Juni 08 kila mwaka ni siku ya Kuthamini rafiki yako wa karibu ambayo mnaongea mambo mengi ya siri bila mtu mwingine kujua.
Kila mtu ana rafiki yake wa karibu, leo ni siku ya kuthamini urafiki wenu.
Bei mpya ya Mafuta kwa Mwezi Juni, 2026.
Dar es salaam
Petrol 4,086
Diesel 4,333
Dar es salaam Petrol imeshuka kwa shilingi 29 na Diesel ikipanda kwa shilingi 85,
Shuka chini kuona na bei ya mikoa mengine.
Wasafi wawe makini sana na watu wanaowaalika kwenye kipindi cha The Switch pale lasivyo TCRA wataruka nao.
Mose Iyobo leo katamka neno sio zuri kwenda hewani.
Mgeni wa pili huyu wanamwambia aombe radhi
Niliwahi kuwafungisha watu ndoa kupitia post yangu ya instagram!!
Na leo wamenambia wamepata mtoto wa kiume wanempa jina “Roma”
Ilikuwa hiviiiiiiii…..
Kuna siku nilipost andiko fulani Instagram, lile andiko lilileta sana mjadala kwenye comments!!
Umewahi kuona unapost kitu then wanatokea watu wanaanza kubishana wao kwa wao kwenye comments za post yako!?
Unakuta post ina comments 500, ila 100 ni za replies zao!!
Basi ndivyo ilivyokuwa, kuna mchizi na sister du flani hawakuwa hata wanajuana wakaanza kubishana kuhusu nilichoandika….sikuwazingatia hata!!
Miaka ikapita, siku moja
yule mchizi akanicheki DM na kunisimulia.
Kumbe walivyobishana sikuile kwa comments, wakahamia DM, baadae wakawa marafiki, baadae wakaja kukutana…..wakatongozana.
Binti akatepeta….mchizi akaishi!!
Ndio ile DM alikuwa ananihadithia wamefunga ndoa na makutano yao yalikuwa kwenye Post yangu!!
Leo kanambia wamepata mtoto wa kiume wamemuita “Roma” ❤️
kama kumbukumbu ya mtu aliyewakutanisha!!
“Kazi ya viongozi wa dini si kuwa tawi la serikali.
Na kazi ya serikali si kuwa mmiliki wa dhamiri za viongozi wa dini.
Mamlaka zinahitaji kusikia ukweli
hasa ule wasioutaka kusikia.
Kwa sababu history inaonyesha:
taifa huwa hatarini sana pale ambapo:
watawala wanataka kusikia sifa pekee,
na viongozi wa dini wanaogopa kusema ukweli., badala yake wanakuwa public relations officers wa serikali .”
Rev Peter Msigwa
JKT imesema vijana waliomaliza Form Six wanaende mafunzoni kwa lazima, haina maana kama watapita mitaani kukagua 😁 ila apa umewekwa mtego,
Uko baadae huwezi jua kuna vitu vijana watashindwa kufanya bila cheti cha JKT
Washaurini vijana waende jamani ni muhimu sana.
Taarifa: Ili kumuunga mkono Mwenyekiti wetu Lissu na struggles zake gerezani, nimeamua kumuiga style yake mpya ya nywele…Sitachana wala kunyoa nywele zangu mpaka atoke jela akiwa HURU✌🏾✌🏾
#LiMwenyekiti#KatibaMpya#FREELISSU
Ili ujiunge na chama cha siasa inatakiwa uangalie, itikadi yake, sera zake, uongozi wake, demokrasia ya ndani, uwazi. N.K
Lakini Yericko Nyerere yeye alijiunga na CHADEMA kwa mapenzi yake kwa Mbowe. Yericko alisahau kuwa jukumu la kumpenda Mbowe lilikuwa la mke wake
Ulinzi wa taifa si kulinda mipaka pekee.
Ni pia kulinda misingi inayolifanya taifa libaki taifa.
Taifa hulindwa si kwa bunduki tu, bali pia kwa:
Taasisi imara,sheria zinazoheshimiwa, mahakama huru, bunge lenye uwezo wa kuisimamia serikali, uchaguzi unaoaminika, na wananchi wanaoamini kuwa haki inaweza kupatikana bila nguvu wala hofu.
Kwa sababu mipaka inaweza kubaki salama…
lakini taifa ndani likaanza kuoza.
Mahakama zikikosa uhuru,
bunge likigeuka muhuri wa kupitisha kila kitu,
taasisi za umma zikianza kuogopa watu kuliko sheria,
ndipo taifa huanza kupata ufa wa ndani ambao ni hatari kuliko adui wa nje.
Historia inaonyesha:
mataifa mengi hayakuanguka kwanza kwa kuvamiwa
yalianguka pale ambapo taasisi zilianza kudhoofika, ukweli ukaogopwa, na mamlaka ikawa kubwa kuliko sheria.
Ulinzi wa taifa wa kweli ni kuhakikisha:
Hakuna mtu aliye juu ya sheria,taasisi zinafanya kazi bila hofu,na madaraka yanabaki kuwa dhamana ya wananchi, si mali binafsi ya watawala.
Kwa sababu mwisho wa siku:
jeshi linaweza kulinda mipaka,
lakini ni taasisi huru zinazolinda roho ya taifa.”
Hatimae nimerejea uraiani baada ya miezi 6 katika kuta za Gereza R/Bunda.
Mateso yote niliyopitia tangu 01/11/2025 - 22, Mei 2026 yamenipa nguvu ya mapambano zaidi.
Sasa basi ili kuiondoa CCM Madarakani lazima tuwe na Vijana Watundu, Vijana Wakorofi na Vijana wenye Hasira.
“Msimamo wa mwanadamu haupaswi kuwa gereza la dhamira yake.
Kuna nyakati ambapo ukimya huwa mzigo kuliko maneno.
Sidai kuwa mimi ni mkamilifu, lakini nimeamua kutii dhamira yangu kuliko kuigiza consistency isiyo na ukweli. Si busara kushinikizwa kuonyesha “uanaume wa kisiasa” kwa kubaki sehemu ambayo dhamira yako haiwezi tena kutulia”