@shalha187 Ushauri wa bure akaape kubadilisha jina kuepuka kuwa bullied. Sometimes jamii huwa too emotional than rational matokeo yake ndio kama hivi. Sasa binti mdogo kama huyo anaunganishwa kwenye mambo asiyoyajua
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 129
Anaitwa Mh. Lissu.
Anasimama na kusema naomba na mimi nitoe Rejoinder yangu baada ya kuwasikiliza Mawakili wa Serikali.
Nitafuata utaratibu huo huo ambao wao wameufuata walipokuwa wanajibu mapingamizi yangu.
Kuhusiana na hoja ya kwanza.
Je hizo video zilichezwa Kisutu?
Je nyaraka zingine zote zilisomwa ukiaichia witness statement. Je video zilionyeshwa?
Waheshimiwa majaji mashauri ya Kisutu yalikuwa ni hadhara yalifanyika hadharani members of the public pia walikuwepo.
Amesimama Katuga anasema huko kwingine hatukwenda, tuliishia kwenye Court Records pekeee. Tusimuache aende mbali zaidi.
Lissu Mh. Jaji video hazikuchezwa na kama Wakili wa Serikali anasema hadharani kuwa video zilichezwa maana yake tuna shida kubwa sana.
Waheshimiwa Majaji, je ni kweli kwamba hii rekodi ya Kisutu haikuwa impeached? Wakili anasema kwamba record ya Mahakama haiwezi kuwa impeached?
On the question of record: kuna ruling mbili za Mahakama hii juu ya integrity ya hiyo record mtakumbuka kwamba record hii haikusema chochote juu ya majina ya mashahidi niliowataja.
Anasimama tena Katuga anasema hii ni Rejoinder tunaona anaanza kuingiza vitu vipya tena.
Katuga anaogopa kuna mambo kusemwa. ๐ anasema vitu vipya.
Mhe. Lissu anasema hii rekodi nimeichallenge mara kadhaa.
Hiyo page 92 exhibit zimekuwa listed na page 93 inasema the records has been read out.
Hiyo kuandika hivyo haina maana ukweli wangu unabadilika. It doesn't change my position.
Sitaki kukubali jambo ambalo ni uongo.
Mimi sipendi uongo na ukweli wa kwamba video haikuchezwa kisutu utabaki kuwa hivyo hapa Duniani na hata Mbinguni.
Siwezi jidanganya au kutenda dhambi ya namna hiyo namuachia Katuga pengine yeye amezoea dhambi na kudanganya mambo ambayo sio ya kweli.
Video hazikuonyeshwa anasema zimeonyeshwa tena kwa ujasiri wa kusema hadharani na hapa mahakamani.
Niendelee sasa.
Katuga anasema pia kuwa mimi nilisema kuwa sikatai maneno yangu ya tar. 03/04 pale Makao Makuu ya Chama.
Nilichosema mimi ni kuwa hizi video haziko sahihi kupokelewa kwasababu hazikuonyeshwa Kisutu.
Kwa vile hazikuonyeshwa Kisutu haziwezi kuonyeshwa hapa, zilikuwa listed YES. Hazikuonyeshwa na haziwezi kutolewa hapa Mahakama.
Kuhusu mimi kusema sina shida navyo swali linabaki kuwa haviwezi kupokelewa kama havimeet masharti ya kisheria.
Amerejea mashauri ya Mahakama ya rufani wakati natoa hoja yangu. Shauri la Sharif Mohamed @Athuman, Lemina Omary Abdul na Musa Ramadhani Magai.
Hakuna kesi mbili zinazofanana kwa kila jambo. Kitu muhimu what is the principle ambayo inatokana na mashauri hayo yote matatu.
Principle ni kwamba nyaraka na vitu vyote vinavyotajwa katika mashauri kabidhi kama ni vya kusomwa visomwe na kama ni vya kuonyeshwa lazima vionyeshwe kwahiyo ulitakiwa kuonyeshwa huu ushahidi kule Kisutu.
Mahakama ya rufani ilisema the issue is not authenticity basi issue ni compliance of the law.
Kwenye hoja hii ya kwanza videos ambazo hazikuonyeshwa Kisutu haziwezi kuonyeshwa hapa.
Naomba sasa niende kwenye hoja ya pili.
Kwenye ushahidi wa shahidi ambae anadai yeye ni mtaalamu.
Kitu cha kwanza ni taarifa yake ya kitaalamu na sio alichokifanyia kazi.
Katuga amesema kwamba hakuna sheria mahususi inayolazimisha tuanze na Report badala ya kuanza na video iliyochunguzwa na alisema inantegemea na mazingira ya kesi.
Hajasema mazingira gani ya kesi hii ambayo yanataka ianze report na baadae video.
Sasa katika kesi hii tunayo report ya uchunguzi asa ripoti ndio inayo estabalish genuinely ya hicho kilichofanyiwa uchunguzi.
What is the legal logic ya kutanguliza video na kuacha report ya mtaalamu.
Ukisoma vifungu 216 hadi 223 vya CPA vinasema kuhusu ripoti na sio video na ndio maana ya mfano wangu wa mkokoteni na punda.
Ushahidi wa kitaalamu unahitaji kuletwa na mtaalamu na baada ya ushahidi kuo kuletwa ndio utazingatiwa.
Part 130 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Dear @ACTwazalendo, mtamuwia radhi #Jasusi endapo atawakwaza lakini haiwezekani ku - #LindaKura huku watu WANATEKWA. Mnaenda kushiriki uchaguzi haramu ambao mnajua fika mtadhulumiwa haki zenu... but hey who the heck is Jasusi to tell you how to run your affairs?