Je, wale waliopoteza viungo vyao vya mwili? Waliokatwa masikio? Waliogongwa misumari miguuni? Waliofanya ukatili wa kutisha kama kulawitiwa wakati wakimtetea Mzee MBOWE akiwa mbunge wa HAI, wamepewa faraja au kuombwa msamaha? Wengine walilazimika kutelekeza familia zao na kuwa wakimbizi kwa kuhofia usalama wao. Hali hii inajenga picha kuwa Mzee MBOWE ameweka maslahi yake binafsi mbele na kusahau gharama kubwa waliyolipa wafuasi wake. Hii ni dhihaka kwa watu wote ambao waliwahi kuamini katika njia zake. Hii inatuogopesha ambao tumewahi kumpambania hadharani. Hata hivyo, SABAYA anatakiwa kuomba msamaha mwenyewe, siyo kuombewa msamaha. Kimsingi, msamaha ni jambo la kibinafsi na la kimaadili kati ya mtu aliyekosea na yule aliyekosewa. Msamaha wa kweli unahitaji sauti ya mkosaji mwenyewe.
Leo Dodoma, script iliyobaki ni kumsifia Mama. Wanatembea nayo kwa bidii. Lakini ukweli ni huu: umma hauna muda na kinachoendelea Dodoma. Japo wameamua kumpigania aliyewaweka bungeni sio wanaowawakikisha bungeni.
Hatari ninayoiona ni kubwa zaidi. CCM ikishindwa kabisa ku-set agenda, ikashindwa kufanya diversion au deception, umma uta-set agenda yake yenyewe, na hiyo agenda itakuwa na nguvu kama Agenda ya No Reforms No Election ambayo hata ukamfunga muasisi wa Agenda umma haugeuki nyuma. Na siku hiyo ikifika, hali itakuwa mbaya zaidi kwa wanaojiita watawala.
Lakini kwa nini CCM inazidi kupoteza ushawishi kila uchao?
Kwa sababu imeshindwa kujibu maswali magumu, inaongea lugha ambayo umma hauiongei, wakati inawaambia Gen Z hamjui tuliko toka na Genz wanawaambia hamjui tunako kwenda
.
Maswali maguku kwa CCM yasiyo na majibu ni haya:
1. Tarehe 29.10.2025 waliuawa watu wangapi?
2. Miili iliyopotea iko wapi ili ndugu zao wazike?
3. Walioua wamechukuliwa hatua gani?
4. Ni lini serikali itasema: βtulikosea, tunatubu, tusameheni, turidhiane, tusonge mbele kama taifa?β
Bila majibu ya maswali haya, wasahau kabisa ku-set agenda ya umma.
Simbachawene akajaribu kuiga staili ya Mzee Kinana, akasema baadhi ya polisi ni mizigo, wanaonea watu, hawafuati sheria. Akasahau jambo moja muhimu.
polisi sio vichaa; wanatekeleza script ya mtawala aliyepo.
Ndipo Simbachawene bwana, kikamramba. Namshauri akitika kipindi hiki alicho nje ya baraza la mawaziri autumie kusoma kitabu cha Robert Green cha 48 Principles of Power. Kanuni ya kwanza tu inasema, "Never outshine your master"
Hatutaweza kusahau bila uwajibikaji.
Hatutaweza kusonga mbele bila ukweli.
Taifa linahitaji uponyaji wa kweli, sio propaganda.
Share Zaidi
Wasalaam,
John Pambalu
Mwalimu wa Zamu
2/2
Mwaasiasa aliyegoma kuwafanya Watanzania kama Kuku au Mbuzii kwa watawala Dharimu.
Mwaasiasa ambae katika miaka yake yote amefundisha kwa vitendo namna Taifa linapaswa Kuongozwa na watu wenye uwezo wa kufuata sheria
"A man with unshakable good character Hon" @TunduALissu .
Nawashukuru sana wote mlionitakia kheri kwenye birthday yangu na wote mlionipa zawadi.
Nimeona upendo wenu kwangu kwa kweli sina cha kuwalipa zaidi nawaombea Mungu awabariki sana kwa baraka za rohoni na mwilini.
Nawapenda sana wapendwa wangu.π₯