@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
“Kumekuwa na majaribio na vitisho kutoka kwa watawala kunizuia nisiongee. Kuna wakati niliambiwa nizime simu yangu, nisiitumie mpaka (wao) watakapo niambia. Nikawauliza, kwa sheria gani? Kuna wakati nilikaribishwa mahali fulani, nikapigiwa simu na watawala, wakasemam mzee usiendee kwenye huo mkutano. Kwanini? Hauna manufaa. Nikawauliza, nani anaamua hayo manufaa? Nikakataa. Wakawafuata watu walio karibu na mimi ili wanishawishi nisiende, nikakataa pia. Mnakumbuka nilifanya mahojiano hapa na Jamhuri? Wakatoa summary, wakasema watachapisha mahojiano yote, neno kwa neno. Baadae Jamhuri wakanieleza wamezuiwa wasitoe yale mahojiano. Kuna viongozi wanaogopa kuzungumza na mimi, wanatuma ujumbe kupitia mbali huko. Marafiki zangu wanaogopa wakisema nitatekwa au kupewa sumu. Nawaeleza mimi ni mali ya Mungu, ndiye atakayeamua lini ananihitaji.”
— Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Tanzania.
Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crowne.
Fikiria kijana ambae ameanza maisha hapa Dar, kutokana na adha ya usafiri anajibana ananunua kagari ka usd 6,000 ambazo ni sawa na 14 m.
Hiyo gari ikifika inatozwa ushuru mwingine wa 14 m, yaani fikiria ushuru unalingana na ununuzi wa gari!!!
Yaani gari Machuma yote, engineering iliyopo pale kwenye gari unanunua bei sawa na ushuru wa mtu ambae amekaa ofisini tu na anakuchaji hela yote hiyo!!!!
Wakati mwingine kodi zinakua bei juu kuliko manunuzi!!!!
Huyu kijana awe mkulima au mfanyakazi, anafanya kazi ngumu sana kupata hiyo fedha, then inachukuliwa hivi…
Alafu baada ya mda CAG anasoma ripoti kwamba uwanja ulitakiwa kujengwa kwa bilioni 187 baadae ukajengwa kwa bilioni 337..
Mara umekaa unaambiwa kuna eti Waziri anatumia gari binafsi ya bilioni 2, unajiuliza mtumishi wa umma ametoa wapi bilioni 2 kununua gari na mshahara wake unafahamika, au anamiliki nyumba tano za thamani ya bilioni tatu, nne au tano… aniliki mashamba ya mabilioni, amempa mama mkwe wake nyumba ya bilioni tano na gari la kutembelea la milioni 500.
Pesa zote hizi za mlipa kodi anaeumizwa kiasi hiki na mzigo wa kodi…
Hapa nimesema magari tu, Ukienda kwenye kila kitu kinachoingizwa na kutoka Nchini ni mzigo wa kodi na maumivu kwa Mwananchi..
Na mwisho wa siku badala hizi fedha zitumike kwaajili ya maendeleo yetu zinaishia kwenye mifuko ya vibaka.
Hakuna barabara, hakuna maji, hakuna umeme.. Maisha magumu , mishahara duni hasa kwa walimu na manesi.
Hatuwezi kukubali kuwa watumishi wa vibaka wanaopora mali za umma.
mimi pia nawasihi watanzania, wanaoweza, waichangie chadema. tunafaidika moja kwa moja tukiwa na upinzani imara, unaoweza kuishika mapembe ccm na serikali yake, hususan kwenye sera na matendo yake ya kionevu na kikandamizaji dhidi yetu w'nchi. tujihimu: