CCM na ninyi mlioko madarakani, mnaelekea mwisho wa aibu na laana ya historia. Watoto wenu wataishi na fedheha ya kulelewa kwa maisha ya dhuluma, na siku moja watawauliza kwa maumivu, “Kwa nini mlitupeleka shule kwa thamani ya uovu? Kwa nini mlilisha familia zenu kwa gharama ya kuua haki na uhuru wa Taifa letu?” Watajuta. Watachukia historia yenu. Watajificha. Watatamani kuondoa ubini wenu katika majina yao. Kwa sababu hamkuacha urithi wa heshima, bali mliwaachia kumbukumbu ya mateso, uonevu, na utawala wa mabavu.
Mlipotumbukiza Taifa kwenye giza la kimya, woga na unafiki; mlipouzika ukweli na kukumbatia uongo; mlipojenga utawala wa hila na mauaji ya kisiasa, mlifanya hivyo mkidhani mnaandika ushindi. Kumbe mlikuwa mnaandika hukumu yenu wenyewe.
Na sasa mmebakiza kuendesha chama chenu kwa mkutano wa dharura kwa njia ya mtandao, si kwa sababu ya maendeleo ya teknolojia, bali kwa sababu hamuaminiani, mnaogopana, na hamna tena ujasiri wa kukutana uso kwa uso. Huu si mkutano bali ni kisingizio cha hofu, ni jukwaa la hila lililofichwa kwenye skrini, ni mkakati wa kudhibitiana badala ya kujadiliana. Mnaendesha chama kama kikao cha usaliti wa kimya kimya, ambapo kila mmoja anaangalia kamera huku akihisi kisu mgongoni. Mmekwepa mkutano wa hadhara kwa sababu mnajua ukweli ungepasuka mbele ya umma wa wanachama. Mmekataa uwazi kwa sababu hofu imezidi hekima.Lakini hebu tukumbushane.Hamkuanza leo kuua demokrasia mliianza zamani.
Wakati viongozi wa upinzani walikuwa wanapigwa risasi, kunyimwa fursa ya mikutano, kufungwa kwa tuhuma za kutungwa, mliimba, mlipiga makofi, na kushangilia kana kwamba Taifa si la wote. Mliamini mna kinga ya kudumu. Mliamini nguvu ya dola ingewalinda milele. Leo hiyo dhambi imewageukia. Leo mnashuhudia chama chenu kikichukuliwa mateka, si kwa kura wala ridhaa ya wanachama, bali kwa matakwa ya cartel za kisiasa. Leo hamna uhuru wa kuamua uongozi kwa heshima, bali kwa hofu. Mnachokiona sasa ni madhara ya mfumo wa kisiasa mlioujenga kwa mikono yenu, mfumo wa kunyamazisha, kudhulumu na kuvunja haki za msingi.Huu ni mwanzo wa mwisho wa chama kilichogeuzwa genge.
Watoto wenu wataenda kuhiji kwenye makaburi ya wanaharakati waliouwawa wakati ninyi mlikuwa madarakani. Wataomba msamaha kwa niaba yenu. Watatamani wasiitwe kwa majina yenu. Watajua walikula matunda ya udhalimu. Watasema, “Wazazi wetu waliisaliti Tanzania.”Mlioanzisha moto huu, msidhani mtauruka moshi wake. Mlioharibu demokrasia kwa mbwembwe na kelele, leo mnalia kimya kimya ndani ya vikao vya siri. Mliofanya siasa kuwa dimbwi la damu, leo mnaogopa hata kupiga kura mbele ya wenza wenu. Mliojifanya miungu wa siasa, leo mnaona aibu hata ya kukutana uso kwa uso. Hii ndiyo gharama ya kuabudu mabavu.
Hii ndiyo bei ya kushangilia maumivu ya wengine. Hii ndiyo aibu ya historia
@SimbaSCTanzania Alafu nyie wapuuzi hamtaka mfanikiwe na hao wajinga wenzenu,habari ya mjini kwa sasa ni NO REFORMS NO ELECTION...huo upuuzi wenu na hayo derby tumewashtukia,MTAANDA VIMBWANGA VYA KILA AINA ILA NRNE NDIO KWANZA IMESHIKA KASI
stupid people here jump around defending police’s brutality against innocent people w/ “my country this, my country that” bs. shut the fuck up you pieces of shit. if you can justify violence against someone just ‘cuz they don’t share your nationality, you’re not a human being!
📌 Pin this!
‼️ZANZIBAR VS TANGANYIKA‼️
Nimewaza na kuna jambo muhimu nimeona
Facts:
👉🏽 Wajumbe wote waliopeleka @ChademaTZ2 mahakamani ni wazanzibari
👉🏽 Ingawa wanadai ugawaji wa rasilimali lakini wanataka shughuli zote za Chadema zisimamishwe mara moja yaani kuPARALYZE chama
Sasa taarifa za ziada nilizowaambia
👉🏽 Chief coordinator ni Salum Mwalimu si mmeona wenyewe ndo anawapa maagizo akina Kigaila pia ye ndo coordinator wa kesi! Tuzingatie kuwa Salum Mwalimu alikuwa hana mahusiano mazuri na Kigaila na Mrema muda wote wakiwa pale sekretariat! Wakatae kama watu hawajaja kutoa ushuhuda 😀 huu urafiki wa ghafla umekujaje!? Tena leo Kigaila anakubali kupewa maelekezo na Salum kama mtoto mdogo “Tusiruhusu maswali!” !! Pesa mwanaharamu!
👉🏽 Maelekezo na pesa yanatoka “kwa Mama” directly na karata kubwa inayotumika kwenye kesi ni UZANZIBARI - walindane hata wakiwa chama tofauti!
Lakini kuna kitu kimenisumbua zaidi
Kwa sasa chama pekee kinachotetea rasilimali za Tanganyika bila kupepesa macho kama kupinga uuzwaji wa ardhi ya wamaasai na Bandari zetu kwa waarabu kupitia Samia Suluhu ni CHADEMA
Hili suala la kesi la kuhujumu CDM litakuwa zaidi ya suala la kubaki madarakani bali pia ni suala la kunyamazisha sauti kuu ili waendelee kuvuna utajiri wa Tanganyika!
Hii kesi si ya CHADEMA tu bali ni suala la Zanzibar vs Tanganyika na inatupa picha mbaya sana! Watu wasikubali kutumika!
Watanganyika amkeni! CCM Tanganyika mmekaa tu mnafikiri mko salama na vijivyeo vyenu? Ndiyo maana tunahitaji #KatibaMpya ile ya Warioba! Tunaambiwa hakuna Tanganyika ila Zanzibar ipo! Huku wanavuna rasilimali zetu kwa jina la Muungano! 🚮
Tujiandae hii vita ina fronts nyingi - tuwe tayari kukabiliana na madhulmat!
Eniwei #TutaelewanaTu
📌 UPDATE PIN THIS‼️
‼️Bunge la Ulaya laleta mtafuruku kwenye njama zao ‼️
Source ameniambia Bosi mwenyewe nyuma ya hawa anatakiwa kujitokeza na kuhama rasmi mapema iwezekanavyo (hata wiki hii ) ili kuua hoja ya Bunge la Ulaya na waseme upinzani uko CHAUMMA na NRNE haina mashiko na Chadema sasa si chama kikuu - so ishu ya Lissu na demokrasia Tanzania haipo tena🙄 hiki kiliamuliwa kwenye kikao jana usiku! Wanavuja kama pakacha!
🤣🤣
Hii sinema nani anawatungia script?? Mwesiga?? Utumbo mtupu!
Eniwei as I said “bye bye” 👋🏽
#NoReformsNoElection
#TutaelewanaTu
✊🏽Shujaa wa #Tanzania@mdudenyagali 🔥
Msifikiri RC Homera na RPC Kuzaga kuwa tuko tayari kumpoteza huyu shujaa! Msiseme amri kutoka juu! Hii ni JINAI!
Hii kesi hamuwezi kuikwepa kwa sababu waliomshambulia na kumbeba Mdude ni maaskari polisi walijitambulisha hivyo na ushahidi wa wao kumtafuta kupo pia tumeshadhihirisha kuwa polisi ni watekaji tarehe 24 April
@SuluhuSamia damu hunena na utalipa ila baadaye msije kujitilisha huruma maana ukatili wenu lazima uwajibishwe
Mrudisheni Mdude akiwa salama
#FreeMdude
#FreeMdudeNyagali
Ameuwawa mbele yetu,
Muda wote alikuwa anawalaumu Polisi kwanini wanakamata watu? Wakasogea Polisi wawili wenye Mbwa wakali, wakaanza kumng'ata, wakati akijihami Polisi wakamzingira ,wamempiga sana na virungu, akaanguka chini, akaanza kung'ata meno aridhini, baadae akatulia.
🚨🚨BREAKING NEWS🚨🚨‼️
It’s official 👊🏽🔥
@TunduALissu has refused to take part in the fake virtual meeting set up by @judiciarytz
Tundu Lissu amegoma kushiriki kesi kwa njia ya mtandao!
God bless you Tundu Lissu
@SuluhuSamia you have created a CRISIS!
Unajua haki zako! Hawawezi kukiuka haki zako hivi
#FreeTunduLissu
#FreeTunduLissuNow