpango maarufu King Kikii amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Novemba 15, 2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Miongoni mwa nyimbo zake ni Kitambaa Cheupe
MWANAMKE NI MTU NA NUSU
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kati ya nyimbo ambazo Msanii Harmonize (@harmonize_tz) ameimba amezipenda zaidi 'Never Give Up' kwakuwa inahamasisha Watu wasikate tamaa na pia 'Na Nusu' ambao unaelezea ubora wa Mwanamke katika Jamii.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye uzinduzi wa Albamu ya #MuzikiwaMama kutoka kwa Msanii wa kizazi kipya Rajab Abdul aka #Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul aka Harmonize akitumbuiza katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Albamu yake ya #MuzikiwaMama tarehe 25 Mei, 2024.
#Harmonize
Wakazi wa Mkoa wa Arusha leo Mei 08, 2024 wamejitokeza kwa wingi katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa #Arusha, Paul #Makonda kwa lengo la kuzungumza na kusikilizwa kero zao katika programu maalum ya siku tatu ya mkuu wa mkoa ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa mkoa huo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewaambia wakazi wa mkoa huo kuwa yupo tayari kupoteza chochote alichonacho ili mwananchi wa Arusha apate haki yake
#Makonda amayasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa #Arusha waliojitokeza kwenye wiki ya haki
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), leo imewasilisha katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala ya Arusha maombi ya kuiondoa rufaa Na. 155 ya mwaka 2022 dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake, ikisema haina tena nia ya kuendelea nayo.
MKUTANO WA TANO WA MWAKA WA TEHAMA TANZANIA.
Kauli mbiu: "Kujenga Taifa la Kidigitali" @ Arusha International Conference Centre https://t.co/kYyblUsayp