‼️HATUTASAHAU WALA KUSAMEHE BILA UWAJIBIKAJI‼️
Makambi ya jeshi pia yamefikiwa na satellite na inaonekana palikuwa bize sana! Mabasi yalijaa na tukumbuke viongozi waliambiwa jioni wapeleke familia zao kwenye makambi ya jeshi! Ndo ubize huu nadhani! Maana walishajiandaa kuua mitaani watakavyo! Walionusurika mauaji halaiki wakiwa mtaani wamshukuru Mungu ILA tusiache kudai Haki! Na JW mjipime sana maana uwajibikaji unakuja soon na mtatueleza kila mmoja wenu alilindaje wananchi kama mlivyoapa? Who knew what, to what extent, how much ?
Kwa teknolojia ya sasa ni suala la muda ila kila kitu tutajua hata jeshi haliwezi kujificha!
#TutaelewanaTu #SamiaMustGo
FUNGA MWAKA NA TUNDU LISSU
Wengi tulitamani kwenda gerezani Ukonga kumsalimia Mhe Tundu AM Lissu, lakini ilishindikana. Hatukuruhusiwa kuingia gerezani. Tuliishia getini, tukarudi nyumbani kinyonge.
Dola imewekwa utaratibu mgumu sana, na kuanzia Desemba 5 hadi leo, hali imekuwa mbaya zaidi.
Maisha ya upweke na mateso gerezani ni magumu sana. Na Mhe Tundu Lissu anapitia hali hii ya kutengwa dunia – haoni jua wala nuru, kwa miezi 9 sasa.
Hii imeathiri hata yeye kufikia huduma za kijamii, si tu chakula, bali pia taarifa za familia yake, Chama chake CHADEMA, na hata hali ya kisiasa nchini – ikiwemo kusoma kupitia magazetu au mazungumzo na ndugu na jamaa zake.
Ili kumuunga mkono katika giza nene alilomo, tunakualika ushiriki “MASAA 48 YA FUNGA MWAKA NA TUNDU LISSU (Baba wa Gen Z).”
Gen Z wanafunga mwaka na Mtetezi weo, na sisi Watanzania tuungane kumtumia salamu za mwisho wa mwaka, tumtie moyo ili aanze Mwaka mpya kwa ujasiri mkubwa.
Kama ambavyo Mhe Lissu amejitoa kwaajili ya Taifa letu, tunalazimika kumkimbilia katika wakati ambao anatuhitaji zaidi.
Tuioneshe dunia maana halisi ya “NGUVU YA UMMA” kwa kuchangia chochote ulicho nacho.
Mwenyezi Mungu akubariki sana.
ASANTENI SANA.
MaCCM ni waongo sana. Kifo cha nyani…?
1. Samia alikutana na kaimu balozi wa Marekani na kusema mambo yapo safi kabisa. Marekani ikatoa tamko la ku-review uhusiano wetu kwa sababu ya mauaji waliyo yafanya na ukandamizaji wa dini na haki za binadamu.
2. Kombo akaenda kupiga picha na wabunge wa Marekani na kusema mambo yapo safi kabisa— kesho yake Marekani ikatupig partial ban ya visa
3. Mwigulu akakutana na Fr. Kitima na kusema mambo yapo safi kabisa na TEC— Fr. Kitima akatoka na mahojiano na kusema maCCM yameua watu wengi na kuwalazimisha wauguzi wao wawapeleke watu wenye majeraha ya risasi mochuari wakiwa wazima
4. Hii ya mwisho na Jaji Warioba, Samia amepiga naye mapicha kama yote kuaminisha umma Warioba amekubaliana na hali ya mauaji. Leo, Mzee Warioba kachana mkeka na kuwaambia wameua Watanganyika wengi kuliko Idd Amini Dada.
Kifo cha nyani— Miti yote huteleza
#SamiaMustGo #TanzaniaMassacre
MKAKATI WA IDD AMIN MAMA NA WASHIRIKA WAKE KUELEKEA DISEMBA 9, 2025.
Tumejulishwa kwamba kuna mpango mbaya sana umepangwa na umeanza kutekelezwa dhidi ya wapigania Haki nchini hasa wale ambao wanaonekana wana mrengo wa CHADEMA ili waje kuwatia hatiani kwa makosa ya Uhaini na Ugaidi.
Mpango uko hivi zimeandaliwa namba za simu nyingi za kigeni kutoka nchi za Uganda, Congo, Zambia, Msumbiji, Burundi, Rwanda, Malawi na Kenya.
Hizi namba zitakuwa zinawapigia simu za kawaida au kuwatumia watu ujumbe mfupi kupitia Whatsapp au kupigwa moja kwa moja kupitia Whatsapp call ambapo watumiaji wa namba hizi Watajifanya ni Watanzania ambao wanaishi kwenye izo nchi na wengine ni raia wa izo nchi tajwa.
Wakishakupigia wanaomba uwasiliane nao kuhusu namna wanavyoweza kusaidia Katika maandamano ya Disemba 9, 2025.
Lengo lao ni kuweka Record nzuri ya mawasiliano kati yao na mtu/watu waliowapigia au kuchat nao ili baadaye mawasiliano hayo yaje kutumika kama ushahidi katika kesi zitakazofunguliwa baada ya Disemba 9 ambazo ni kesi za Ugaidi na Uhaini dhidi ya watu ambao watafanikiwa kuwaingiza mkenge.
Watu hao wanapowasiliana na wewe ujumbe wao ni huu.
1. Wanataka Ushirikiano kati yako na wao Kwenye maandamano ya Disemba 9, 2025.
2. Wanasema wanataka kufadhili fedha ili kutimiza lengo la maandamano kwamba watafadhili fedha zipitie kwako direct ili kuandaa maandamano hayo.
3. Wanauliza namna utakavyowasaidia kuingia nchini kushiriki maandamano kwamba utawasaidiaje ili waweze kuingia nchini kwa njia za panya yani njia zisizo rasmi.
4/ Watakutaka utoe orodha ya vitu au taasisi zinazotakiwa kufanyiwa uharibifu wakati wa maandamano.
Sasa ni muhimu sana kila mmoja wetu akachukua tahadhari maana kwenye vikao vyao wanadanganyana kwamba Watanzania wengi wananjaa so wao wanaamini wakitumia ushawishi wa pesa ni rahisi kuwanasa watu wengi.
Na watu ambao wako targeted sana kwenye mpango huu ni Wanachama na Viongozi wa CHADEMA ili mwisho wa siku CHADEMA ndo ije kubebeshwa msala wa kuhusishwa na vitendo vya Ugaidi na Uhaini maana baada ya maandamano ya Oktoba 29 walihangaika sana kujaribu kuihusisha CHADEMA na matukio yote yaliyotokea kwenye Maandamano ya Wananchi lakin walikosa ushaidi.
Nimeambiwa mpango huu tayari ushaanza kutekelezwa tangu siku ya Jumapili yani Novemba 23, 2025.
So kwa kuwa tumeshajua mipango yao mapema tuishi kitaalam kila mmoja achukue tahadhari, Hakikisha hauingii au kuingizwa kwenye huu mkenge.