VIDEO:
Mwenyekiti wa zamani wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ameitaka Serikali kukiri ukweli na kuwaachia wafungwa wa kisiasa waliopo magerezani ili kuponya majeraha ya watanzania ambao wana maumivu makubwa.
Akizungumza wakati wa salamu fupi za familia katika ibada ya mazishi ya Mzee Mtei, Mbowe amewataka Waziri Mkuu pamoja na viongozi wengine wa serikali kutambua kuwa taifa bado lina maumivu makubwa.
“Nitakuwa mnafiki nisipolisema hili. Maendeleo mnayoniambia serikali inasimamia ni jambo jema, lakini hakuna jambo la maana na la muhimu kuliko uhuru wa watu katika nchi yao,” amesema Mbowe.
Ameongeza kuwa viongozi wa CHADEMA waliopo magerezani wanaendelea kuumiza mioyo ya Watanzania, akisisitiza kuwa magereza yamejaa viongozi wa kisiasa ambao walipaswa kuwa huru, uraiani, wakishiriki na kuona matunda ya nchi yao.
“Njia bora ni kurejesha uhuru wa watu, haki za watu, na serikali ikiri ukweli pale ilipokosea,” amesisitiza Mbowe.
Aidha, amesema kuwa kwa jinsi anavyomfahamu marehemu Mzee Edwin Mtei, alikuwa ni mtu mwenye misimamo thabiti, asiyeyumba na aliyekuwa akitekeleza kwa vitendo ahadi alizoamini.
Kijana Jovin Kaaya, aliyekuwa akimbeba mgongoni mwenzake Baraka Chacha wakati wa kesi yao ya uhaini Mahakamani, ameeleza kupokea mchango wa zaidi ya Shilingi Milioni 10 kutoka kwa Watanzania, baada ya kitendo chake cha huruma kuwagusa wengi mitandaoni.
Jovin alivutia hisia za wengi baada ya kuonekana akimbeba Baraka Chacha, aliyekuwa hawezi kutembea kutokana na kuvunjika miguu, jambo lililoibua wimbi la wananchi kujitokeza kumchangia fedha.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Jambo TV, yaliyofanyika jana nyumbani kwao, eneo la King’ori, mkoani Arusha, Jovin amesema hadi sasa amepokea jumla ya Shilingi Milioni 10.8.
Ametumia fursa hiyo kuwashukuru Watanzania wote kwa kumuonesha upendo na kumthamini, akibainisha kuwa hakutarajia kuchangiwa fedha yoyote kwani alichokifanya kilitokana na upendo wa dhati na huruma kwa mwenzake.
“Nimechangiwa hadi sasa kiasi cha shilingi milioni kumi na laki nane. Nawashukuru sana Watanzania wote walionichangia, pamoja na wale waliokuwa wakinipigia simu kuniambia walikuwa wakiniombea. Nawashukuru sana kwa maombi yao na msaada wao,” amesema Jovin.
Juzi,tarehe 4 Dec 2025,nchi za Rwanda na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, zimesaini mkataba wa amani unaelenga kumaliza vita vilivyodumu Mashariki ya Kongo kwa zaidi ya miongo sita
Mkataba huu unaitwa Washington Accords kwa kuwa yamefanyikia nchini Marekani mbele ya rais Trump
Sisi kama kanisa ni wahanga, tulishapewa tahadhari tutapotezwa, hatupuuzi.
Ametekwa Padri Jordan Kibiki Mafinga.
Ametekwa Padri Padre Camillus.
Tarehe 26 Novemba 2025 juzi mwanafunzi wa usista ametekwa Mwanza.
Tusikilizwe ama tusisikilizwe tutaongea.
Fr. Charles Kitima
“Is there a more important undertaking than to defend the defenseless and to be a voice of the voiceless?”
Rabbi Harold M. Schulweis
“Kuna jambo muhimu zaidi ya kuwatetea wasio na mtetezi au kuwa sauti ya wasio na sauti?”
@bonifacemwangi@TitoMagoti@MariaSTsehai@MpaleMpoki
Uzuri Mungu yupo upande wetu, lipress lao la Jana la mchongo limepigwa kaputi, kwa sababu ya agenda walizozipenyeza wenyewe!
Vijana wa sikuhizi sio kama zamani wanajua wanachokisamia, na wanajua kila kitu!
Tuendelee kupuliza wakuu, mali inazidi kuonekana!
@Advocate_Jebra "Charity begins at home"
Hayo wanayolilia huko waanze kwanza kuyafanyia kazi nyumbani kwa kusikiliza nini wananchi wanataka, vinginevyo wasituletee jangwa kwa kumaliza miti kutengeneza karatasi.
Kumbe mnajua umuhimu wa haki ya kusikilizwa!!
Mngeomba amani kwanza sio haki ya kusikilizwa!! Si amani kwanza, haki baadae? Kwanza kwanini mnataka kujieleza kwa watu wanaotuonea wivu?
@Advocate_Jebra "Charity begins at home"
Hayo wanayolilia huko waanze kwanza kuyafanyia kazi nyumbani kwa kusikiliza nini wananchi wanataka, vinginevyo wasituletee jangwa kwa kumaliza miti kutengeneza karatasi.
VIDEO:
Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Michael George Mabuga Msonganzila, amewataka waumini na viongozi wa dini nchini kutokubeba jazba wala kujiingiza katika mijadala ya matusi, lawama na kejeli inayoibuka mitandaoni na kwenye mikutano ya kijamii, akisema kuwa njia ya Kristo ni ya upole, uvumilivu, huruma na kutanguliza haki.
Akizungumza kufuatia mfululizo wa matamko kutoka taasisi kadhaa za Kikristo na Kiislamu kuhusu matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu, huku baadhi ya kauli zikiishambulia Kanisa Katoliki kwa kile kilichoelezwa kuwa ni uchochezi dhidi ya amani ya nchi, Askofu Msonganzila amesema kuwa migogoro na kejeli haviwezi kuizima nguvu ya ukweli.
“hamna sababu ya kuijibu, ni kuinyamazia tu wakati mwingine watu wakisema sisi tumeenda shule sio zamani, kwani kwenda shule ni shida? Shida ni kusoma, shida ni kuelimika, sasa kuzozanazozana katika misingi hiyo haina haja- ni kunyamaza kama Kristo aliyedhihakiwa: Wewe si ni mwana wa Mungu Jiokoe basi nafsi yako, Nyamaza kimya endelea kusali”, amesema.
Askofu Msonganzila amesisitiza kuwa nguvu ya maneno ya kupotosha haiwezi kuzidi uzito wa maadili, utu, na dhamira njema ya Kanisa, akionya kuwa matusi na vitisho ambavyo vimekuwa vikitolewa haviwezi kubadilisha msingi wa imani wala wajibu wa viongozi wa dini kusimama katika kweli.
“Mahangaiko yakitokea ndugu zangu tusiogope kwa sababu ndio Kristo amepitia njia hiyo, Kanisa Katoliki linaweza likateseka kwa njia za namna hiyohiyo na matishio mbalimbali: umemwaga ugali tutamwaga mchuzi, tutawakatakata- tusiogope Mungu yupo”, ameeleza.
Ameongeza kuwa ufalme wa Mungu haujengwi kwa hasira, vitisho au ubabe, bali kwa misingi ya huruma, mapendo, upatanisho, haki, unyenyekevu na uvumilivu.
“Ufalme wa Mungu ni ufalme wa huruma na mapendo, haki, upole, upatanisho, tukiteseka kwa njia hiyo na tuteseke lakini haki na amani, upole na unyenyekevu na upatanisho ndio ziwe sare zetu, tumsifu Yesu Kristo”, ameeleza.
Kauli ya Askofu Msonganzila imekuja wakati ambapo mjadala kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika kueleza ukweli wa kijamii na kisiasa umeendelea kushika kasi, huku baadhi ya taasisi za kiimani zikitoa matamko yanayopingana kuhusu misimamo ya Kanisa Katoliki na makundi mengine ya kijamii kuhusu mwenendo wa uchaguzi na matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.
“An unnecessary appointment”
Kwanza hatuitambui hii serikali haina uhalali!!
Na hata kwa mfano tuki-assume otherwise…..
Moja ya kitu kinazidi kuwafelisha ni kutokujua kuzifanya siasa!!
Ni kama hamsomi alama za nyakati,
Ni kama hamuwezi kucheza na atmosphere ya nchi!!
Either muhusika mkuu au wanaomshauri
wanamuingiza chaka bovu!!
Hakukuwa na haja wala ulazima wala umuhimu wa huu uteuzi wa binti huyu
HASA KATIKA NYAKATI HIZI!!
Yapo mambo mnayafanya ni too obvious , na ndiyo yanakwenda ku-trigger HASIRA na CHUKI za wananchi.
Hasa kwenye kipindi hiki ambacho tayari
mna makashfa ya ufisadi na upigaji toka kwa mtoto mwingine ambaye hata hajakuwa kiongozi bado!!
Kwamba kitu kama hiki hamkukiona?
Washauri waliomzunguka hawakuona?
Hawakujua ni kitu hakiendi kupoza machungu ya raia bali kuongeza hasira na chuki?
Otherwise kimefanyika kwa kiburi na jeuri tu na kukomoa watu kwamba ndio mmeamua hivyo na raia hawana cha kuwafanya!!
Then raia wakikusanya hizi hasira
na waka-take action wao wenyewe,
mnaanza kutafuta mchawi kwamba wameshawishiwa na watu toka nje!!
Wakati wachawi ni nyie wenyewe mmeenda na kiberiti sheli mnachochea moto!!
Mbona hili lingeweza kuepukika tu!!
Mtu anayeijua siasa asingefanya hivi nyakati hizi!!
Mwanasiasa mzuri angeacha papoe kwanza then angekuja kumteua huyu binti yake hata December 2026 huko au 2027!!
inakuwa ngumu hata kwa raia kuunga dots.
Mnafanya vitu obvious sana either kwa kutokujua au jeuri za madaraka!!
Mnatujaza hasira wenyewe then tukichukua hatua mnatuita wachochezi tunatumika na watu toka nje!!
Kumbe nyie ndio wachochezi, nchi iko kwenye joto, hasira, chuki
na bado mnakoleza kuni mnajaza ukoo kwenye teuzi mle keki ya taifa familia moja!
HAMSTAHILI KUTUONGOZA!!
HAMNA UHALALI HUO!!
Kwa watanzania wote hasa waliokufa wakitetea nchi yao, Mwenyezi Mungu awape Pumziko la Amani na wagonjwa, majeruhi wote tunawaombea mpate hafueni mapema.
Mko katika Maombi Yetu🙏❤️Ayubu 1:21.
Ujumbe kutoka gerezani Ukonga wa Mh. Tundu Lissu
21/11/2025
Tume za Uchunguzi ni dekio la uchafu wa serikali na Jaji Mkuu Mohamed Chande ndiye msafishaji mkuu wa uchafu huo!!
Alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Mauaji Bonde la Ihefu mwaka 2006. Matokeo yake? Sifuri!!
Alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Vyombo vya Haki Jinai Mwaka 2023. Matokeo yake? Sifuri!!
Sasa ni Mwenyekiti wa Tume ya Mauaji Makubwa katika historia ya nchi yetu yote. Tutegemee matokeo gani? Sifuri!!
Hakuna Maridhiano bila Ukweli na Uwajibikaji!
Hakuna Amani bila Haki.
TAL, Ukonga Central Prison.
-Admin.