VIDEO:
Safari ya maisha ya Bibi Janeth Yohana (56), mkazi wa Ngo’ngona Jijini Dodoma, imejaa tabu, dhiki na mateso makubwa yasiyoelezeka. Bibi huyu amejikuta akibeba jukumu zito la malezi ya wajukuu wake wawili baada ya kupoteza mtoto wake wa kike aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kujifungua kutokana na changamoto za mshono.
Miongoni mwa wajukuu hao, mmoja ana umri wa miezi minane ambaye aliachwa katika umri mdogo na sasa anakabiliwa na changamoto ya kiafya ikiwemo mwili wake kutokwa na vidonda sehemu mbalimbali. Hali hiyo imezidisha maumivu ya maisha kwa Bibi Janeth ambaye hana uwezo wa kumhudumia ipasavyo mjukuu wake huyo.
Akizungumza na Jambo TV, Bibi huyo amesema mtoto huyo bado anahitaji maziwa ya dukani kama chakula muhimu, lakini hali ngumu ya maisha imemfanya ashindwe kuyapata mara kwa mara, hali inayosababisha mtoto kulala njaa. Aidha amesema hajawahi kupata fursa ya kumfahamu mwanaume aliyemzalisha marehemu binti yake wala kupata msaada wowote kutoka kwake.
Kwa sasa Bibi Janeth anaishi na wajukuu wake katika nyumba ya kupanga, lakini tayari amepewa siku saba za kulipa kodi ya nyumba yenye thamani ya shilingi elfu kumi na tano, vinginevyo atalazimika kuondoka. Hali hiyo inaongeza hofu na sintofahamu juu ya hatima ya makazi yao.
Kutokana na mazingira hayo magumu, Bibi Janeth ameomba msaada kwa Watanzania wenye moyo wa huruma pamoja na Serikali ili apatiwe chakula kwa ajili ya wajukuu wake na sehemu salama ya kuishi, ili watoto hao wapate fursa ya kuendelea na maisha. Kwa yeyote atakayeguswa kusaidia, anaweza kuwasiliana na Jirani wa Bibi Janeth Yohana kupitia namba ya simu 0650 938 253
@malik_hubby14@mangekimambi Hili ndo jila lao kabisa “Gen Z zero brain”
Nikisikia mtu anasema hiki kizazi et kina akili nyingi uwa natamani kulia aisee.
Hiki ni kizazi chenye hakina akili kuliko vizazi vyote duniani.
@JayleenRickie Wengi ni vile walivyolelewa.
Mfano n mm, kipindi nakuwa nilikuwa nikikatazwa sana kwenda kwa majirani hata ningekutwa na watoto wa majiran nilikuwa nachapwa sana. So niliamua kukaa mwenyewe hadi leo hii kuchangamana na watu ni tabu sana puls aibu hata shule sikuwa na rafiki.
@MacAlpho@KShengelo@Awesially 😂 nimeacha upumbavu mkuu maana nimehesabu idadi ya vituo vilivyopo Kisesa hadi Buzuruga havizid hata 5 so nilikosea naisi hakuna hata 1 kilichomwa.
Nisamehe🙏
@LKingker@godbless_lema Kweli kabisa.
Hiki kizazi kinaitwa kizazi chenye akili lkn ukichunguza kwa umakini utagundua ni kizazi kisichokuwa na uwezo wa kudadavua mambo.
Tz bado ni nchi yenye myanya mingi ya kuwezesha vijana kutoboa ni vile hatujagundua hilo. Vijana tuamke tuwakatae wachochezi tunapotea.