๐จLeo sisemi sana hapo mjini Gemini upload picha yako kumbuka ku edit sehemu ya country weka nchi unayoshabikia kombe la dunia.
Kisha tukutane kwenye comment section.
๐๐
An ultra-realistic portrait of a man wearing the national team [COUNTRY] jersey, ripped jeans, sporty sneakers, aviator sunglasses, and a rounded smartwatch. He is sitting leaning against a wall, head slightly tilted, calm and cool expression, one leg stretched out in front, one leg bent, hands resting on his knees.
Next to him there is a World Cup trophy and a scarf lying on the floor. The background is a wall covered with posters and graphic designs of the national team [COUNTRY], shiny wooden floor.
The shot is taken from a low angle, the legs looking big and dominant in the foreground. Cinematic composition, slightly tilted framing.
Dramatic lighting focused on the subject creating a vignette, vibrant color tone, high contrast, sharp details, high resolution, 8k, ar 2:3.
Ningekuwa naweza kuelezea vizuri ningekuwa nafanya contents anazofanya huyu jamaaa!!!
Cause haipiti siku sijaangalia series au movie moja.
Haya sikiliza story ya "The Gray 2026"
Tambala moja kali saana!!
Video kwa Comments ๐
STORY YA KWELI
Huyu binti bhana, alikuwa anaishi kwa mama yake na wadogo zake wawili. Akiwa na miaka 26 alikutana na huyu mkaka ambaye alikuwa amemzidi miaka 5. Jamaa alikuwa mtu wa kawaida tu akifanya biashara zake ndogo ndogo na binti alikuwa ametoka chuo yupo nyumbani. Basi wakaanza mahusiano.
Katika muda wa mwaka mmoja na nusu pamoja, jamaa akafanikiwa sana kibiashara, akaanza kwenda China na Dubai kuchukua mizigo mwenyewe, akanunua magari mawili na kutafuta apartment mpya ya kupanga. Siku ya kuhamia binti akaenda kumsaidia kusimamia usafi huku jamaa ameenda kufuata samani zake.
Basi jamaa akarudi na gari, wakaanza kushusha. Baada ya vitu vyote kushuka, jamaa ndio akashuka akiwa amevaa kanzu na kofia huku ameshika fimbo (mkongojo) zile za kutembelea za kuchongwa na miti. Ameishika kama mtoto aliyelala akitembea taratibu asimuamshe. Alipofika ndani akaitundika ukutani, akamgeukia binti akamwambia, huu ni ulinzi wangu, nilipewa na wazee wangu kuwa itanilinda.
"Sasa ina ulazima gani kukaa sebuleni?"
Akamjibu, Hapa kuna mlango wa kuzimu.
Kwa sababu ilikuwa busy day, binti akapuuzia wakaendelea kupanga vitu.
Alivyorudi nyumbani akamwambia mama yake jinsi gani ana wasi wasi na jamaa sababu hajawahi muona amevaa kanzu wala kwenda msikitini na mazingira yote. Mama yake akamwambia, ingawa jamaa alikuambia alikuwaga mkristo akabadili, mwambie asilimu tena na akuoe sababu mmeshakaa almost two years.
Basi binti akamwambia jamaa, jamaa akawa yupo tayari kusilimu but sio kuoa. Wakavutana kwa muda mpaka wakaachana kama mwezi hivi. Mara ghafla jamaa akarudi akakubali kusilimu na akamuoa ndani ya siku 4 bila kuchangisha michango yoyote kila kitu aligharamia mwenyewe.
Usiku wa Honeymoon jamaa akamwambia binti, Unajua kwa nini nimerudi kukuoa? Sababu una nyota kali sana siwezi bila wewe.
Basi maisha yakaanza na kila kitu kikawa sawa mpaka binti aliposhika mimba mwezi tu baada ya ndoa.
Jamaa akaanza kubadilika, akaanza kulala mzungu wa nne na kupunguza ukaribu na binti. Binti nae mimba haikumpenda, so toka mwanzo mpaka mwisho alikuwa anatematema kila siku na kuumwa umwa sana.
Basi tumbo likaanza kuchomoza, siku hiyo jamaa anatoka kazini, akamkuta binti yupo mtupu chumbani amejilaza, akafoka sana na kumuambia
'kuanzia leo sitaki kukuona ukiwa uchi na nitakuwa nalala chini'.
Basi wakagombana sana lakini jamaa akasimamia maamuzi yake. Na toka siku hiyo kila siku binti akawa anajitanda hata akitaka kuoga anaenda kuvulia nguo bafuni.
Binti anasema, toka apate mimba hakuwahi kuguswa tena kimapenzi na mumewe na akawa analala chini sakafuni.
Siku moja anamuona jamaa anaamka usiku wa manane anaenda sebuleni. Mara nyingi hufanyaga hivi but binti hudhani labda anaenda kunywa maji. Lakini hii siku moyo ukamuambia mfuate.
Akamfuata taratibu nyuma. Akamuona amechukua kikopo cha Asali, anapaka ule mkongojo ambao umeuning'iniza sebuleni huku anaongea maneno kwa sauti ndogo. Binti akarudi kitandani akajifanya kalala mpaka asubuhi jamaa alivyoondoka akaenda kuangalia akaona kweli mkongojo una natanata kama umepakwa asali.
Hakumuuliza kitu, siku ya pili pia alivyosikia anaamka akamfuata akagundua kila usiku wa saa 8 huamka kuupaka mkongojo asali.
Hapo ndipo binti akaanza kujiuliza, kwani nimeolewa na mtu wa aina gani??
Akaanza kupekua ndani kote akakuta kikapu cha kusukwa mahali. Ndani yake kuna vifundo vitatu, cheusi, cheupe na chekundu, asali, mizizi miwili na kaniki moja iliyokuwa imekunjwa kufunika kwa juu.
Akamsubiri mumewe aje na kumuuliza, kwani haya makolokolo ya nn? Jamaa akaanza kufoka kwanini unafungua vitu vyangu brah brah but mwisho wa siku akampooza kwa kumwambia ulikuwa ni ulinzi kwa ajili ya biashara yake.
Mpaka hapo jamaa bishara zake zipo juu kiasi kwamba akirudigi nyumbani hurusha burungutu za hela tumboni kwa mkewe kama mtu anayetunza kwenye sherehe, then binti ndo anazikusanya na kuzihifadhi.
Kesho yake binti akafungua kikapu tena akagundua mizizi imetolewa, akachukua vitu vyote mule ndani akaenda kuvichoma..
Itaendelea
Thread ๐งต Tuhuma kutoka kwa Mshabaha kwenda kwa Buyobe, maelezo ya Hilda na Majibu ya Buyobe
Uwezo wako wa kusoma tuu, hakuna kusogelea Telegram ๐๐๐ฝ
Leo imefanyika misa ya kumuaga Padre Peter Rwezahura, CMF aliyepotea mwaka jana na mwili wake kupatikana juzi tar. 12 May 2026 jijini Dar es Salaam.
ANAANDIKA @MalisaGJ_
Tarehe 2 February 2026, Mkuu wa Shirika la Moyo Safi wa Bikira Maria (CMF), Fr. Joy Mampilikunnel alitoa taarifa ya kupotea kwa Fr. Peter Rwezahura ambaye hadi kufikia mwezi February mwaka huu alikuwa hajaonekana kwa zaidi ya miezi 6.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jitihada mbalimbali za kumtafuta zilikuwa zimefanyika kwa kushirikiana na vyombo vya dola lakini hazikuzaa matunda, hivyo Kanisa liliamua kuujulisha umma ili yeyote atakayemuona aweze kutoa taarifa.
Hata hivyo hapakuwa na taarifa nyingine rasmi kutoka kanisani juu ya kupatikana kwa Padre huyo hadi juzi tar. 12 May 2026 ambapo uongozi wa shirika hilo ulitoa taarifa fupi kuwa Fr. Rwezahura amepatikana akiwa tayari amefariki dunia, huko jijini Dar.
Taarifa hiyo ilisomeka: โIt is with deep sorrow that we share the passing of our brother, Peter Rwezahura. We have received information that he was found deceased in Dar es Salaam, and his body has been taken to the mortuary. Fr. Abel visited the mortuary earlier and confirmed that it is indeed his body.
We are currently engaging with the authorities to proceed with the necessary formalities. Further details will be communicated as soon as they are available. We kindly ask you to keep the departed soul of our brother in your prayers. May his soul rest in eternal peace.โ
Hata hivyo hakuna taarifa zilizo wazi juu ya maiti yake ilipatikana wapi, na kama ilikuwa na majeraha au la.
Padre Peter Rwezahura, CMF alizaliwa tar. 23 March 1976 katika kijiji cha Rwamashonga mkoani Kagera. Baada ya kumaliza kidato cha sita, alipata wito wa Upadre na alichagua kufanya utume wake kupitia Shirika la Moyo Safi wa Bikira Maria maarufu kama Claretian Missionaries (CMF). Mwaka 1998 alijiunga na kituo cha malezi cha shirika hilo kilichopo Makoko, Musoma hadi mwaka 2000.
Mwaka 2000 alihamishiwa nchini Uganda kwa ajili ya Novisi na tarehe 9 July 2000 aliweka nadhiri za kwanza (temporary vows) za utume wake. Mwaka huohuo 2000 alijiunga na Chuo Kikuu Kishiriki Jordan kwa shahada ya kwanza ya Falsafa (Bachelor Degree in Philosophy) na kuhitimu mwaka 2004. Mwaka 2004 aliendelea na shahada ya Theolojia (Bachelor Degree in Theology) chuoni hapo.
Tar. 21 October 2006 aliweka nadhiri za maisha (Perpetual vows) katika Shirika la Moyo Safi wa Bikira Maria (CMF). Tar. 20 October 2007, alipata daraja la Ushemasi. Alirudi Jordan kuendelea na masomo na kuhitimu mwaka 2008.
Tarehe 24 May mwaka 2008 alipata daraja takatifu la Upadre katika Parokia ya Maria Mtakatifu, Kimara jijini Dar. Alianza utume wake katika Parokia ya Maria Mtakatifu, Kimara kama Paroko Msaidizi mwaka 2008 hadi 2009.
Mwaka 2009 alitumwa katika nyumba ya malezi Makoko Musoma kuwa mlezi wa miito. Alitumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2011 alipotumwa Roma kwa masomo ya Uzamili ya Saikolojia (Masterโs Degree in Psychology) katika Chuo Kikuu cha Gregorian ambapo alihitimu mwaka 2014. Alitumwa tena chuoni hapo kwa shahada ya uzamili ya Theolojia ya Maadili (Masterโs Degree in Moral Theology) na kuhitimu mwaka 2016.
Alipohitimu alitumwa katika nyumba ya malezi ya shirika la Moyo Safi wa Bikira Maria (CMF) iliyopo Jinja, Uganda kama mlezi mkuu. Mwaka 2017 aliteuliwa kuwa Msaidizi wa Mkuu wa Shirika hilo kwa Kanda ya Afrika Mashariki, nafasi aliyoitumikia hadi mwaka 2020.
Mwaka 2020 alitumwa kuwa Mhadhiri wa Saikolojia katika Chuo cha Queen of Apostles Philosophy Center (PCJ) kilichopo Jinja nchini Uganda. Mwaka 2021 aliteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya Mt. Anthony wa Maria Clareti, maarufu kama Parokia ya Michungwani, iliyopo Kimara jijini DSM. Alihudumu katika parokia hiyo hadi mwaka 2024.
INAENDELEA ๐๐