Nataka nitumie muda wangu mwingi nimfahamu 50 Cent, nijue zaidi kuhusu huyu mwamba.
Jamaa ana akili sana, naweza kusema kuliko wasanii wote wa Marekani ukimtoa Kanye West.
NB: Hiyo ni kwa upande wangu.
50 Cent akiwa anakuchukia, huwa ana sababu nzuri ya kukuchukia, na huwa hajifichi, anakuchana ukweli.
Hajasoma sana lakini ana akili mno.
Kuna kipindi kuna mwanamke alisema alibakwa, ni kesi ya kishenzi sana, akataka kulipwa mamilioni ya dola, kesi ikaenda mahakamani na Cent akaonekana hana hatia.
MEN ONLY!!👊
Huu Ndio Ukweli Mchungu Kuhusu Maisha
Ukweli Mkali Usiokwepeka Wa Maisha Ya Mwanaume
Ukweli Wa Mambo Ambayo Wanaume Hujifunza Wakiwa Wamechelewa Sana
Learn Or Perish
NB. Na Mwanamke Anaruhusiwa Kusoma Huu Uzi.
//THREAD//UZI//
Shuka Nayo Kwenye Coment...↓
Amini hii chukua kutoka kwangu kuwa wapo Wanetu walikataliwa na Ndugu zao halafu dunia ndio ikageuka Mzazi wao, hawana wa kumpigia simu kumwomba msaada wowote, hawana wa kumlilia zaidi ya kujilalia na kuamka kupambana, mitaa imewalea na mioyo imekufa ganzi.
Unaona nini ukimtazama Mwanetu aliyeomba saana ajira na kutuma sana CV lakini wanazitazama kama TV? Wanangu hawajachoka kujaribu, Wanangu wameuza vitu vingi ghetoni ili wasafiri mbali kujaribu maisha ila kila kitu kimefeli.
Unaona nini ukimtazama Mwanetu ambaye ni Yatima? Mali zote ndugu waligombania, Mama akakosa nafasi na Watoto wakakosa jasho la Baba yao, kutoka Watoto wa mwenye pesa mpaka Watoto wa Mjane asiye na kesho, Wakike wakauza utu wao na wakiume wakageukia dili haramu ili Mama aishi.
Champion mwingine unamwona? Unamtazama Mshindi pale, tumaini lake kahamishia kwenye betting, furaha yake ni matatizo yake, ameshagonga sana milango ila walituaminisha hakuna fursa, Wazazi waliuza kila kitu ili asome na sasa wamepoteza kila kitu na Msomi karejea home bila tumaini la kweli.
Waona nini ukimtazama Kijana jioni hii? Anapiga Bodaboda ila ndani kafungia degree yake, anasaga juice na ndani kafungia Masters yake, anatembeza mitumba na ghetto lina Diploma yake,
Elimu sio ufunguo wa maisha tena bali chanzo cha kupoteza muda na kuchelewesha kesho zetu.
Maisha yamekuwa magumu na tumaini letu kubwa kama la Musa na Israel kuwa tutafika Kanaan, kuna tuliowapa proporsal zetu wakageuza kuwa zao na simu hawakupokea tena! Tunawaomba watuunganishe na Maboss wanatukatia waya wanahofia uwezo wetu, Champions wapo mitaani wanaishi kwa tumaini.
Wanangu Mimi bado hawajakata tamaa, wanalazimisha sana vitu vitokee! Wapo Mawinga Pale Kariakoo, wapo wenye viduka vyao wanakimbizana na TRA, wapo Wanangu ni Washindi wanajaribu Depo Jeshini, wapo Wanangu wanaenda kujaribu Jeshi la Police, wapo Wanangu wameacha ndoto zao ili kuishi maisha ya ndoto za wengine.
Wanangu mimi nawatazama nawaona ni Washindi, hatuna Ndugu popote pale, shida zimetufanya tuwe sugu, mpaka mwisho Wanangu! PLEASE LETS GO HARD, DONT GO HOME PLEASE.
KATIBU.
BABU ALISEMA…
"Kabla haujafanya maamuzi kwanza inabidi umueleweshe kuwa umemuoa, ameolewa, na sio mmeoana"
Aliongea kwa sauti ya chini sana, na alishajua sijamuelewa, ama sijasikia asemacho. Babu akaendelea.
"Wapo wanawake wanataka kuwa na ndoa, wengine wanahitaji kuwa👇