@FKihamu Sio kweli. Cash huonekana ni kubwa kwasababu unalipa mwenyewe, Bima huonekana ni ndogo kwasababu kampuni inalipa. Bima ni ghali zaidi kwasababu wengi hata hawapitii bills zao kama
Kuna overcharge, tofauti na Cash mtu hupitia bills na kufanya marekebisho. It is psychological
Mimi si mshabiki wa mpira, lakini baada ya PSG kuichapa Arsenal, nimegundua noise pollution si tatizo la viwanda pekee. PSG walifanya usafi wa mazingira hadi mtandaoni.
Jana kuna mahali nilipita nikawakuta dada fulani wamevaa jezi za Arsenal. Walikuwa na kelele na kujiamini kuliko hata zile za “Oktoba tunatiki”. Kila dakika walikuwa wanatoa uchambuzi, utabiri na walikuwa wamepiga pamba kwa kiwango cha juu kabisa. Bado kidogo ningejifanya na mimi ni mshabiki wa mpira tena Arsenal. Naamini PSG hawakushinda mechi tu… walishusha pia decibel za mijadala ya mitaani. 😄 Sasa turudi kwenye FREE TUNDU LISSU na KATIBA MPYA ni SASA.
Hili nalo ni kosa ambalo natuhumiwa kulifanya kwa mujibu wa Msajili. Sasa narudia tena kusisitiza, ofisi za Serikali si duka la wazazi wenu wala mali ya familia zenu. Mkipewa mamlaka ya umma, mnapaswa kuvumilia kukosolewa, kuulizwa maswali na kuwajibika kwa maamuzi yenu. Kama hamtaki kusemwa, kuhojiwa au kuwajibika, acheni hizo ofisi mrudi mkakae na wake zenu, waume zenu na familia zenu. Mamlaka si kinga dhidi ya uwajibikaji. Na hili linamhusu kila mmoja wenu, hususani pia na wewe Msajili
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imechukua hatua dhidi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Faustine Jackson Mafwele, kutokana na taarifa za kuaminika kuhusu kuhusika kwake katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
Hatua hii dhidi yake inatangazwa hadharani chini ya sheria za Marekani zinazolenga kuimarisha uwajibikaji kwa ukiukaji wa haki za binadamu.
https://t.co/gKyKpF2rpk
Zama za Ofisi ya Msajili wa Vyama kuwa mchezaji namba 12 wa CCM FC zimekwisha.
Dola isome alama za nyakati. The writing is on the walls!
Msajili STOP THIS NONSENSE ya kutaka kufuta CHADEMA. Utafutwa wewe, No doubt about this!
Tume ya Chande iliyoundwa na Rais imetoa Taarifa inayosema wananchi wanailalamikia Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kutokutenda haki kwenye kusimamia shughuli za vyama vya Siasa. Badala ya Msajili kuchutama, kuwajibika na kubadilika anarudia makosa yaleyale yaliyopelekea mauaji yaliyoanza Oktoba 29.
Msajili anajua, Watanzania wanajua na Dunia inajua kuwa Kuna ushahidi wa kutosha wa CCM kufanya makosa makubwa kuliko hata ambayo msajili ameituhumu Chadema, hatukuwahi kuona hatua zozote zimechukuliwa na Ofisi hii ya Msajili.
Ofisi ya Msajili ijue WATANZANIA SIO MABWEGE. Tunachukulia tishio lolote dhidi ya CHADEMA ni tishio dhidi ya Demokrasia. An attack to one, is an attack to all.
Iacheni CCM ifanye Siasa za Ushindani dhidi yetu. Nasi tufanye siasa za ushindani dhidi yao.
Acheni kuwa mbeleko ya CCM. Mtaanguka nayo. Ujumbe huu sio wa Msajili tu bali pia ni kwa VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA pia. Kaeni pembeni acheni vyama vya Siasa vifanye Siasa.
Mnataka watu wangapi wafe ili mpate somo?
Siasa zina gharama. lakini gharama ya kukaa kimya ni kubwa zaidi. Mabadiliko hayafadhiliwi na maneno pekee. Yanahitaji kujitoa, uthubutu, na support ya wananchi wenye IMANI na nchi yao.Changia leo kusaidia operation za chama nchi nzima. Tafadhali usiupite ujumbe huu bila kufanya chochote. Just be concerned.
TAFAKARI, gharama wanazolipa walioko mbele ya mapambano haya kwa ajili ya nchi yetu. Fikiria sacrifices, muda, mateso, na jinsi walivyoweka maisha yao rehani kwenye haya mapambano kwa ajili ya Watanzania wote. Je, wewe kweli unashindwa kuchanga chochote kwa ajili ya kazi hii muhimu na bora sana kwa kizazi cha sasa na hapo baadae.
Tafadhali tunakuomba ujali , kwani mchango mdogo unaweza kufanya tofauti kubwa. Pls do something. We need your support. Hatuna ruzuku, lakini tuna IMANI pamoja na wewe. Usiseme mtu fulani atafanya , huyo mtu fulani ni wewe.
Mungu akubariki sana.
#TANZANIA: TLS WATAKA HAKI KWA LISSU KESI YA UHAINI NA YA UCHOCHEZI, WATOA MAPENDEKEZO MAZITO
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (@TanganyikaLaw) kupitia kwa Rais wao, Wakili Msomi @Mwabuk2Boniface leo Mei 11, 2026 amesema wanafuatilia kwa ukaribu kesi ya Wakili mwenzao na Mwenyekiti wa @ChademaTZ2 Taifa, Wakili msomi @TunduALissu anayekabiliwa na kesi ya uhaini pamoja na kesi ya uchochezi.
Mwabukusi amesema kesi hizi zimesimama kwa muda mrefu bila sababu za msingi, amesisitiza Lissu apewe haki yake kuliko kuendelea kusota gerezani bila kesi kuendelea Mahakamani jambo ambalo amesema ni kinyume na sheria.
Zaidi: https://t.co/1GvRY6Izyk
“Kumekuwa na majaribio na vitisho kutoka kwa watawala kunizuia nisiongee. Kuna wakati niliambiwa nizime simu yangu, nisiitumie mpaka (wao) watakapo niambia. Nikawauliza, kwa sheria gani? Kuna wakati nilikaribishwa mahali fulani, nikapigiwa simu na watawala, wakasemam mzee usiendee kwenye huo mkutano. Kwanini? Hauna manufaa. Nikawauliza, nani anaamua hayo manufaa? Nikakataa. Wakawafuata watu walio karibu na mimi ili wanishawishi nisiende, nikakataa pia. Mnakumbuka nilifanya mahojiano hapa na Jamhuri? Wakatoa summary, wakasema watachapisha mahojiano yote, neno kwa neno. Baadae Jamhuri wakanieleza wamezuiwa wasitoe yale mahojiano. Kuna viongozi wanaogopa kuzungumza na mimi, wanatuma ujumbe kupitia mbali huko. Marafiki zangu wanaogopa wakisema nitatekwa au kupewa sumu. Nawaeleza mimi ni mali ya Mungu, ndiye atakayeamua lini ananihitaji.”
— Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Tanzania.